UKAWA fanyieni kazi jambo hili

UKAWA fanyieni kazi jambo hili

Papa1

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2012
Posts
2,023
Reaction score
2,218
Suala la kusimamisha mgombea mmoja kwa kile kinachoitwa UKAWA katika majimbo ya uchaguzi katika ngazi za udiwani, ubunge na hata urais ni jambo muafaka. lakini hebu fanyieni kazi jambo hili muhimu saaana.

Utaratibu wa uwakala:
Mawakala wa uchaguzi katika vituo nya kupigia kura wanaruhusiwa wale tu wenye wagombea. Chama kisicho na mgombea hakiruhusiwi kuweka wakala. Hii inamaana UKAWA wakimteua mgombea kutoka NCCR katika udiwani, katika kata husika kila kituo kitakuwa na wakala mmoja tu wa NCCR, na huyu ndiye atakuwa mlinzi wa kura za diwani huyo.

Jinsi ya kuibiwa kura kwa wakala mmoja.
1. Endapo huyo wakala akiwa mbinafsi, au mroho wa pesa anaweza kushawishiwa kirahisi akauza kura.
2. Akitoka tu kwenda haja, atakuta kura za ziada za CCM zimeishajazwa ndani ya box au box limebadilishwa.
3. Mtu mmoja ni rahisi kumbabaisha wakati wa kuhesabu kura na akapoteza kile alichotakiwa kufanya.

Kupoteza jimbo au udiwani kwa mgombea mmoja wa UKAWA na kipa CCM ushindi wa bila kupingwa
Kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza kiti cha udiwani au jimbo la ubunge katika hali ifuatayo:
1. Mgombea akitekwa na wana CCM muda mfupi kabla ya kurudisha na kuachiwa baada ya muda kuisha.
2. Mgombea akiamua kusaliti akala pesa ya CCM akaingia mitini baada yakurushwa form.
3. CCM kuweka pingamizi kwa huyo mgombea mmoja na tume ya uchaguzi ikakubaliana nalo.

Njia ya kutokea.
Kwa maoni yangu napendekeza yafuatayo:
1. Kuhusu uwakala, chama kilicho achiwa jimbo na nafasi ya udiwani kiweke wagombea wasindikizaji kwa tiketi ya vyama vingine. Maana yangu ni kwamba kama jimbo wameachiwa NCCR. mgombea halisi wa NCCR ni A. NCCR iteue wagombea wasindikizaji B ajifanye CHADEMA, C ajifanye CUF, D ajifanye NLD. wachukue form za kugombea na uongozi wa vyama vya CHADEMA, CUF, NLD wawapitishie form zao. Hawana haja ya kupiga kampeni. Watawezesha kituo kimoja cha kupiga kura kuwa na mawakala wanne. Kuwaibia kura mawakala wanne ningumu kidogo. Hii ifanyike kwa ngazi ya kata tu. katika ubunge mawakala hawa ndio watasimamia kura za mbunge.

2. Kuhusu Mgombea mmoja, kuwepo ulinzi madhubuti kwa wagombea siku za kurejesha form. Ikiwezekana awepo mgombea wa ziada wa chama kilichoachiwa jimbo. achukue form kwa ticketi ya chama kingine na apige kampeni ya kuwaomba wananchi wampigie yule mlengwa. endapo ikitokea masuala ya mapingamizi na usaliti, huyu wapili aendeleze mchezo.
​
Toa ushauri zaidi.
 
Watu aina yako papa 1 tunawahitaji ktk pambano hili tukufu, big up kwa wazo zuri, tulichambue kwa pamoja tuone kama litafaa zaidi na watu makini wengine waje na mawazo mbadala su kuboreshs zaidi
 
Watu aina yako papa 1 tunawahitaji ktk pambano hili tukufu, big up kwa wazo zuri, tulichambue kwa pamoja tuone kama litafaa zaidi na watu makini wengine waje na mawazo mbadala su kuboreshs zaidi

mtawachanganya wapiga kura,na kura zenu zitagawanyika....
 
mpango huo ni hatari,hakuna cha kuogopa,wakala ambaye atakuwa kituoni ni yule wa kuaminika
 
Papa1

Well said mkuu! UKAWA hilo hapo neno.
 
Last edited by a moderator:
Ni kama nakuelewa...umefikiri sana, at least we can tag you a great thinker
 
umefikiria mbali sana mkuu. big up sn. viongozi UKAWA chukueni wazo zuri hilo mlijadiri ktk vikao vyenu.
 
Pia si kuna issue ya kumpa mwenzio kura? So hata wakisimama wanne watatu wanampa alueteuliwa kura zao. Ilifanyika kwa Dovutwa na JK
 
Mkuu wazo lako zuri ila usingelimwaga hapa maana kuna fisi wana randaranda wanangoja mkono udondoke
 
Well said, however kunahitaji maboresho ya nawazo yako.

Mfano, kwa nini mgombea asiwe kwenye uangalizi kuanzia hatua ya kuchukua form hadi kurejesha? Sisi vijana wa UKAWA tuko tayari kujitolea kuwalinda kweli kweli wagombea wetu bila malipo na tusio na nafasi tupo tayari kuchangia fedha kuwezesha waliojitolea kufanya kazi yao pasipo kuingiwa na tamaa. Tunachohitaji ni perfect coordination & organization tu, baasi!

Jingine ninaloweza kuchangia ni kuwa, pamoja na hoja yangu hiyo hapo juu, kuna haja kubwa ya vyama washirika wa UKAWA kuhakikisha wanasimamisha wagombea walio tayari kwelikweli kutumika, wenye uchungu wa mabadiliko na wenye chuki ya kwelikweli na CCM kuliko kuteua wagombea wenye tamaa ya kuhongwa fedha ya kula labda nwezi mmoja kama akina Shibuda au ZZK na kuwaachia maumivu wananchi ya miaka mitano mbele wakiwa wamebeba lidudu baya lenye harufu mbaya linaloitwa CCM!!

Na hili liko wazi sana, kwamba kuna watu kibao tu wanaotafuta uteuzi kupitia vyama vya upinzani wakijifanya ni wanabadiliko lakini ni mamluki/mapandikizi ya CCM yameshapewa au wako ktk makubaliano ya kukatiwa mafungu ya fedha kwa mtindo ambao CCM watautumia sana mwaka huu.

Sisi huku maeneo yetu tuneshawang'amua baadhi tena yako ndani ya CHADEMA na kwa nje ni wanachama watiifu, lakini ukichunguza nyendo zao ni mbwa mwitu wanatafuta wa kumtafuna tu, wanatafuta fedha tu!!
 
Ina maana hamuaminiani ktk muungano wenu, lazima kujenga watu madhubuti ktk kuleta matokeo chanya ya muungano huu msiwekama mnabahatisha, haya mawazo ni mazuri kwa kwa watoto wenye utindio wa ubongo, hii ni kuleta au kuendeleza utengano sababu hamna haja ya ukawa sasa. lan yako hii inahitajika elimu kwa wapiga kura wenu na muda uko ukingoni huu, sina tatizo na mawazo yako ila ni mazuri kwa mataira sababu hayatekelezeki
 
Back
Top Bottom