Ujumbe wa matumaini.

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Kizazi chetu kinakabiliwa na changamoto nyingi sana kama Taifa. Tumeridhi taifa ambalo limegawanyika na lisilokuwa na malengo ya pamoja wala maono. Kiwango cha uzalendo wa watu wetu kimeshuka mno katika hali ya kuogopesha na kunifanya nijiulize ni wapi tunaelekea. Taifa hili linahitaji uongozi na dira. Linahitaji atayeleta upya uzalendo na kuamsha roho ya kulitumikia Taifa hili kwa watu wote.
Watu wa Taifa hili lazima wahisi utaifa wao ndani ya roho zao na wawe tayari kulitumikia. Sisi ni watu wamoja. Majaliwa yetu ni mamoja kama Taifa. Naamini kama tukiji organize kwa pamoja kukabiliana na matatizo yanayotukabili kama Taifa bila ya ubinfasi tutafika. Ni lazima tujue ni wapi tunataka kwenda kama Taifa. Ni nini azma yetu na malengo yetu. Taifa hili halijazaliwa kusudi liwe ombaomba, tuna nafasi ya kukua kama tukilipenda na kulitumikia Taifa hili.

Tunapozungumzia mabadiliko ni pamoja na kulipenda Taifa hili, kupenda Raia wenzako kwa moyo wote na kuwa Tayari kuwatumikia. Ukweli ni kwamba hatujawa Taifa kusudi tunyonyane au kundi moja likandamize kundi jingine. Tumekuwa Taifa ili tufikie kilelele fulani cha mafanikio na ndio hasa itakayo kuwa sababu ya furaha yetu kama Taifa. Mafanikio yetu ya pamoja iwe ndio furaha yetu. Lazima tukumbuke tunawajibu kwa vizazi vijavyo, ni sisi tunaotengeneza baadae ya vizazi vyetu. Lazima tuvipende vizazi vyetu ambavyo havijazaliwa kwa kuwatengenezea mazingira bora kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa kupendana kama raia wa Taifa hili. Tumaini hili lazima lizame katika mioyo yetu. Lazima tujue tunapotaka kwenda kama Taifa.

Ukweli ni kwamba , hatutaweza kulijenga Taifa hili pasipo kulipenda kwanza. Ni lazima tulipende kwanza ndipo tutakapo litumikia kwa mioyo yetu yote. Tujenge Taifa ambalo Raia wanaheshimiana kwa dhati na kushirikiana katika ujenzi wa Taifa lao na viongozi wakitenda Haki na kuwajibika. Hili ndilo Taifa ninalo lihitaji . Ambalo wanawake na wanaume wanashirikiana na kuheshiamiana katika ujenzi wa Taifa lao, ambalo wazazi wanawajibika kwa pamoja katika malezi ya watoto. Hatujawa Taifa kusudi kila mmoja ajiangalie mwenyewe, tunawajibu kwa kila mmoja wetu.. Tunachohitaji ni Taifa hili kusonga mbele kwa nguvu ya umoja wetu. Sisi ni Watanzania na ni lazima tuungane pamoja ili tupambane na matatizo yanayotukabili sasa hivi, ili tupambane na uovu unaolikabili Taifa hili.

Tuna changamoto za rushwa, uzembe na kutokuwajibika kwa watu waliopewa dhamana. Wakati wa kutawalaiwa kama waafrika na kama watu weusi ni lazima uishe kwa kuamua sasa na kwa dhati kuwa wamoja na kutia juhudi katika kujikomboa. Nina amini kwa dhati kabisa tunauwezo wa kuwa Taifa kubwa kama mataifa mengine. Ni jitihada zetu na kujitolea kwetu na dhamira yetu isiyififia ya kuleta mabadiliko. Ya kuona maisha ya mwafrika na mtanzania yakibadilika. Natumaini siku moja kuona WANAUME KWA WANAWAKE WAKIJITOLEA KWA DHATI KULITUMIKIA TAIFA HILI. Mabadiliko haya lazima yaje na yaonekane. Kwa juhudi za pamoja ni lazima tutashinda kama tumedhamiria kwa pamoja kukusanya nguvu zetu na uwezo wetu wa kiakili. Watanzania tuna uwezo wa kuwa Taifa kubwa.

Nafikiri tofauti kuhusu Taifa hili. Naliona katika macho ya uwezekano. Taifa hili linauwezo wa kuwa kitu chochote linachotaka ni juhudi zetu na umoja wetu na jitihada zetu zisi zisizofifia.

Katika kizazi chetu leo hii tuna viongozi wanaogawa watu na kuondoa umoja wetu ambao ni nguvu yetu ya kuleta maendeleo. Uchu na ubinafsi umetamalaki. Wajibu wetu wa dhati kwa kila mmoja wetu ni kuliona Taifa hili likisonga mbele ni kuona Taifa hili likisonga mbele na kuliletea heshima yake.. Vijana wa Taifa hili ambao tunaishi sasa tunawajibu huu, majaliwa ya taifa hili yanatutegemea sisi ni lazima tuwe Taifa lenye malengo. Ni lazima tuwe taifa lenye ushawishi na nguvu. Ni lazima vijana tujikusanye tufanye mapinduzi haya kwa faida ya Taifa na heshima yetu na vizazi vyetu vingi vijavyo.. Hili ni lazima tulidhamirie. We must have a fighting spirit. The spirit of those who conquer and not conquered. Ili tuwahadidhie watoto wetu jitihada zetu na mafanikio yetu tuliyoyaleta kwa Taifa letu, lazima tuwe na kitu cha kuwaelezea vizazi vyetu vijavyo ni nini tumefanya kwa Taifa letu. Ni lazima tuwe Taifa la washindi.. lazima tuwe wamoja.

MABADILIKO YA KWELI YATAKUJA KAMA TUKIWA WAMOJA NA KAMA TUKIBADILI MITAZAMO YETU KUHUSU TAIFA LETU. WATOTO WETU NI LAZIMA WALIPENDE TAIFA HILI KAMA WANAVYOJIPENDA WENYEWE.. TUMAINI LANGU HALITOFIFIA KWA WATU WA TAIFA HILI NA BAADAE YETU. UPENDO WANGU UENDE KWA WATANZANIA WOTE NA UJUMBE HUU WA MATUMAINI KWA BAADE YETU.
 
Back
Top Bottom