CCM, kama baraza la katiba, ilishatoa maoni yake tayari na yakaingizwa kwenye rasimu. Sasa wasubiri wajumbe wa bunge la katiba wayafanyie kazi. Kwanini wanataka kulazimisha mambo ambayo hayamo kwenye rasimu inayojadiliwa bungeni yaingie kwenye rasimu. Suala la serikali 2 halimo kwenye rasimu. Kwanini wanataka kuliingizamo kimabavu? Huoni kwamba wanatishia uhai wa bunge la katiba?