‘Ukaguzi hesabu za UDA haujakamilika’

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,919
19,614
IKIWA sasa ni takriban miezi miwili tangu serikali kutangaza uchunguzi wa hesabu za Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ameshindwa kukamilisha kazi hiyo katika kipindi cha mwezi mmoja kama ilivyotangazwa awali.

Agosti 13 mwaka huu, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), George Mkuchika, alimkabidhi rasmi CAG barua ya kufanya uchunguzi wa hesabu za UDA baada ya sakata hilo kuibuka katika mkutano wa nne wa Bunge.Wakati akimkabidhi CAG jukumu hilo, Mkuchika alisema uchunguzi huo ungefanywa katika kipindi cha mwezi mmoja tangu kutolewa rasmi kwa agizo hilo.

Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, CAG Luddovick Utouh, alisema uchunguzi huo ndiyo uko katika hatua ya kati kabla ya kufikia mwisho. *


"Ni kweli waziri alitoa agizo kwamba uchunguzi ufanyike ndani ya mwezi mmoja. Lakini ukweli ni kwamba hadi sasa, uchunguzi haujakamilika na ndiyo uko katikati," alifafanua CAG Utouh.Utouh alisema tatizo kubwa ni serikali kutoa muda maalumu wa kufanya uchunguzi bila kujali* ukubwa wa tatizo lenyewe na kutoa mfano wa uchunguzi huo wa UDA.Alisema, ofisi yake inafanya mambo kitaalamu na kwamba ni* vigumu kupewa muda maalumu wa kufanya kazi kabla ya kufahamika kwa ukubwa wa tatizo.

"Tatizo kubwa wao serikalini wanapotaka nifanye special audit (ukaguzi maalumu) wanatoa muda maalumu wa kufanya kazi pasipokujua ukubwa wa tatizo kitaalamu. Sasa ofisi yangu inafanya kazi kwa kutumia vigezo vyake kitaalamu. Hatuwezi kusema tuache kufanya kazi muhimu zilizobaki kwa sababu tumepewa mwezi mmoja," alifafanua CAG.


Alisema ofisi ya CAG itafanya ukaguzi huo kwa umakini hadi utakapokamilika ndipo utatoa ripoti baada ya kujiridhisha kwamba kila eneo la msingi kwa mujibu wa hadidu rejea, litakuwa limeguswa kwa kina.


"Tunafanya uchunguzi hadi tuone maeneo yote ya msingi tumeyagusa, kwa hiyo kusema ni lina uchunguzi utakamilika kwa sasa siwezi kusema lakini tuko katika hatua nzuri na bado tunaendelea kufanya hivyo," alisema Utouh.


Alisema kufanya ukaguzi wa mahesabu si jambo la kuharakisha kwani kuna mambo ya kupitia nyaraka muhimu moja baada nyingine, mambo ambayo yanahitaji muda wa kutosha kuweza kuyafanyia kazi zaidi.

Uchunguzi wa POAC
Hatua hiyo ya CAG kutokamilisha* uchunguzi katika kipindi cha mwezi huo mmoja, imefanya uchunguzi wa mchakato wa ubinafsishaji wa UDA uliopaswa kufanywa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), kushindwa kuanza.

Kukwama kwa uchunguzi huo kunatokana na wajumbe wa kamati ndogo ya POAC kushindwa kupata ripoti ya CAG, ambayo ni moja ya hadidu zao za rejea.

Mmoja wa wajumbe wa POAC, ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kimsingi, wao katika uchunguzi wao pamoja na hadidu nyingine wanalazimika kupitia ripoti ya uchunguzi ya CAG baada ya kukamilika kwa uchunguzi wake.

Mwenyekiti wa POAC ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, alifafanua kwa kifupi mwishoni mwa wiki kwamba, "kimsingi, hakuna tofauti kubwa kati ya uchunguzi wa CAG na wetu. POAC inafanya kazi na CAG. CAG ni afisa wa Bunge".
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom