UKAWA Hawajiamini Na Hawana Makubaliano Ya Uhakika..

UKAWA Hawajiamini Na Hawana Makubaliano Ya Uhakika..

Tony antony

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
4,988
Reaction score
3,270
habari wanaforum.. kuna hz taarifa za mkanganyiko kwamba UKAWA ishampata rais wakati huohuo gazet la jana la mwananch kupitia naibu katibu wa CHADEMA Salum Mwalimu Linasema Kua Hakuna Mwananchi Aliyechukua Fomu Ya Kugombea Urais Had Trh Ya Mwsho Ya Kurudsha,hvo Wamesogeza Had Trh 31.Sasa Nashndwa Kupata Jibu Hz Taarifa Za Kua Rais Kashachaguliwa Na Huku Hakuna Alyechukua Fomu Inakuaje Hii? Pia Najaribu Kujumuisha Na Taarifa Tofaut Tofaut Zinazotolewa Na CUF na CHADEMA.Mara Cuf Inasubiri Uamuzi Wa Chadema Mara Chadema Nao Wanadai Wanasubiri Cuf Ifanye Kikao Chao...Huku Msemaji Wa Ukawa (Mwkt Wa NCCR) Akiutangazia Umma Itamtangaza raisi wao baada ya siku 7,najiuliza siku 7 hazijapita kweli? kwa uelewa wangu mdgo wa siasa naweza nikasema UKAWA ikiongozwa na CHADEMA hawajiamini kwa wanachokifanya.na kama kweli wanamsubiri lowassa hv tujiulize lowassa angechaguliwa kule CCM kua raisi inamaana UKAWA isingetoa mgombea uraisi?Mm Nahisi Hawa UKAWA Wajipange Tena!!
 
Hata mi leo wameniboa... kama hawajiamini bora kunyamaza kwanza mpaka wamalize mambo yao
 
magufuli kawavuruga mpaka wamegairi kuwasimamisha kina slaa lipumba na mbatia. polen mnasubir sahihi y fisadi. na lazima oktober mchapwe tu
 
mambo mazuri hayataki pupa,

"This is a plan"
 
Mliambiwa mwali atatolewa kwa ngoma, nderemo na vifijo. Istoshe tukio hilo la kihistoria litakuwa kwenye luninga moja kwa moja. Muweni na subira ngoma zinawambwa
 
mambo mazuri hayataki pupa,

"This is a plan"
That is true, kwenye politics kuna tactics nyingi inabidi zitumike.

Ukawa wanacheza hiyo game ya siasa kwa umakini mkubwa, hasa wakizingatia timu yao pinzani wanayopambana nayo CCM ni timu yenye kucheza 'faulo' nyingi uwanjani, na hata hiyo delaying tactic ni miongoni ya mbinu wanazotumia.

Tukumbuke kuwa msemaji wa Chama cha CCM Nape, alitamba waziwazi kuwa for hooks and crooks lazima watalazimisha ushindi hata ikibidi kufunga kwa goli la mkono!

Kwa mazingira hayo Ukawa nao wanalazimika kuchukua extra precaution ili kuhakikisha kuwa goli alilotamba nalo Nape kuwafunga Ukawa halifungiki.
 
habari wanaforum.. kuna hz taarifa za mkanganyiko kwamba UKAWA ishampata rais wakati huohuo gazet la jana la mwananch kupitia naibu katibu wa CHADEMA Salum Mwalimu Linasema Kua Hakuna Mwananchi Aliyechukua Fomu Ya Kugombea Urais Had Trh Ya Mwsho Ya Kurudsha,hvo Wamesogeza Had Trh 31.Sasa Nashndwa Kupata Jibu Hz Taarifa Za Kua Rais Kashachaguliwa Na Huku Hakuna Alyechukua Fomu Inakuaje Hii? Pia Najaribu Kujumuisha Na Taarifa Tofaut Tofaut Zinazotolewa Na CUF na CHADEMA.Mara Cuf Inasubiri Uamuzi Wa Chadema Mara Chadema Nao Wanadai Wanasubiri Cuf Ifanye Kikao Chao...Huku Msemaji Wa Ukawa (Mwkt Wa NCCR) Akiutangazia Umma Itamtangaza raisi wao baada ya siku 7,najiuliza siku 7 hazijapita kweli? kwa uelewa wangu mdgo wa siasa naweza nikasema UKAWA ikiongozwa na CHADEMA hawajiamini kwa wanachokifanya.na kama kweli wanamsubiri lowassa hv tujiulize lowassa angechaguliwa kule CCM kua raisi inamaana UKAWA isingetoa mgombea uraisi?Mm Nahisi Hawa UKAWA Wajipange Tena!!

Mbona unaandika havisomeki wala havieleweki? Kama unaimba vile!
 
JUMUIKO la vyama vinavyounda muungano wa kutetea katiba ya Wananchi (UKAWA), linatarajiwa kumtangaza mgombea wake urais jioni hii, jijini Dar es Salaam. Anaandika Saed Kubenea … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya umoja huo zinasema, mgombea urais wa UKAWA aweza kupatikana leo, baada ya mashauriano ya kina yaliyofanyika baina ya viongozi wakuu wa vyama vinavyounda umoja huo. “Jioni hii ya leo, tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwa lengo la kumtangaza mgombea wetu wa urais. Tutatangaza moja kwa moja mgombea au tutakitangaza chama ambacho kitatoa mgombea,” ameeleza mmoja wa viongozi wakuu wa UKAWA kwa sharti la kutotajwa gazetini. Amesema, “ikiwa tutakitangaza chama, basi kitakachofuata, ni kukiruhusu kuendelea na mchakato wake wa ndani. Lakini katika hayo mawili, moja lazima litafanyika, tutangaza mgombea au chama kitakachotoa
mgombea. Mkutano wa viongozi wakuu wa UKAWA unaotarajiwa kutangaza mgombea wake urais, umepangwa kufanyika katika hoteli ya Bahari Beach.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa wa gazeti hili, chama ambacho kitatoa mgombea urais wa Muungano, kimetajwa kuwa Chadema. Mgombea urais wa Zanzibar, atatoka CUF. Anasema, makubaliano kuwa Chadema ndicho kitoe mgombea urais wa Muungano tayari yameridhiwa na Baraza Kuu la Uongozi la CUF, lililokutana mjini Zanzibar jana Jumamosi. Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema, hatua ya CUF mmoja wa washirika wakubwa katika umoja huo kuridhia Chadema kutoa mgombea urais, limekuwa pigo kubwa kwa wapinzani wa muungano huo. “Haya mawili ya rais wa Muungano na rais wa Zanzibar, tayari tumekubaliana. Chadema kitatoa mgombea urais wa Muungano na CUF kitatoa mgombea mwenza. Mbali na mgombea mwenza, CUF kitatoa pia mgombea urais wa Zanzibar,” anaeleza kiongozi huyo.

Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya Chadema zinasema, chama hicho kinaweza kuzuia kumtangaza mgombea wake wa urais katika mkutano wa leo na waandishi wa habari, ili kukamilisha mazungumzo yake ya ndani. Kinachoitwa na chama hicho, “mazungumzo ya ndani,” kimetajwa na afisa mmoja wa Chadema kuwa ni suala la kuchelewa kupatikana jina la mgombea mwenza kutoka CUF. Aidha, taarifa zinasema, kushindwa kwa chama hicho kumtangaza mgombea wake urais wa Muungano, kunatoka pia na kutokamilika kwa “mashauriano” kati yake na mmoja wa watu muhimu nje ya chama hicho.”

Lakini kwa zaidi ya wiki mbili sasa, vyombo vya habari vimenukuu vyanzo mbalimbali vya taarifa vikieleza, anayesubiriwa na Chadema kutoka nje ya chama, ni mbunge wa Mondoli (CCM), Edward Lowassa. Taarifa kuwa Lowassa, mmoja wa wanasiasa machachari nchini, anataka kujiunga na Chadema, zimepamba moto katika wiki za hivi karibuni baada ya jina lake kuenguliwa katika hatua za awali katika kinyang’anyiro cha urais kupitia CCM. Tayari madiwano 20 na viongozi wengine mbalimbali wa CCM wamekihama chama hicho na kujiunga na Chadema, jambo ambalo limeashiria kukamilika kwa safari ya kiongozi huyo ndani ya Chadema.

Chanzo: MwanaHalisi Online
 
Ukawa ni matapelitapeli tuu, waganga njaa kibaoo,wamempata mbumbumbu wa kumwibia pesa zake na kisha kuendeleza utapeli wao....KWELI asili ya kitu hajifichi jamani...
 
Ukawa ni matapelitapeli tuu, waganga njaa kibaoo,wamempata mbumbumbu wa kumwibia pesa zake na kisha kuendeleza utapeli wao....KWELI asili ya kitu hajifichi jamani...

Asili ina nguvu sana mkuu na ndo maana huwa hatuhoji sana inapotokea ukaona mtu anafanya jambo fulani in lkwasababu ya nguvu ya nature
 
Back
Top Bottom