Ujumbe wa siri kwa Vijana

Ujumbe wa siri kwa Vijana

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
39,580
Reaction score
91,889
UJUMBE WA SIRI KWA VIJANA.

Na, Robert Heriel.

Warembo, mabrazamen, mashalobaro, Slay Queen, Watanashati, Kwa vijana wote muishio Tanzania. Ikiwa unasoma ujumbe huu basi jua ya kuwa wewe ni kiumbe hai. Haijalishi una afya njema au laa. Basi jumbe hii imetoka kwangu, mimi kijana mwenzenu, naam ndiye Taikon wa Fasihi, kuhani katika hekalu jeusi.

Nikitumia nafasi ya wingi katika umoja wangu. Ndio huo uishio ndani yangu. Nawaandikia haya ili mpate kujua yawapasayo kufanya.

Nasi tuna nguvu, kuliko rika lolote lile. Nguvu ya mwili, wala sio hiyo pekee yake, nguvu ya akili, nayo sio hiyo peke yake, nguvu ya hisia ambazo zote zinatufanya tuwe watu bora katika habari za rika au hirimu kuliko rika lolote lile. Ingaweje rika zingine sio kama ni mbaya lakini haiondoi ubora wa rika la
ujana wetu.

Vijana, nguvu ya mwili, akili, na hisia ndio huamua maisha yetu ya baadaye. Huamua tujenge familia ya namna gani, ukoo wa namna gani, jamii ya namna gani, na taifa la namna gani. Ama kwa hakika mambo haya yanahitaji uangalifu na uzingatiaji katika kuyafanya katika maisha yetu ya kila siku.

Vijana, kutawala mambo hayo matatu(Mwili, akili na hisia) ni kujitawala na kujipa furaha ya maisha. Kushindwa kufanya hivyo ni kuruhusu mtu mwingine aje kukutawala. Hatuwezi kuyapa mambo hayo uhuru uliopitiliza kwani kwa kufanya hivyo ni kuruhusu maisha yawe huru kutuendesha. Kudhibiti uhuru wa mambo hayo matatu ni kuyadhibiti maisha kwa hakika.

Hatuwezi ruhusu akili zetu ziwaze jinsi zinavyotaka, au mtu fulani atakavyo. Hatuwezi ruhusu mwili uamua vile utakavyo, halikadhalika na hisia zetu. Ni wajibu wetu wa msingi kudhibiti mambo haya. Hata katika miili yetu viungo vyetu vina mipaka ya kiutendaji. Hivyo hata sisi kama vijana bora kuliko jamii yoyote ile, ni wajibu wetu kudhibiti mambo hayo matatu.

Hii ni kusema, hata watoto wetu lazima wadhibitiwe katika mambo ya mwili, namna zao za kufikiri na jinsi ya kuendesha hisia zao. Kwa kufanya hivi tutajenge jamii bora ambapo ndivyo tulivyo.

Mimi nami ni kijana, ninafahamu changamoto kama vijana wengine. Lakini kitu pekee ninachoweza kusema kwa muda huu tokea nimeingia rika hili ni kuwa; Kuendekeza nguvu moja pekee yake kati ya zile tatu nilizozitaja(mwili, akili na hisia) ni kupoteza mwelekeo. Lazima pawe na usawa katika mambo hayo matatu ili kuyafanya maisha yawe murua.

Vijana wengi kwa sasa wamejikita zaidi katika nguvu ya hisia, wengi muda wao mwingi huruhusu kufikiri mambo ya mapenzi zaidi kuliko kitu chochote. Mapenzi yanaongozwa na hisia. Kwa kufanya hivi wengi tumepoteza uelekeo wa maisha. Tumepoteza shabaha(focus) kwa mambo ya msingi. Mapenzi ni muhimu lakini sio muhimu kuliko mambo mengine. Maisha yanahitaji uwiano. Kufikiri jambo moja kila saa na kulifanya ni kupoteza furaha katika jambo jingine. Hata hivyo wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kuweka uwiano au msawazo kwenye mambo yetu lakini hiyo ndio njia bora ya kulinda furaha zetu.

Wengine wamejikita zaidi katika akili na kupuuzia mambo ya hisia, nao wamejikuta kwenye taabu za kutendwa na mambo ya hisia. Hata hivyo miili yao nayo imedhoofika Mpaka kufikia hatua afya zao zimedhorota na kupata maradhi yasiotibika.

Kujikita katika jambo moja katika ya mambo niliyoyataja huitwa ubinafsi na kuwadhuru wengine. Kwa mfano, watu wanaotumia akili na nguvu za mwili nyingi kutafuta pesa hujikuta katika shimo la ubinafsi wa kujilimbikizia mali nyingi na hiyo husababisha kuwafanya wengine kuwa masikini. Hii ni kutokana na ubinafsi wao kuwa kila fursa aionayo hutaka kuitumia. Kilimo yupo, biashara yupo, usafirishaji yupo na fursa zingine. Hii hupelekea wengine kukosa fursa na kuwa masikini.

Halikadhalika na watumiao hisia za mapenzi kujipatia wanawake wazuri au wanaume wazuri. Kila mwanamke atakayepita humtumia au kumuoa. Hii hupelekea wengine kuumia kwa namna ya kukosa wake wa kuwaoa au kama amepata basi mke kuchepuka kutokana na nguvu ya uvutano anayoitumia mwanaume mwingine kumvuta.

Vijana, siri ya maisha ipo katika uwiano wa kila jambo tulifanyalo. Kila jambo linahitaji tuwe na kiasi. Bila kiasi hakuna amani wala furaha. Kutafuta pesa nyingi ni kujiingiza katika shimo la majonzi. Pia kuwa masikini kupitiliza ni kujiingiza katika shimo la kilio. Lazima tujue namna ya kuweka uwiano wa mambo. Hata wanaotaka wanawake wengi hujikuta katika tabu na misongo ya mawazo. Mifarakano na migogoro ya kifamilia kamwe haiwezi kuisha kwenye ndoa za wake wengi. Hilo halina ubishi. Tunajua migogoro hata kwenye ndoa ya mke mmoja ipo, lakini haiwezi kulingana na ya wake wengi.

Vijana, tunajua umri hausubiri, unaenda kwa kasi. Hatuwezi kusubira watu wengine wafikiri badala yetu. Hivyo ni kujiingiza katika utumwa wa kifikra. Hatuwezi kufanikiwa kwa kusubiri wengine watufikirie sisi cha kufanya, tena tusubirie wengine watutafutie kazi za kuendesha maisha yetu. Hivyo ni dalili ya matumizi mabovu ya akili na nguvu na kuendekeza hisia mbaya za upendo wa wazazi au jamii yetu. Hatuwezi kufikiri tunapendwa kama watoto wadogo ili wazazi wetu watutafutie kazi, ati jamii zetu zitupe kazi.

Sisi sio watoto tena mpaka tusubiri mapenzi ya wazazi wetu. Tusubiri kufanyiwa kila kitu.

Tunajua akili zetu zinanguvu kuliko wazee wetu, zinanguvu kuliko watoto wetu. Tunajua tuna miili yenye nguvu kuliko wazee wetu na watoto wetu. Hisia zetu zinafanya kazi zaidi kuliko wao. Sasa kwa nini tutegemee badala ya kutegemewa.

Akili ilibuni Elimu. Hivyo elimu sharti iisaidie akili kubuni mambo mengine yenye tija kwa jamii zetu. Kusoma na kupata elimu fulani iwe chachu ya kupata mabadiliko chanya katika jamii zetu. Sio lazima kile tulichokisomea ndio tukifanyie kazi. Tunaweza somea fani fulani lakini tukaitumia fani hiyo kufanya fani nyingine.

Vijana wenye elimu lazima tujue kuwa; tumepata elimu ili kubuni kazi na kuzipa hadhi yenye kuheshimiwa katika jamii. Pia tutupaswa kutumia elimu zetu kuzigeuza kazi zilizokuwa zinaonekana hazina maana kuzifanya ziwe na maana. Mfano; kazi za kuuza karanga, kushona viatu, fundi nguo, bodaboda na kazi zingine. Tunapaswa kuzigeuza na kuzipa thamani ziwe kazi za heshima.

Kusoma sio kudharau kazi zingine au fani nyingine. Kusoma ni kuzipa heshima kazi zinazotuhudumia katika maisha yetu.

Vijana, lazima tuelewe kuwa; kuheshimu kazi ni chanzo cha ubunifu na mafanikio katika kazi hiyo. Kazi yoyote ile ni bora kutegmeana na anayeifanya.

Vijana, yote hayo yatafanyika endapo tutaweza kuweka uwiano wa mwili, akili na hisia.

Ukiwekeza zaidi kwenye kimoja, utapoteza viwili vya msingi ambavyo vitaathiri furaha yako.

Kulalamika sana ni matokeo ya matumizi mabovu ya akili. Ni dalili ya kuendekeza hisia kuliko akili na nguvu ya mwili. Lazima utambue kuwa hakuna aliyekuwa kwa ajili yako hapa duniani. Bali wewe ndio upo kwa ajili ya wengine. Ukilijua hili hutamlaumu yeyote na utafanikiwa.

Weka uwiano baina ya Nguvu ya mwili, akili na Hisia kwa mustakabali wa furaha ya maisha yako.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300 au 0711345431
 
Full comedy hii nchi, kijana yupo radhi ale tunda kimasihara anakataa mishe ya laki 2, baada ya kula tunda kimasihara unaanza kutusumbua tumkope elf 2
 
Kijana hii staili yako ya kuandika kwa kirefu.sio ya kispoti spoti hongera sana lkn
 
Back
Top Bottom