UKAWA itisheni maandamano ya nchi nzima kupinga ukatili wa polisi dhidi ya raia

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Niseme tu ukweli kwamba polisi kwangu ni adui yangu namba moja. Nikiwa katika shida na ninahitaji msaada wa polisi sijawahi kuupata. Tuliwahi kuingiliwa na majambazi tukapiga simu polisi, walikuja dk tano baada ya majambazi kuondoka - hapa naongelea majambazi waliokaa ndani kwa zaidi ya saa moja, na simu ilipigwa polisi wakati wakianza tu kuvunja mlango.

Niliwahi kupata ajali ya gari, polisi wa Mkuranga wakanidai laki tatu ili waweze kuja kukagua ajali na kuchora michoro ya ajali. Nilipojaribu kuonyesha kwamba sikuwa na hela, waliniacha hapo kwa siku nzima hadi nilipolipa laki mbili na nusu, ndipo walikuja.

Haya ni matukio ambayo yamenipata mimi binafsi, sijui wengine wameshakutana na matukio ya namna gani dhidi ya polisi. Naweza kusema, sijawahi kupata msaada wowote wa maana kutoka polisi zaidi ya kunikomalia niwape rushwa nikikutwa na kosa la barabarani.

Sasa ninapoona uwezo wa polisi kuwashughulikia watu wanaoandamana kwa amani namna hii, huku wakiwa hawana uwezo hata wa kukamata jambazi au kushughulikia wauaji wa albino, napata shida kuelewa. Ninaposikia maandamano yamezuiwa kutokana na taarifa za kiintelijensia huku hatuoni hao intelijensia wakipata habari juu ya matukio ya ujambazi na mauaji, sielewi somo kabisa. Hii ni hali isiyo ya kawaida na isiyovumilika.

Kwa tukio hili lililompata Lipumba, ni wakati mzuri sasa wa kuitisha maandamano ya nchi nzima kupinga ukatili mkubwa wa polisi ambao hauna manufaa kwa watanzania zaidi ya ukandamizaji wa kutisha. Haya yaliyompata Lipumba, yanakuja pia kwa Mbowe na Mbatia, na zaidi sana watanzania wa kawaida ndiyo wanakabiliana nayo kila kukicha, lakini hawana mahali pa kusemea.

Ni sheria gani ya nchi inayozuia maandamano? Kama kuandamana ni haki ya raia kikatiba, kwanini maandamano yazuiewe kwa nguvu kubwa kiasi hiki? Ni lini maandamano ya CCM yaliwahi kuzuiwa kwa namna yoyote ile? Hivi hizo taarifa za kiintelijensia huwa zinawahusu wapinzani tu? UKAWA itisheni maandamano, nitakuwa mstari wa mbele kushawishi watanzania wahudhurie kwa wingi maandamano hayo. Tumechoka watanzania kunyanyaswa na polisi, tumechoka kuwa na jeshi lisilokuwa na msaada kwetu.
 
mkuu hao ndo polisiccm intelijensia yao inafanya kazi kwenye maandamano ya amani ya vyama vya upinzani
 
Back
Top Bottom