UKAWA kugomea Kamati za Bunge

Tarudi baadae kuchangia kiduchu...
 
Hoja zaifu sana kudai wabunge wa upinzani waliowekwa kwenye kamati hizo (PAC & LAAC) Ni wabunge wachanga na hawana uzoefu kwani bunge hili halina uhasiano wa namna yoyote na historia wala bunge lililopita na sifa ya kuwa mjumbe wa kamati au mwenyekiti kikanuni haisemi uwe mbunge kwa awamu mbili au moja, watanzania naomba mtambue wazi kuwa kinachopiganiwa ni masilahi tu na network pana ya wizi wa dhahiri na hivyo unapaswa kukemewa vilivyo.
 
Kwani sheria na kanuni zinasemaje kuhusu nani ana wajibu wa kupanga hizo kamati? Ukawa fuata sheria za bunge wakati mnasubiri kupata speaker wenu.
 

Nadhani mawazo ya wabunge wetu hasa wa kambi ya upinzani - wamefocus kuibua ufisadi na kuona matumizi ya PAC na serikali za mitaa , wakidhani ndio kazi pekee, wanaweza kuwa sahihi ila wanasahau kufahamu hizi sekta za uzalishaji ni muhimu zaidi kuliko hizo sekta za matumizi wanazozililia.
 
Majukumu ya PAC unayafahamu lakini?

Kwa namna wanavyokuwa na kuenenda wabunge wa CCM ni dhahiri kamati hii itakuwa butu na haitatimiza majukumu yake ipasavyo kama hawataweka ushabiki wao pembeni na kufanya kazi kwa maslahi ya Taifa
It's just watching expenditures, na wanainga'ang'ania PAC kwa ajili kick ya kisiasa, ila wanastahili kutuinyesha ubunifu zaidi kwenye hizo kamati za uzalishaji - kilimo, mifugo, uvuvi ambazo zinawahusu watu wengi zaidi. Naona kwa kulilia PAC ipo kibinafsi zaidi maana kamati zote za bunge zipo sawa na hakuna mbunge bora zaidi ya mwenzake.
 
Kwenye hio kamati ya PAC huwa inakuwa na wajumbe wangapi? Je akidi inakuwaje?

Kilimo na mifugo ndio uti wa mgongo wa taifa - kupitia wapinzani tunataka kuona mifugo, kilimo na uvuvi vinatutoa, kamati zingine majungu na unafiki tu.

Hizo kamati zingine zimejaa ulaji na rushwa.
 
Reactions: bdo
Naomba mnisaidie kwa wabunge wa ukawa Kama ni kutendewa haki kweli baadhi ninafahamu mfano msomi Lissu H Mdee hawa no sheria Sugu na J mziki mwenyekiti wao Mbowe Dj hawa wengine kina kubenea wanafani gani maana hata ktk habari hauumo na mnalilia kamati za???
 
ccm ni wajanja sana. wameweka wabunge dhaifa kwenye kamati muhimu za taifa letu kama nishati na madini,maliasili na utalii. nk. kiukweli wabunge hawako sawa kiuwezo na kimtazamo. hilo ni kwa vyama vyote hasa ccm. mfano wabunge wa viti maalumu.
 
Wabongo Kwa ushabiki!
 
K


Kama mlipanga kuwaburuza sasa mtakiona cha mtemakuni nyie ccccccccm, kama mlijipangia kivyenu na kuweka wadhaifu ili mambo yenu yasonge mbele kilaini huu si wakati wake. tunataka usawa na si vinginevyo. Bunge ni la wooote si lenu na marafiki zenu
Sisi wananchi tunachotaka kazi na maendeleo baassi. Mambo ya midomo. fijo, mahakamni hatutaki!!! Hapa ni Kazi tu sio ubabaishaji na visingizio kibao!
 
Pole sana Movich boy. Wasingekuwa sawa Kubenea mwenye elimu ya hapa na pale asingepata Ubunge. My point tunachotaka wananchi si mbwembwe zozote abli na kazi tu na maendeleo endapo yataletwa na Kubenea mwenye elimu ya hapa na pale sawa , endapo yataletwa na Prof. sawa waht we want ni kazi na commitment ya wabunge period!
 
ku

kumbe kuna wabunge dhaifu upinzani tulikuwa hatujui. !! ni ajabu na kweli. sasa kwa nini wananchi waliwachagua? ? napendekeza wajiuzuru kama wanakubali wao ni dhaifu kwa hiyo ni mizigo

hakuna mbunge mdhaifu upinzani wewe Babeli, ila nyie maccm ndo mnjifanya kujipa shavu kama mlivvyoshauriwa na waziri mkuu mstaafu pinda, tunajua kuna maeneo mmebana kimaslahi ila poa tu haina majoto, bunge si ndo hili liasonge mbele!!!!! tatabanana mulemule hadi kitaeleweka, endeleeni kujipa moyo kwenye hakuna tu.
 
Sisi wananchi tunachotaka kazi na maendeleo baassi. Mambo ya midomo. fijo, mahakamni hatutaki!!! Hapa ni Kazi tu sio ubabaishaji na visingizio kibao!
Najua tunataka maendeleo, maisha bora na mambo kama haya , Lakini si kwa staili ileile ya kihafidhina mkuu. Kila mtu anastahili kupata anachostahili mwingine. Sjui kama umenipata!!! wabunge wetu wanayo stahiki sawasawa na ile ya wale wa ccm, sasa kama umefuatilia kwa karibu kilichoanza pale mjengoni ni ama kuna mtoto wa tumboni na wa mgongoni wakati mama yetu ni mmoja.
 
Narudia tena hawa wabunge wa ukawa ni wajinga maana wabunge wote wanahadhi sawa hakuna mbunge mwenye thamani kuliko mwingine.
 
Tatizo Hao wabunge wa ukawa wamepewa vichwa na wafuasi wao nyumbu sasa wakajiona ya kuwa wao ni muhimu na wao ndiyo wenye haki ya kupewa priority kila kitu. Wanajiona wao tu wenye elimu wakati wengi wao rcord zao za shule zinaoneka na upeo wa wa kufikiri ni mdogo sana lakini kinachowasaidia ni madomo kaya na hawa nyumbu wetu wakiona hivyo ndiyo wanapagawa kwa kuwamwagia sifa kem kem. hata wakigoma haitosaidia kitu kwani speaker ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho au wataenda mahakamani??..
 
Fani ya Mnyika ni nini kaka?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…