Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Igwe wanaJF!
Nimewajibika kuandika hii hoja nikiwa na mtanziko kwanini Mbowe na Seif wanakabidhi "chungu" kwa hawa maveterani ambao hawana mbinu mpya za kivita?
Naum,Kingunge kipindi cha bunge maalum la katiba aliibuka bungeni kama "mshauri" wa waganga wa tiba asili na kimkakati akapewa muda mrefu kutoa nasaha za Muungano na kuchinjilia mbali tunu za taifa.Sina shida na idadi ya serikali bali hapa kwenye tunu ilikuwa ni mahsusi kuondoa ili kijana wake akichukua nchi asifatwefatwe..Je huyu ana uhalali wa kuanza kuponda katiba pendekezwa ya bunge la katiba?..Je akiyakana maneno yake ataaminika?...Ieleweke tu Kingunge anashawishiwa awe mlezi wa BAVICHA...Je nia ya Kingunge UKAWA ni Katiba mpya au Lowassa awe Raisi.
Ushiriki wa Lowassa katika mchakato wa kukwamisha tume umeelezewa mara kwa mara na wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Katiba kwani aliamini yeye ni Raisi ajaye..na aliitaka tume Mamlaka ya Raisi wa JMT kuhusu Zanzibar yaongezwe.Je huyu ataaminika?..Je dhumuni lake ndani ya UKAWA ni Uraisi au Katiba mpya?...Ikumbukwe kishajitangaza ndiye Mgombea wa Uraisi wa CHADEMA 2020.
Sumaye,huyu ni mjumbe wa kamati kuu chadema kama Lowassa.Huyu alikuja CHADEMA kumnadi Lowassa na kingine.Msimamo wake juu ya katika mpya ni Serikali 2.Je amebadilisha mtazamo wake kuwa serikali 3?
Kati ya wote watatu hamna hata mmoja anayefanana na maono ya UKAWA ambaye mwenyekiti wake mwasisi ndani ya Bunge la katiba ni Prof.Lipumba na Katibu wake Mtatiro.Je wanaweza kumshawishi nani juu ya katiba?
Mbowe na Maalim Seif na Mbatia ndio mliobaki na UKAWA iliyo na lengo moja tu la kupata madaraka na sio kushawishi upatikanaji wa Katiba mpya yenye maridhiano.Ni kwanini msijitumbue wenyewe?Hivi hamjui mmejidhalilisha kisiasa kwa kukubali vijihela kwa kuuza nafasi za kugombea uraisi na ubunge?
Tutoe hoja kinzani na sio matusi.
Nawasilisha