UKAWA mbona kimya kuhusu ufisadi na mafisadi?

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,286
Reaction score
6,727
Nanukuu gazeti la HABARILEO

"UKIMYA wa wanasiasa walioongoza harakati za kupambana na ufisadi katika majukwaa ya kisiasa, wakati huu Serikali ikichukua hatua za wazi na haraka kukabiliana na ubadhirifu wa mali za umma, umeibua maswali kuhusu uzalendo kwa nchi yao.

Miongoni mwa wanasiasa waliohusishwa na maswali hayo ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Mhadhiri Mwandamizi wa Masuala ya Siasa na Utawala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Benson Bana, alisema kama kweli ni wazalendo, ni vyema wale wote waliokuwa wakipinga ufisadi wajitokeze hadharani, kupongeza hatua zinazoendelea kuchukuliwa".

Nami naongezea "magwiji wa kuzungumzia ufisadi - Lissu, Mnyika, Mdee nk" mko wapi kumuunga mkono Rais hata kwa kumpa majina ya mafisadi, au ndo mmefungwa
Midomo!
 
Aghhhhhhhhhh!!! hili jiwe acha na mie nilikwepe, linaelekea kumtoa mtu chongo
 
waseme nini, wamepigwa butwaa. hawakutegemea jpm atayafanya anayofanya. kumbuka waliwalaghai hasa vijana kwamba hata malaika akijiunga ccm atageuka na kuwa shetani, tatizo mfumo. sasa jpm hajatoka nje ya ccm bali ndani. kumbe ndani ya ccm wapo watu safi wapo malaika ambao waweza ongoza taifa letu kwa ufanisi mkubwa.
ukimya wao pia unatokana na uwepo wa el kwenye kambi yao, mtu ambae walimshutumu kuwa fisadi papa kwa muda mrefu. sasa ndo wanatambua makosa waliyofanya kumkaribisha. roho zinawasuta. nawashauri wamtafute lipumba atawapa ushauri nasaha.
 
wanaona aibu saivi, lowasa asingeweza fanya haya anayoyafanya JPM, tusubiri labda bungeni watasema nini,,
ila nakumbuka walisema et hawatambui matokeo ya urais, hivyo hata hawamtambui JPM labda ndo maana hawamzungumzii, jamaa mapumba kweli kweli. au makontena yanawahusu pia labda ndo maana wapo kimya
 
Ila Sisiem ndio haipo kimya, he he hee! Na mtakoma maana wafanyabiashara waliokuwa wanachanga fedha sasa wameshakoma na kujuta, kwani michango yao haijathaminiwa kabisa
 
Nanukuu gazeti la HABARILEO

"UKIMYA wa wanasiasa walioongoza harakati za kupambana na ufisadi katika majukwaa ya kisiasa, wakati huu Serikali ikichukua hatua za wazi na haraka kukabiliana na ubadhirifu wa mali za umma, umeibua maswali kuhusu uzalendo kwa nchi yao.
Mbona rais wa nec anatekeleza walichosema hao unaowaita wapinzani, habarileo mbona hawawadai CCM kuhusu kupambana na rushwa?

Miongoni mwa wanasiasa waliohusishwa na maswali hayo ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Mhadhiri Mwandamizi wa Masuala ya Siasa na Utawala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Benson Bana, alisema kama kweli ni wazalendo, ni vyema wale wote waliokuwa wakipinga ufisadi wajitokeze hadharani, kupongeza hatua zinazoendelea kuchukuliwa".

Nami naongezea "magwiji wa kuzungumzia ufisadi - Lissu, Mnyika, Mdee nk" mko wapi kumuunga mkono Rais hata kwa kumpa majina ya mafisadi, au ndo mmefungwa
Midomo!

Serikal ya Magufuli si serikali ya CCM inapambana na mafisadi waliopo CCM; hatujasikia fisadi lo lote toka upinzani limeshughulikiwa kwenye kadia hii.
 
Wana ccm,hatuna shukrani.Hivi hawa si ndiyo tuliwaona wajinga walipokuwa wakikemea madudu ya serikali? Jpm akashawishika na sasa anatumbua majipu,why tunafanya siasa za kijinga kutetea wezi pindi upinzani unapowaumbua.Leo unawatukana hao ambao walitetea wanyonge.Acheni unafki Nchi hii inajengwa na watanzania na si ccm peke yao.
 
Huu ni wakati wa kutenda na mtendaji ni yule mwenye serikali. Magufuli vipi kuhusu ufisadi?
 
Kwa nini sisiem ilikuwa kimya wakati wapinzani wanazungumzia ufisadi?
 
Yaani aliyepost hapa ni mat....a...ako kweli kweli, sasa unataka waseme mini wakati Magufuri anatekeleza ahadi na Ilani ya UKAWA.
 
Huyu bana akili zake sijui anaziachaga wap? Ss unataka wafanye nn? Wao wanamsubir maguful atumbie majipu waliyoyatengeneza ak?na lordlofa na mkwele, afu yale aliyoshindwa ataulizwa kwann hajatumbua na hapo na huo ndo wajibu wa wapinzan. Ss huyu mtu na akil zake zote anataka wapinzan waimbe nn? Je kama rais anaigiza? Unataka waingie kwenye huo mkenge? Na was was na uwezo wake wa kufikil licha ya kuwa yeye ni prof.
 
Uloi nga mâché68;14800603 said:
Chadomo wameumbuka. Hawana sera tena. Wamebaki kufanya siasa kwenye misiba tu. CCM mna akili kama kuku wakati wa JK, kina Mnyika hadi walitolewa nje ya bunge nanyi mkabeza. Sasa maneno yaleyale mnapayuka, machizi nyie
 
Wakati CDM inapambana na ufisadi SISIEM ilikuwa ikiutetea,
Sasa rais anapambana nao ufisadi SISIEM wapo kimya,

CDM waseme nni wakati wanalolitaka linatekelezwa

Mim najua wanavutia kinyesi ndan kwao sasa wote wameziba poa
 
Serikal ya Magufuli si serikali ya CCM inapambana na mafisadi waliopo CCM; hatujasikia fisadi lo lote toka upinzani limeshughulikiwa kwenye kadia hii.

Rejea posts za Zitto. Makontena yote yaliyokamatwa ni ya wafadhili wa ukawa. Bado fisadi la Richmond na sakata la bilicanas. Miungu yenu inatupwa kuzimu soon
 
hivi wapinzani au ukawa watakuwa waajabu sana kama wataendelea kupiga kelele kuhusu utawala wa MAGU wakati anatekeleza kile walichokuwa wakikipigia kelele kila siku!! itakuwa ajabu sana
 
Nanukuu gazeti la HABARILEO

"UKIMYA wa wanasiasa walioongoza harakati za kupambana na ufisadi katika majukwaa ya kisiasa, wakati huu Serikali ikichukua hatua za wazi na haraka kukabiliana na ubadhirifu wa mali za umma, umeibua maswali kuhusu uzalendo kwa nchi yao.

Miongoni mwa wanasiasa waliohusishwa na maswali hayo ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Mhadhiri Mwandamizi wa Masuala ya Siasa na Utawala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Benson Bana, alisema kama kweli ni wazalendo, ni vyema wale wote waliokuwa wakipinga ufisadi wajitokeze hadharani, kupongeza hatua zinazoendelea kuchukuliwa".

Nami naongezea "magwiji wa kuzungumzia ufisadi - Lissu, Mnyika, Mdee nk" mko wapi kumuunga mkono Rais hata kwa kumpa majina ya mafisadi, au ndo mmefungwa
Midomo!

Naomba kujuzwa ubaya wa wapinzani kusema kuwa serikali ilikuwa imeoza. Walikosea? Au Mheshimiwa Magufuli anayofanya ni usanii? Kama kweli kuna hayo madudu yastahili kuupongeza sana wapinzani kwani wangekaa kimya hawa watu wasingebadilika

Yastahili basi kuwaunga mkono tuzidi kuwapa nguvu ili waiamshe serikali badala ya kubeza wanayofanya
 
Huyu bana akili zake sijui anaziachaga wap? Ss unataka wafanye nn? Wao wanamsubir maguful atumbie majipu waliyoyatengeneza ak?na lordlofa na mkwele, afu yale aliyoshindwa ataulizwa kwann hajatumbua na hapo na huo ndo wajibu wa wapinzan. Ss huyu mtu na akil zake zote anataka wapinzan waimbe nn? Je kama rais anaigiza? Unataka waingie kwenye huo mkenge? Na was was na uwezo wake wa kufikil licha ya kuwa yeye ni prof.

Na ni maigizo kweli makontena yameanza kutoka horribly wakati na baada ya uchaguzi au?Na kama yalikuwa yanatoka wapi mawaziri wenye dhamana husika??hizo ni mbwembwe tu.hamna kitu.
 
Back
Top Bottom