Ukaguzi wa Magari Mwezi Machi

laptop90

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2017
Posts
1,827
Reaction score
2,298
Tanzania imetangaza kua kutakua na ukaguzi wa vyombo vyote vya usafiri vya moto kwa mwezi March, na hela itakayopatikana itatumika kununua usafiri kwa mapolisi.

Ni majuzi kama sii Aug au sept 2021 tulipeleka magari kukaguliwa na kupewa stika za nenda kwa usalama.

Ni miezi takribani 5 tangu huo ukaguzi ufanyike.

Sana nataka kujua hivi dhumuni hasa la huu ukaguzi ni nini.

Kama ni kupata pesa kwanini wasingesema tu wenye magari walipe kiasi flani kuliko kumpotezea mtu mda kwenda polisi kukaguliwa gari?

Hivi kweli pamoja na adhabu zote tunazotozwa hazijawatosha kununua vyombo vya usafiri?[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849] sasa natamani JPM afufuke aone madudu ya kijinga haya.[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848].

Mafuta yamepanda petrol kesho 2540, huku mkijinasibu kupunguza shs 100 kwa lita.

Ni unafuuu upi tunaupata sasahivi,
Zanzibar rais amepunguza bei na kusema isiuzwe zaidi ya 2000 huku bara 2800 what a hell?
 
Hatuna vyombo vya moto, tunasiraha za moto tuu, Sasa ni razima tupate vyombo vya moto kwaaajiri ya matumizi yetu. 🤔
 
Mama bora achapishe noti nyingine ili apate hela, hata mikopo inaanzakulipiwa VAT na kodi nyingine kuanzia march
 
Hili jeshi mchosho wana fixed mentality, kuna changamoto nyingi tu kuhusiana na huo mpango
  1. Hizo stika zenyewe wanasema zipo za magari ya biashara na binafsi, lakini ukisema una gari binafsi wanasema stika zimekwisha, wanataka uchukue za magari ya biashara ambazo bei juu zaidi.
  2. Huo ukaguzi huwa hawafanyi, wanakaa ofisini wanauliza gari ni aina gani na namba zake hata bila kulitazama, usanii mtupu, Sagini asipokuwa makini atajipaka matope kwenye hilo zoezi
  3. Wakati mwingine hizo stika wanapewa vijana wakaziuze mtaani kwa bei ya kuruka
 
Yes yes acha inyeshe watanganyika waone panapovuja...
 
Huyo mtu wako alipokuwapo alikuwa na jipya Gani zaidi ya one Man show una Hoja Ila kutaja huyo mtu aliivuruga hii Nchi unakosea
 
Tatizo hao wanaopanga hizi Kodi na tozo, wanakula na kuishi Bure kwa Kodi za watanzania, hawajui machungu yoyote ya maisha maana hata maliwato wanaenda kwa Kodi zetu.
 
Kinachotafutwa hapo ni tozo si kingine, wameanzia kwenye mabenki wanadai wanakata VAT kwenye akaunti za wateja.........tutarudi kuweka pesa kwenye mchago.
 
Nchi ya mazuzu wacha tuonyeshwe cha moto. Na bado! Watawala wanatapanya fedha kwa safari zisizo na maana na kutumia mamilioni bila kujali umaskini wa nchi huku sisi tumekalia kwenye ushabiki wa Simba na Yanga. Ni vizuri maisha yazidi kuwa magumu!
 
Sasa unadhani Rais kusafiri na jopo kubwa la wajumbe wa kamati CCM huku na kule Ulaya unadhani pesa zinatoma wapi?
 
Nchi ya mazuzu wacha tuonyeshwe cha moto. Na bado! Watawala wanatapanya fedha kwa safari zisizo na maana na kutumia mamilioni bila kujali umaskini wa nchi huku sisi tumekalia kwenye ushabiki wa Simba na Yanga. Ni vizuri maisha yazidi kuwa magumu!
Yaani hawana habari kabisa.
 
Tatizo hao wanaopanga hizi Kodi na tozo, wanakula na kuishi Bure kwa Kodi za watanzania, hawajui machungu yoyote ya maisha maana hata maliwato wanaenda kwa Kodi zetu.
Yaani hawa watu watalaaniwa sana. Pesa mtaani ngumu wao wanajipangia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…