Ujumbe

mumemwema

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
2,094
Reaction score
1,580
UJUMBE KWA WAKE (WIVES) NA WOTE MNAOCHUMBIWA
Wewe Mrs, au Mrs Mtarajiwa, SIKILIZA mama: Kila unapokwenda mahali ambapo Wanaume wanaonesha kukupenda, au tayari unajua kama wanaume wanakupenda, Jitahidi uende na Mume wako. Kama mume wako hawezi kwenda, ongea na mume wako ili mtafute ufumbuzi. Aiseee Tusidanganyane dada yangu Mrs. Mahwago-hwago, KILA MWANADAMU anafurahia kupendwa ! ! ! Epuka kwenda saaana sehemu ambazo Wanaume wanaonesha kukupenda na HAWAJALI KWAMBA UMEOLEWA na huku wewe moyoni mwako unajua unafurahia kuona Wanaume wanavyokupenda - HUO NI MTEGO MBAYA na usipoushughulikia mapema, LAZIMA UTAKAMATIKA TU upende usipende, na wewe hutakuwa wa kwanza. Wapo weeengi saana waliishia kwenye mapenzi kwa siri saana sana na leo mioyo yao inawasuta. Usi-imwagilie mbegu hio ya kufurahia kupendwa na Wanaume, Mama, hiyo mbegu LAZIMA itaota baada ya mwezi au mwaka, au miaka. Biblia inasema "Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia." Mithali 27:12
NUNUA KITABU CHETU "You Want a Happy and Enjoyable Marriage. But How Much Have You Changed?" by Pastor Donis and Nnunu Nkone - Kiswahili Page
 
Biashara matangazo.......mwanamke mjinga hubomoa nyumba yake kwa mikono yake bali mwerevu huijenga kwa mikono yake .......


Tamaa mbaya sana watu hawajui kuridhika na kukinai na walivyonavyo..
 

Umenena vyema mpnzi.
 
Jamani eehee samahani kama nimewakwaza lakini Mimi Nia yangu haikuwa kuwatangazia biashara kama mnavyofikiria . Hata Yesu alihubiri ,, mwisho akasema mwenye masikio na afanyaje, asikieee. Kama hii ni safu ya MMU kwa nini tusikumbushane especially kwa sisi wakina Mama na wakina Baba .

Badala ya kuponda hili somo , hebu tujaribu kuwa wazito Wa kujibu na tuwe wepesi Wa kusikia hii meseji. Sio wote tunaojua kila kitu , wengine tunahitaji kujikumbusha au kujua vitu . Na kama unaona Huu ujumbe haukufai just pita Hakuna aliyekulazimisha usome kuliko kutapakaza mambo ambayo siyo . Hii sio biashara Bali ni mafunzo ya mahusiano na mnajua hilo ilamnajifanya hamjui . Wengine ndoa ziko kwenye moto kwa kuwa wepesi Wa kujibu kuliko kusikiliza hebu tujaribu kujitahidi kujifunza watz aiiii tunaongea sana saa.nyingine na kupenda kuponda vitu bila hata points za kueleza au bila ya kutojua ukweli Wa mambo. Alamsiki.. Asante ni wote.
 
Loveissweet, vipi kuhusu wanaume pia, wafanyeje?

Kwa wanaume inakuja pale mpenzi or mkeo anapotaka kutoka na wewe msiwe Wazito Wa kukubali kwa.maana kuna wanawake wengine hatuwezi kusema straight sababu kama ya hiyo meseji , ila tunaomba umtoke tuu na sisi. Asante !
 
kwenda na mumewe haisaidii kama mwanamke mwenyewe hana msimamo!!!'
cha muhimu ni kujielewa na kumheshimu mwenzako!!
 
kwenda na mumewe haisaidii kama mwanamke mwenyewe hana msimamo!!!'
cha muhimu ni kujielewa na kumheshimu mwenzako!!

Sikatai . Bali actions speak louder than words. Ni vizuri kwenda na mkeo some other place. Kwa sisi wanawake tuko wengine tunapenda sana attentions kutoka kwa wapenzi / mume zetu . Sisemi kila safari Muwe pamoja ,lakini kwa nini umpe shetani nafasi ,wakati kuna vitu vingine vinaweza kufanywa bila shida . I don't know hebu niwaache wengine watoe ya moyoni. Thanks.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…