Ukanda maalum wa Uuzaji Bidhaa Nje ya Nchi (Export Processing Zones)

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,482
54,839
Ukanda maalum wa Uuzaji Bidhaa Nje ya Nchi (Export Processing Zones)
Mpango maalum kwa ajili uanzishaji wa uwekezaji unaolenga katika mauzo ya bidhaa nje ya nchi kwa ili ya kuanzisha ushindani wa kimataifa ili kuwezesha uchumi utakaojikita katika kusafirisha bidhaa zilizozalishwa Tanzania.

Kanda Maalum za Uchumi
Mpango huu una madhumuni ya kuwezesha ukuaji wa haraka wa uchumi, kukuza mapato ya nje, kutengeneza ajira na kuvutia wawekezaji binafsi kwa njia ya Uwekezaji wa Nje wa Moja kwa Moja (FDI) na Uwekezaji wa Ndani wa Moja kwa Moja (DDI) katika sekta zote za uzalishaji na utoaji huduma.

Maeneo yenye Vipaumbele

Uendelezaji Miundombinu:
Kwa kutumia mpango wa Kanda Maalum ya Uchumi (SEZ), mwekezaji anaweza akaanzisha maeneo ya viwanda na biashara katika Kanda Maalum ya Uchumi (SEZ). Uwekezaji kwa upande wa miundombinu unaweza kufanyika kupitia ujenzi wa barabara, huduma za jamii, na masuala ya msaada wa kiutawala na maeneo yanayohusu huduma.

Uzalishaji:
Wawekezaji wanaweza kuanzisha shughuli za uzalishaji katika Kanda Mahsusi ya Uchumi kwa kutumia Leseni ya Ukanda Maalum wa Kiuchumi (SEZ) au kwa kutumia Leseni ya Kusafirisha Bidhaa Nje ya Nchi ya mpango huu na kunufaika na faida mbalimbali zinazotokana na mpango huu.
Miongoni mwa za fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania ni pamoja na usindikaji wa mazao ya kilimo, vito vya thamani (madini), uchakataji wa ngozi, usindikaji wa samaki, misitu na mazao ya misitu, na viwanda vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na uundaji.

Biashara na Huduma:
Wawekezaji wanakaribishwa kuanzisha uendeshaji wa biashara na huduma katika Kanda za Biashara Huria na Bandari Huria ambazo kwa kiasi kikubwa bado fursa hizi hazijatumika.

Utalii:
Wawekezaji wanaweza kuwekeza katika maendeleo ya utalii kupitia Kanda Maalumu za Kiuchumi kwa kutumia Leseni ya kanda hiyo. Miradi inaweza kuwa ya hoteli, makumbusho, sehemu za kuburudisha na kilabu za gofu.
Sifa za kuwekeza kupitia SEZ: Mwekezaji ye yote ana sifa za kuwekeza chini ya Mpango Maalumu wa Kanda za Uchumi. Mwekezaji sharti atimize vigezo vifuatavyo:

  • Uwekezaji lazima uwe mpya, kwa maana ya usiwe uwekezaji ambao umeshafanyika katika ukanda huu maalum
  • Mapato ya biashara ya usafirishaji bidhaa nje ya nchi isiwe chini ya dola milioni tano kwa mwekezaji mgeni kwa mwaka na yasiwe chini ya dola za Marekani millioni moja kwa wawekezaji wazawa.
  • Lazima muwekezaji ahakikishe Usalama wa mazingira unaojitosheleza
  • Utumiaji wa vifaa vya kisasa katika uchakataji na mitambo mipya
  • Mwekezaji lazima awe katika maeneo yaliyoainishwa katika paki za Kanda Mahsusi za Uchumi (SEZ) kama vile Ukanda maalum wa uwekezaji wa Benjamini William Mkapa uliopo Mabibo, Dar es salaam.
Chanzo: FURSA ZA UWEKEZAJI | MSMEs Information Portal
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom