Ujumbe wangu kwa vijana wa vyuo vikuu

Ujumbe wangu kwa vijana wa vyuo vikuu

Dr wa Kaliua

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2020
Posts
1,634
Reaction score
3,883
Maisha ya chuo kikuu ni mafupi Sana, maisha ya chuo ni Kama ndoto ya kuota usiku na kuamka ahsubui kukiwa kumekucha.

Vijana wengi waliovyuoni huishi maisha ya kifahali Sana na kusahau uhalisia wa maisha yao.
Hii hutokea kwa baadhi ya hao WANAFUNZI kupata pesa za matumizi kutoka katika bodi ya Mikopo.

Vijana wa vyuo vikuu naomba mfahamu kuwa hiyo pesa mnayoipata ni ndogo Sana, rakini endapo utajibana na ukiwa na malengo unaweza kutoka kimaisha(niamini Mimi).

Wapo wanaosoma vyuo wakiwa kazini, wapo wanaosoma chuo wakiwa tayari wameandaliwa kazi.

Pia mpaka leo wapo ambao hawajui hata wanasoma Nini Hali ya kuwa wapo mwaka wa Pili au watatu.

Sasa ujumbe wangu upo kwa wale watoto wa masikini. Hakika wakifuata Yafutatayo wanaweza kufanikiwa katika maisha yao chuoni na baada ya chuo.

1. Mahusiano
usiingiie kwenye mahusiano kichwa kichwa, wapo walio poteza matumaini ya maisha yao kwa sababu ya mahusiano. Wapo walio maliza chuo wakiwa hawana hata asset moja ya maana kwa sababu ya mahusiano.

Hivyo Basi Hakuna mtu aliepoteza maisha kwa ajili ya kuwa single. Hivyo Tumia muda mwingi kutafuta mpenzi wako. Awe na sifa zifuatazo.

Moja, awe mwenye kujitambua, sikushauri uwe na mahusiano na mwanachuo mwenzako, atakupotezea muda, na mahusiano yatakuwa masomoni tu. Tafuta beki tatu mmoja, mwenye Imani ya Mungu, mbunifu, mchapakazi, mzuri, tulia nae panga nae malengo. Alafu baada ya miaka mitatu utakuja kunishukuru.

2.Marafiiki

Bora kukaa peke yako kuliko kukaa na marafiki wanafki, wapenda starehe, kumbuka wewe ni Mtoto wa masikini umekuja kutafuta maisha, hivyo Basi Bora uishi bila marafiki kuliko kuwa na marafiki wanafki, ambao watakuwa kikwazo Cha maisha yako.

3. Kaa peke yako
MTU yoyote Alie chuo kikuu ni mtu mzima, jiweke kwenye Hali Fulani ya kutafuta maisha, acha uswahili acha usela Anza maisha wewe Kama wewe hata Kama unalala chini, baada ya miaka miwili kila kitu kitakuwa Chako na Utakuwa na experience kubwa ya maisha.

4. Acha ulevi wa pombe
Kulewa sio sifa, acha kuiga watu, pombe ni hatari kwa maisha yako. Pombe ni chanzo Cha maambukizi ya virusi vya ukimwi.kuwa makini Sana, tumia pesa Kama una hamu ya kunywa nunua maziwa nunua asali kunywa kwa Afya yako na sio pombe..

5 wekeza
Anza kwa kununua asset mbalimbali, hata Kama kidogo kigogo Ila viwe vyako.

6. Fanya biashara
Chukua mkopo wa bodaboda, au BAjaji ingia barabarani pesa ya boom utaisahau.

7.kaa pembeni na wanafunzi

Usiiishi maisha ya wanafunzi panga ulaiani kwenye watu wa kawaida, ili kupata uhalisia wa Maisha.

Mwisho mtaani ni kugumu Yani kupata laki tano kwa miezi miwili sio Jambo rahisi.

Maisha ni magumu ajira Hakuna, ajira Hakuna malizeni chuo alafu mtakuja kunambia.

Karibu kwenye group langu la WhatsApp la wanafunzi wenye chachu ya mafanikio kwa nambari 0783855049.

Ili nikuunge tupeane michongo mbalimbali.
 
Sawa,ujumbe mzuri,nadhani utawafikia wahusika...
 
Ujumbe mzuri huu, ingawa pesa ya boom huwa ni ndogo ukilinganisha na watu wa uraiani wanavyofikiria
 
Big up bro, ushauri mzuri sana kwa freshers...ila kwa wanaosoma dar pesa ya boom huwa haitoshi kabisa kwasabb maisha ya dar yako juu sana..
ila kwa waliobahatika kusoma mikoani, trust me ukipanga malengo vizuri, pesa ya boom inakutoa kimaisha
 
kongole kwa ushauri mzuri kabisa...
 
Back
Top Bottom