Ujumbe wangu kwa wanaume wenzangu juu ya wake/wapenzi wenu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,814
34,196
Moyo waliopewa WANAWAKE akipewa Mwanaume hata kwa Siku tu LAZIMA AFARIKI!
Ule uwezo wa kuvumilia Maumivu ya Kuzaa ndio huwa unawafanya wavumilie mambo wanayotendewa na Wanaume kiasi ambacho hadi wewe Mwanaume unajiuliza,HADI HILI

AMENISAMEHE,INAWEZEKANAJE!
Kama kuna jambo Wanaume huwa wanakosea basi ni kudhani kwamba Wanawake ni Wajinga...Hawajawahi kuwa Wajinga ila

Wameumbwa na Moyo wa Uvumilivu uliopitiliza..Na Mungu aliwatengeneza hivyo makusudi...Ni sawa na Mwanamke anavyoweza kumvumilia Mwanaume ambaye kwa Miaka 10

anamgusagusa tu bila kumfikisha kileleni lakini Mwanamke yupo tu..Uvumilivu ulioje!Mwanamke anayeweza kukaa na Mwanaume mlevi anayempiga ngumi kila akirudi ila yeye yupo tu..Sio kwamba

ni Mjinga,LA HASHA!Ni katika ule Uvumilivu tu..
Kasheshe ni pale Mwanamke huyu ANAPOCHOKA...Anaweza akavumilia miaka 10...Unampiga...Anakufumania..Humfikishi

Kileleni..Ila Siku Akichoka akasema KWAHERI,Ule Moyo wa Uvumilivu huwa UNAGEUKA na kuwa JIWE GUMU na hata uimbe mashairi ya "Bado ananijia ndotoni ila nikiamka simuoni bado ananijia nikilala Haki ya Mungu sio masihara"

HATARUDI na utabakia kiwete wa mahaba yake daima...Kabla hajafikia Stage ya KUKUCHOKA,chondechonde kumbuka nayeye ana Moyo,MPE ANACHOSTAHILI!
Usichanganye Uvumilivu wake ukadhani ni Ujinga,ITAKUCOST
 
Namashaka na mtoa mada ngoja niulize wanawake wenyewe.. et wadada wa humu jf alichoandika jamaa hapo ni kweli..?
 
Mimi sinaga hulka ya kumtesa mwanamke, najua wajibu wangu katika kumhakikishia furaha yake ingawa kuna kipindi nilishawahi kujifanyisha kauzu ili tu nimtie discpline maana nao ukiwalegezea sana wanakuwaga na pigo sizo!
 
Wavumilivu sana, unaweza wapa kila kitu cha gharama ila bado wakakusaliti macho makavu mchana kweupe.
 
Asante sana kwa ujumbe huu mkuu, kweli kabisa ni wavumilivu huwa Napata shida nikimuona mtu anamnyanyasa mwanamke kwa kiwango kilichopitiliza, tuwapende na kuwaheshimu pia, kukwaruzana kupo ila isifike mahali unamkosesha raha.
Umeoa? hahahahahahha yaani nimeshangaa mtu kulitambua hili hongera na mpe hongera mkeo kapata thaman kubwa
 
Back
Top Bottom