nyembeason
Member
- May 4, 2009
- 44
- 21
Haya majanga, njaa na ukame, lazima yakabiliwa kwa njia za kisera na kisayansi, siyo matamko au ubabe kwa wananchi wanayokumbana nayo kwa sasa. Rais lazima aelimishwe kitaalamu KISHA atumie mamlaka yake ya kutoa matamko yake kuyakabili, siyo kuwatupia wananchi. Awaambie wakuu wa wilaya, mikoa na wengineo kuwa ndani ya miaka miwili au mitatu (long time approach) pasiwepo na njaa na ukame. Waje na mikakati ya kitaalamu kukabiliana nayo. Mwisho wa siku, Wafugaji wawe na mabilioni ya mifugo, wakulima wawe na mabilioni ya magunia. Hapa ndiyo Tanzania ya viwanda itakuwepo. Viwanda bila kuunganishwa na kilimo na kazi bure. Kilimo hakiwezi kukua bila kukabiliana na ukame, bila kuacha kutegemea mvua. Mwelimisheni Rais vizuri.