Ujumbe wa wiki kwa kila mpenda AMANI Tanzania.

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,318
Wengi mlijiuliza walionteka ni maaskari?
Mkanitafuta vituo vyote central hadi stakishari
Wakasema… hawajui nilipo mama alienda hadi mochwari
Dah.....
Ya Kaisari mwachie Kaisari
Machozi yenu yatalipwa mimi nafunga na kusali

IMBA ROMA IMBA X3

Mungu wa Paulo… ndio Mungu wa daudi
Na ndio Mungu wa John mnayemuita Yohana wa Yahudi
Mwanangu alimuuliza, mama baba lini atarudi?
Na mke wangu aliwaliza kuwashukuru sinabudi

Fahamu yakuwa..

Me sio tu rappa pia ni baba wa familia
Na watoto mahitaji nawapa kama isemavyo biblia

Kipi bora?..

Nife museme nilikufa kiharakati?
Siogopi kufa… ila nnawaachaje waliobaki?

Je?..

Nani katiyenu mwanangu atampa malezi?
Wapi atapata mahitaji?
Wapi atapata mapenzi?
Mama naye?..
Wapi atapata mahitaj na malezi?
Na report ya upelelezi
Vipi akiteka mtekaji?

Je?…

Kaburi langu mtalipalilia majani?
Nimeumwa hamjakuja kuniona
Mnangoja mje msibani?
Nlipokuwepo skuwa nnajua hii saa nne hii saa nane
Nlichohitaji… nitoke mzima na ndugu zangu tuonane

Nimechapwa mijeledi
Nimevunjwa bila huruma
Ahsante mliopaza sauti
Nimeiona nguvu ya umma
Siku tatu nimefumbwa macho
Mikono nimefungwa nyuma....

NAKWENDAA ZIMBABWE ZIMAMA YELELE MAMA WEE X4

IMBA ROMA IMBAA...SEMA BABA WEEEE

Nasimama na nnaunga hoja kwenye uchumi wa viwanda
Nanasi linaoza msoga kibiti linaoza shamba
Walioniteka hawakuja na noah… ni uvumi na visanga
Ila KUTEKANATEKANA Ni uhuni wa kishamba…
Weka bunduki chini si tubishane kwa hoja
Maana sote lengo letu ni kuijenga Tanzania moja
Me skuona nyota kwa shoulder ila najua we ni soja

Inshaalah..

Ulikuja mwenyewe ama ulipewa order?

Ewalah..

Aminini siku hazigandi
We ni yanga me ni samba kuwa mpinzani sio dhambi
Ipo siku mtawala atakuwa mpinzani
Simba akichukua kombe sijui atapona nani?

Na kuna Mbunge alisema eti nimemtukana mkuu
Utahukumiwa na mkono wa Mungu… namshtakia aliye juu

Kwanza lini?
Na kwanini?
Me nimtukane mjomba?
Umepewa gari ya wagonjwa mimi Tanga nalililia bomba

Me mbarikiwa na nikifa kuume kwa baba ntaketi
Na mtu wa watu.. that’s why lilisimama bunge la
bajeti Kunijadili mtanzania kuwa MAKINI PIA MAKINIKIA
NAYATUNGIA MAPINI PIA

Me nlitabiri utakuwa rais kipindi unaitwa waziri
Japo maisha sio rahisi ila pongezi unastahili
Waliosadiki Roma ataonekana kabla ya Jumapili
God bless imetimia injili niliyoitabiri

NAKWENDAA ZIMBABWE ZIMAMA YELELE MAMA WEE X4

IMBA ROMA IMBAA
SEMA BABA WEEEE
 
Back
Top Bottom