Ukarabati wa Ikulu kwa Mwaka-Ungejenga Nyumba za Walimu 611

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Tatizo la Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari limeendelea kuwa sugu siku kwa siku. Serikali imekuwa ikijatahidi kujitetea kwamba tatizo ni ufinyu wa bajeti na hivyo Walimu waendelee kuvumilia mpaka hapo hali ya kifedha itakapokuwa nzuri.

Lakini cha kushangaza bajeti ya kukuarabati Ikulu kila mwaka huwa inapatikana bila matatizo yeoyote kwa kuwa Ikulu ni mahali patakatifu pa patakatifu.

Kwa mfano tangu Serikali ya awamu yanne iingie madarakani takribani bilioni 17 zimetumika katika kukarabati Ikulu.

Kwa mfano,tazama jedwali hili

Mwaka na kiasi cha pesa
2006-2007 - 6,114,562,685
2007-2008 - 5,596,900,000
2008-2009 - 5,712,000,000

Pesa hizi kwa Mwaka zingejengwa Nyumba nzuri za Walimu 611 na chenji inarudi.

Hivyo basi kwa kipindi chote cha miaka mitati jumla ya nyumba 1833 zingejengwa na wala tusingekuwa na tatizo kubwa la nyumba za walimu.

Hoja zangu za msingi:

  • Hivi ni kwanini Ikulu ikarabatiwe kila Mwaka?
  • Ni kwanini ikarabatiwe kwa pesa yote hiyo?
 
Mzee hii habari ni ya kweli????????? Ukarabati au matumizi ya Ikulu?

Ingefaa sana tukapata matumizi yote ya Ikulu kuanzia gharama za safari za mzee, grocery and supplies, ukarabati halafu ndo tujadili, na tukajua pia kiasi gani kilitumika kwenye kila item kwa kipindi cha Mkapa kwa mfano (tuta-apply inflation factor ili ziwe comparable). Kama kweli hii pesa imetumika kwenye ukarabati tu basi haya ni matumizi mabaya sana ya kodi zetu ambazo sababu tosha ya kuwanyima CCM kura. Na walimu na askari wagome kwa kuonewa
 
Mkuu hizi ni za Ukarabati tu!bado mazagazaga mengine...
 
Back
Top Bottom