Fikrazangu
Member
- Dec 31, 2017
- 15
- 25
UKATILI WA POLISI
DHIDI YA RAIA
NINI KIFANYIKE KUTOKOMEZA?
FIKRA ZANGU
Ukatili wa jeshi la polisi dhidi ya raia
Mwanaharakati mmoja nchini Marekani kwa jina Alfred Charles Sharpton aliwahi kusema hivi;
“Many in our community have to live in fear of both cops and the robbers” akimaanisha (Wengi katika jamii yetu inatubidi kuishi kwa kuhofia maaskari pamoja na majambazi)
Hivi karibuni kumekua na malalamiko mengi kuhusu jeshi la polisi juu ya unyanyasaji. Ni kweli haya mambo yapo na baadhi yetu tumekua wahanga na mashuhuda wa matendo ya kinyanyasaji yanayofanywa na polisi dhidi ya raia. Watanzania wengi wakiwa ni mashuhuda wa vitendo hivi, mara nyingi wamekua wakikemea matendo haya ya kinyanyasaji.
Ubaguzi na kujisahau
Tatizo ni kwamba, watanzania tulio wengi tumekua tukichagua watu wa kuwasemea pindi tatizo hili linapotokea. Yani mpaka kitendo cha unyanyasaji kimkute mtu fulani maarufu ndo utakuta watanzania wanapaza sauti kukemea vitendo hivi. Je, ni nani wa kuwasemea wafungwa na wale wanaowekwa rumande, wasio na wadhifa wowote katika jamii wanaokumbana na vitendo vya kikatili kutoka kwa polisi? Kwamfano; Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Mheshimiwa Zitto Kabwe, alipokuwa akifanya ziara mkoani morogoro alikamatwa na kuwekwa ndani. Alipata kuishirikisha jamii, moja ya vitu alivyoshuhudia na kuandika hivi katika ukurasa wake wa twitter;
“Usiku mmoja niliolala kituo cha Polisi Moro umenionyesha namna raia wetu wengi wanateseka kwa haki za msingi kuvunjwa. Kuna watu wanateswa sana na mmoja nimemkuta hajapelekwa hospitali ilhali amevunjwa mbavu kutokana na mateso aliyoyapata akiwa mikononi mwa polisi.”
Hii inaonyesha kwamba kuna vitendo vingi vya kikatili vinavyowapata wengi wanaoangukia mikononi mwa polisi. Rais wa Marekani marehemu John F. Kennedy aliwahi kusema; “The right of every man are diminished when the rights of one man are threatened” akimaanisha (Haki ya kila mmoja hupotea pale haki ya mtu mmoja inapowekwa mashakani)
Tatizo lingine ni kwamba, Watanzania tumekua kama moto uwakao kwa nguvu pindi upepo uvumapo. Upepo ukitulia basi na nguvu ya moto inapungua. Kwa lugha iliyowazi ni kwamba huwa tuna tabia ya kukemea pindi pale tu matatizo haya yanapoibuka. Yakishapita, kila mtu anasahau na kuendelea na shughuli zake kana kwamba kukemea tu inatosha kuleta suluhu ya tatizo hili.
Dhana potofu inayojengeka
Vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na jeshi la polisi, vimefanya watu wengi kuamini kwamba polisi wapo juu ya sheria. Pengine nao polisi kwa kutowajibishwa kwao, kunawafanya wao pia wajione wapo juu ya sheria na kwamba wanaweza kufanya chochote na wakakingiwa kifua.
Hizi ni dhana potofu kwani polisi ni mtumishi wa serikali kama ilivyo kwa watumishi wengine na wana taratibu zao kisheria zinazowaongoza na wanazotakiwa kufuata pindi wanapotekeleza majukumu yao. Taratibu nyingi zimeelezwa kwenye SHERIA YA JESHI LA POLISI NA HUDUMA SAIDIZI SURA YA 322 pamoja na SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI SURA YA 20
Katiba inasemaje kuhusu mateso na adhabu?
Ibara ya 13 (6) (e) ya katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inasema;
“ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha”
Je, Askari wanakingiwa kifua?
Mara nyingi tumekua tukishuhudia polisi wakiwapiga vibaya raia pindi wanapowakamata kama wahalifu. Ila ni mara chache sana tumesikia polisi wakiwajibishwa kutokana na vitendo hivi vya unyanyasaji. Tuchukulie mfano mzuri tu wa tukio lililosababisha kuuwawa kwa binti Akwelina aliyepigwa risasi mnamo tarehe 16 Februari 2018. Baada ya kukamatwa kwa wale askari waliosababisha mauaji hayo, mnamo tarehe 20 Aprili 2018 Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) alifunga jalada la kesi ya mauaji ya Akwelina. Alipokuwa akiongea na waandishi wa habari alisema kwamba;
“Jeshi la polisi linapotumia nguvu kuzuia maandamano, haliwezi kushtakiwa au hata kukitokea vurugu na kusababisha mauaji huwezi kulishitaki jeshi”
Vilevile aliongeza kwa kusema kwamba;
“katika maandamano yale ya watu zaidi ya 200, huwezi kubaini nani amehusika na kumpiga risasi Akwilina na mwili wake haukutolewa risasi yoyote”
Alipoulizwa kuhusu askari waliokamatwa baada ya kutokea kwa tukio hilo alisema;
“Kama jalada nimelifunga, kwa hiyo askari nao wameachiwa huru hawana hatia.”
Matamko kama haya, yanaleta ukakasi kwani yanaonyesha Dhahiri kwamba kuna upande unaokingiwa kifua. Je, ni kweli sheria inafuata mkondo wake? Je, ni kweli sheria ni msumeno unaokata huku na huku? Au tuseme upande mmoja wa msumeno umeshakuwa butu sasa?
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (2002)
Sheria ya mwenendo wa makossa ya Jinai inaeleza wazi kabisa ni kwa jinsi gani na kwa namna gani polisi anatakiwa kutumia nguvu katika ukamataji. Kifungu cha 21 (1) kinasema;
“Afisa polisi au mtu mwengine hatakiwi, wakati wa kumkamata mtu, kutumia nguvu zaidi au kuvunja utu wa mtu huyo zaidi ya ilivyo lazima kufanikisha ukamataji au kumzuia utorokaji wa mtu baada ya kukamatwa.”
Sheria hii inaendelea kueleza katika kifungu 21 (2) kwa kusema;
“Bila kupunguza matumizi ya kifungu kidogo cha (1), afisa polisi hatatakiwa, wakati wa kumkamata mtu, kufanya kitendo kinachoweza kusababisha kifo kwa mtu huyo, isipokuwa kama afisa polisi anaamini kwa sababu za msingi kwamba kufanya kitendo hicho ni muhimu katika kulinda maisha au kuzuia madhara makubwa kwa mtu mwengine.”
Kumbe sheria ipo wazi kabisa kwamba polisi hatakiwi kutumia nguvu zaidi ya ilivyo lazima. Lakini ni mara ngapi tumeshuhudia polisi wakitumia nguvu zaidi ya ilivyolazima? Mfano mzuri tu mnamo tarehe 27 April 2018 iliripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa raia mmoja aliefahamika kwa jina la Suguta Chacha ameuwawa kwa kuchomwa kisu na askari! Miongoni mwa walioguswa na tukio hili ni Mbunge John Heche ambaye ni kaka wa marehemu. Aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter na kueleza;
“Watu hawako salama tena mikononi mwa polisi. Mdogo wangu Suguta amekamatwa usiku na ameuwawa na polisi kwa kuchomwa kisu. Najisikia maumivu mno, hii sio nchi ambayo tunaitaka. Najiuliza maswali mengi ni kwa vipi mtu amefungwa pingu anachomwa kisu tena na polisi.”
Ni takribani mwezi mmoja tu nyuma ya hapo (25 machi 2018) iliripotiwa kufariki kwa kijana aliyefahamika kwa jina la Allen Jijini Mbeya. Kijana huyu alifariki baada tu ya kutoka mikononi mwa polisi ambapo taarifa za awali zilieza kuwa kifo chake kilisababishwa na kipigo kikali cha polisi, taarifa ambazo jeshi la polisi lilikanusha.
Kwanini kuhatarisha maisha yako kwa kukiuka kanuni na taratibu?
Kwa vile wanazo nguvu kisheria, polisi wengi hudhani kwamba hata akikiuka kanuni na taratibu hakuna madhara yoyote. Pengine wanasahau kwamba kwa kufanya hivyo anahatarisha maisha yake pasipo sababu ya msingi. Katika kesi ya Jamuhuri dhidi ya Nicas Lulenga (1983) (REPUBLIC VERSUS NICAS LULENGA) Nicas Lulenga alishitakiwa kwa kosa la kujeruhi kwa kutumia mshale. Katika kesi hii, askari walivamia nyumba ya mshitakiwa kisirisiri kwaajili ya kumkamata. Mshitakiwa pasipo kujua nini kilikuwa kinaendelea wala sababu ya kukamatwa kwake, aliamua kujihami kwa kujibu mashambulizi kwa kutumia mshale na ndipo alipomjeruhi askari mmoja wapo.
Mbele ya mahakama upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha kama walimuonya mshitakiwa kujisalimisha kabla ya kumkamata. Mahakama ilieleza pia kwamba katika kutambua kama ukamataji ulikuwa chini ya taratibu za kisheria, haihitaji kujiridhisha kwamba mshitakiwa ana kosa au la. Mahakama haikuona kama mshitakiwa ana kosa kwani polisi walikiuka kanuni na sheria ya 21 ya Sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai Sura ya 20. Mshitakiwa alishinda kesi kwa utetezi wa kwamba alikua akijihami.
Kumbe tunaweza kujihami dhidi ya askari?
Ndio! Raia anaweza kujihami dhidi ya askari yoyote endapo tu askari huyo anakiuka taratibu na kanuni za kisheria katika kutekeleza majukumu yake. Lakini ikumbukwe kwamba raia pia ana wajibu wa kutii sheria bila shuruti. Askari anapofuata taratibu na kumtaka raia afanye jambo fulani ambalo limo katika taratibu za kisheria basi raia huyo hana budi kufuata maagizo au maelekezo hayo.
Raia anapokiuka au anapoonyesha ukaidi wa namna fulani, sheria inamruhusu askari kutumia nguvu ya ziada (Rejea kifungu namba 21 cha Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai). Nguvu hiyo ya ziada inaweza kuambatana na kipigo. Raia atakapo jaribu kujihami na kipigo hiko kwa kujibu mashambulizi dhidi ya askari, hawezi kushinda mbele ya mahakama kwa kigezo cha kujihami zaidi tu atakua amejitengenezea kesi nyingine.
Hata hivyo matukio ya raia kujihami dhidi ya vitendo kandamizi vinavyofanywa na baadhi ya askari ni machache sana kwani watanzania wengi hatuna huo ujasiri na ni waoga. Askari nao wanatumia woga wa raia kama silaha. Kwa kiingereza tunasema “They feed off our fear”
Uchunguzi unafanyika!?
Mara nyingi yanapotokea matukio kama haya, jeshi la polisi (pengine kwa mazoea) limekua likitamka kuwa uchunguzi unafanyika ili kubaini chanzo na sababu ya vitendo viovu vinavyofanywa na maafisa wa jeshi la polisi ambavyo ni kinyume na haki za binadamu. Lakini cha kushangaza mara nyingi kumekuwa hakuna mrejesho wa matokeo ya uchunguzi na hatua gani zimechukuliwa kwa maafisa polisi waliokiuka maadili yao ya kazi. Suala hili limekua likileta ukakasi kwa wanajamii.
Nini madhara ya ukatili huu?
Ni wazi kabisa uhusiano baina ya wananchi na jeshi la polisi unapungua kwa namna moja au nyingine. Tayari wananchi wamejenga hofu kubwa dhidi ya Jeshi la polisi. Jeshi ambalo lilipaswa kulinda amani yao, sasa limekua jeshi linalotishia amani yao. Kuna madhara makubwa pindi uhusiano wa raia na askari unapofifia. Sio ishara nzuri kwani kufifia huku ni tishio la amani ya kesho.
Nini kifanyike?
Ningependa kuhitimisha kwa kutoa mapendekezo yangu binafsi ninayoona kwa namna moja au nyingine yanaweza kupunguza au kuondoa kabisa tatizo hili. Hata hivyo kiu yangu kubwa ni kuona tatizo hili linaondoka kabisa kwani tukisema lipungue ina maana bado kuna watu wataendelea kuwa wahanga wa unyanyasaji wa polisi.
“We are not anti-police… we’re anti-police brutality” akimaanisha (Hatupo dhidi ya polisi…tupo dhidi ya ukatili wa polisi)
Mwisho kabisa ningependa kumaliza kwa ushairi nilioutunga wenye jina;
Mungu Ibariki Tanzania!

- Kuwepo na Code of Ethics and Conduct for the Police force
- Nadhani hii italeta radha nzuri tukiiweka kwa Kiswahili kama “Sheria za maadili ya uwajibikaji wa Polisi”. Hapa nchini tunayo sheria ya Code of Ethics and Conduct for the Public service ambayo ni kwaajili ya watumishi wote wa UMMA. Ili kukomesha tatizo la unyanyasaji unaofanywa na baadhi ya maafisa wa polisi, kuwepo na sheria za maadili ya polisi katika kutekeleza majukumu yao.
- Sheria hii iweke bayana namna na jinsi gani polisi anatakiwa kutekeleza majukumu yake katika kulinda amani na usalama wa raia na mali zao. Iwe sheria-chimbuko kutoka kwa Sheria ya mwenendo wa makosa ya jina pamoja na Sheria ya jeshi la polisi na huduma saidizi.
- Iwepo tume maalumu (Special tribunal) itakayosimamia mwenendo wa utekelezaji wa majukumu wa jeshi la Polisi.
- Hapa ningependa nianze kwa kutoa mfano mzuri na ulio hai wa Bunge la Tanzania. Wabunge wa Tanzania wana immunity kubwa wawapo bungeni. Kwa miaka mingi jambo hili liliwapa wabunge nguvu ya kuzungumza chochote. Miaka ya hivi karibuni, ikaanzishwa kamati ya maadili ambayo moja ya kazi zake ni kudhibiti immunity kubwa waliyonayo wabunge wawapo bungeni. Hivi sasa wabunge wanaweza kuwajibishwa kupitia kamati ya maadili endapo mbunge atatumia immunity yake vibaya
- Tukirudi kwa Upande wa polisi, suala hili pia linawezekana kabisa. Kwakua askari wanakua na functional immunity pindi wanapotekeleza majukumu yao ambayo inapelekea wao kushinda mashtaka mengi ya unyanyasaji, iundwe tume ambayo itasimamia mwenendo wa utekelezaji wa majukumu ya jeshi la Polisi. Vilevile tume hii ipewe nguvu ya kuhoji askari yoyote yule (kuanzia ngazi ya juu ya IGP mpaka ngazi ya chini ya Police Constable) atakaye kiuka maadili ya utekelezaji wa majukumu yake. Tume iweze kushirikiana na mahakama katika kuwaadhibu maafisa wote watakaokiuka maadili ya utekelezaji wa majukumu yao.
“We are not anti-police… we’re anti-police brutality” akimaanisha (Hatupo dhidi ya polisi…tupo dhidi ya ukatili wa polisi)
Mwisho kabisa ningependa kumaliza kwa ushairi nilioutunga wenye jina;
SHERIA INA MKONDO
Vipi ule msumeno, kukata huku na huku,
Ama butu yake meno, haukati tena huku,
Vilio kusaga meno, Pangu pakavu kapuku,
Sheria ina mkondo, haina budi kufwatwa.
Vipi ule msumeno, kukata huku na huku,
Ama butu yake meno, haukati tena huku,
Vilio kusaga meno, Pangu pakavu kapuku,
Sheria ina mkondo, haina budi kufwatwa.
Ukakasi na simanzi, uchungu mwingi moyoni,
Kwa vitendo kandamizi, Chonde polisi acheni,
Yatisha masimulizi, yaeneayo nchini,