UKAME: Soko la Kimataifa la Kibaigwa lakauka. Sasa linategemea mahindi toka Mutukula

Reucherau

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
756
1,740


SOKO la Kimataifa la Nafaka Kibaigwa mkoani Dodoma ni jeupe baada ya kukosekana kwa nafaka, hususan mahindi huku wimbi la njaa likizikabili familia nyingi.

Uchunguzi wa FikraPevu unaonyesha kwamba, kwa zaidi ya mwezi sasa hakuna mahindi yanayoingia sokoni hapo na mara chache sana mahindi kidogo huletwa sokoni kutoka Mutukula nchini Uganda.


Hata hivyo, haijajulikana ni kwa namna gani mahindi hayo yanavuka mpaka wa Tanzania na Uganda na kusafirishwa hadi Kibaigwa kutokana na hali ya ukame na tishio la njaa lililoikabili mikoa mbalimbali katika eneo la Afrika Mashariki.

Kutokana na uhaba huo wa nafaka, hivi sasa kilo moja ya mahindi sokoni hapo inauzwa kwa Shs. 1,070 hivyo kufanya gunia moja lenye uzani wa kilogramu 130 kuuzwa kwa takriban Shs. 140,000, kiwango ambacho mwananchi wa kawaida anashindwa kumudu.

Februari Mosi, 2017 kilo moja ya mahindi ilikuwa ikiuzwa kwa Shs. 970, lakini wafanyabiashara wa soko hilo wanasema kwamba, mara nyingi bei iliyoandikwa kwenye ubao siyo halisi kwani inayotembea sokoni huwa iko juu zaidi.

“Kama unavyoona, ni wiki mbili sasa zimepita tangu tani 90 zilipoingia kutoka Mutukura, nchini Uganda lakini yale mahindi yaliyokuwa yakiletwa na wakulima wa mkoa wa Dodoma na Manyara hayapo, kwa kifupi hali ni mbaya,” anaeleza Godfrey Ndigomo, mmoja wa madalali wa soko hilo.

Ndigomo anasema, kudorora kwa biashara ya nafaka sokoni hapo kumechangiwa na sababu nyingi, lakini kubwa zaidi ni ukame pamoja na wakulima kushindwa wa mikoa ya Dodoma na Manyara kushindwa kuzalisha kiwango kinacholingana na mahitaji hasa baada ya kufukuzwa kwenye mbuga ya Emboley Murtangosi wilayani Kiteto.

Zaidi, soma => UKAME: Soko la Kimataifa la Kibaigwa lakauka. Sasa linategemea mahindi toka Mutukula | FikraPevu
 
Ukame ni half natural phenomenon and half man made. Serikali ikubali kwamba kuna tatizo na ianze kuchukua hatua mathubuti za kupambana na hili tatizo
 
hamna njaa jamani sema kuna upungufu wa chakula(wanasiasa sio watu wazuri kabisa) hawawezi kukuambia ukweeli ata siku moja
 
Acha uchochezi ndugu yangu, hayo mahindi mengi umeyaona wapi? Vijana wanacheza mpira sokoni humo
Rais ndiye alisema chakula kipo kingi, na nchi ni ya kijani. Pia, yeye ndiye pekee anayejua kama kuna uhaba wa chakula au la. Provided hajasema kuna uhaba, basi hakuna uhaba.
 
Nimefika kujionea hali halisi sokoni Kibaigwa na hali iko hivi,biashara inaendelea na mahindi zipo shehena za kutosha nawaletea picha zaidi!
 

Attachments

  • 1487671123655.jpg
    1487671123655.jpg
    68.2 KB · Views: 41
Back
Top Bottom