Kama hii kauli ni ya kweli basi ni habari mbaya kuliko zote. Chama huwa kina anzishwa kwa kuanagalia vilivyopo vimeshindwa kutekeleza itikagi au malengo Fulani. Kweli Mwigamba, Mkumbo na wengine mnaanzisha chama cha kupambana na Chadema, ina maana Chadema ikifa basi na nyinyi chama chenu kinakuwa mfu? Hivi kweli Dr>Mkumbo na Phd yako nzima tena sijui ya saikoloji unaanzisha chama sera yake kuu na ambayo ya kificho ni kupambambana na Chadema. Chukuwa mfano huu kutoka kwa Malkia, Labour ni chama cha wafanyakazi kule Uingereza sera yao kuu ni kutetea wafanyakazi kwa kila jambo, Conservatives wao ni watetezi wa mabepari wenye viwanda,mashamba nk. Liberal wao wakaja wakaamua kukaa katikati. Miaka ya 1990s ilianzishwa UKIP..UK Independent Party ili kupinga UK kupata amri na maelekezo kutoka Euro, watu wengi waliwadharau kama wapiga kelele na kuwabatiza kuwa ni wabaguzi, sasa uchaguzi wa bunge la ulaya uliofanyika mwezi uliopita wamepata Wabunge wengi kuliko vyama vyote vikuu vya Uingereza.
Natoa mfano huu kwa kutaka kuonyesha siasa za agenda na siasa za mnyukano, Kizazi cha sasa kinazidiwa mbali mno na wazee wetu wakina Mtemvu pale alipotofautiana na TANU kuhusu suala la kura tatu yeye alianzisha ANC kwa ajili ya kutetea Waafrika na wala sio kupambana na TANU.
Kwa malengo haya ya ACT- Mkumbo, ZZK, Mwigamba, Lembu na wengine bado sana...hamjanishawishi kuwafuata