Ujumbe toka udsm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe toka udsm

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yona F. Maro, Feb 1, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  TUAMKE JAMANI TUSILALE, MAPAMBANO BADO........
  Napenda kwanza kutoa shukurani zangu za dhati kabisa kwenu ninyi wanachuo
  wenzangu kwa mshikamano mliouonyesha kipindi chote cha mapambano dhidi ya
  sera kandamizi na dhalimu ya uchangiaji wa elimu ya juu. Hii inadhihirisha
  wazi ni jinsi gani tulivyo wazalendo na kuonyesha ukomavu wa kifikra katika
  kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya Taifa letu. Nawahakikishieni ndugu zangu
  anayedhania mabadiliko ya kweli yatatokea kwa kuibembeleza serikali ajue
  anakosea sana. Naimani wengi wetu tumerudi salama chuoni, poleni kwa
  matatizo yote yaliyotusibu kwa kipindi chote tulichokuwa uraiani naaimani
  kila mmoja wetu amekuwa barozi mzuri katika kuuelimisha uma wa watanzania
  kuelewa kiini hasa cha tatizo ni nini. Hatuna sababu yoyote ile ya msingi ya
  kujilaumu kwa mgomo wetu, kwani tulikuwa tunapigania mustakabari wa maisha
  ya watanzania masikini na mabadiliko kidogo tumeyaona ingawaje hatujafikia
  lengo letu. Cha kusikitisha labda ni wenzetu waliopoteza maisha katika ajali
  ya basi kule singida, ambapo baadhi yetu pia walipata majeraha. Mwenyezi
  mungu awarehemu na zawadi pekee tuliyonayo kwao ni kufanikisha vita hii
  tuliyoianza pamoja. Kilicho mbele yetu hivi sasa ni kuendeleza wimbi la
  mapambano tena safari hii ajenda zetu za msingi ni kuuondoa utawala wa
  kisiasa chuoni, kurejesha wenzetu chuoni, kupigania muhimiri wetu DARUSO
  pamoja na kuizika na kuitokomeza kabisa sera ya uchangiaji. Wakati huu ni wa
  pekee katika historia ya nchi yetu ambapo vijana hasa wasomi ni nguvu ya
  mabadiliko, tukikaa kimya historia hii ndugu zangu itatuhukumu. Najua wengi
  wetu sasa hivi tumejawa na roho za uoga wa kinafiki, lakini jua kabisa fika
  hiyo siyo sirika ya msomi tena wa chuo kikuu mlimani ambayo ni uwezo wa
  kuhoji yanayokubalika na kukataa vitu vya kishenzi vilivyozoeleka na
  visivokubalika mbele ya wapigania haki. Kwa sababu tunapokataa tunajenga
  hoja ya msingi kuonyesha jinsi gani hatukubaliani na maamuzi yanayofanywa
  kisiasa zaidi na kutukandamiza sie wanafunzi. Wote tunakumbuka fedha ya
  matibabu iliunganishwa kwenye ada ya mwanafunzi kwa mwaka wa masomo wa jana
  (2006/07) na tukatangaziwa na huyo Mkaliandara pale Nkrumah, na hata mwaka
  huu wa masomo kabla ya chuo hakijafungwa ilieleweka hivyo, lakini sasa
  tumelazimishwa kulipia gharama za ziada shilingi 50,000 eti za matibabu.
  Jamani hela zetu hizo ndizo zilikuwa zikitumika kujaza mafuta ya AURORA za
  Mkaliandara, kuwalipa wale washenzi FFU na kulipa allowances za kina BUSH
  pale getini geti maji. Leo ni wiki ya tatu tangu chuo kifunguliwe mpaka hivi
  sasa watu hatuna pesa sababu eti bado wanaendelea kuprocess kutokana na
  batch za malipo, tena wengine wanawekewa laki tatu, wengine laki nne na
  wengine laki sita au siku hizi kwenye bum kuna grade?. Huo ndiyo wizi
  tunaoukataa jamani tukigoma wanatuita wahuni, tusipokuwa makini fedha zetu
  hizi zitakuwa zinafisadiwa, kuna umuhimu wa kuipigania DARUSO yetu. Leo hii
  tumerudi chuoni mtu ulikuwa na chumba awali na ulikilipia semistor nzima,
  lakini sasa hivi unanyang'anywa tena bila kulipwa hata fidia anapewa mtu
  mwingine ambaye alikuwa hana chumba kisa umechelewa kulipa, kweli hiyo ni
  haki?. Sisemi mliopata mnyang'anywe ila tulipwe tulionyang'anywa. Bei ya
  vitu zimepanda maradufu si cafteria wala stationary tena hawana huruma
  kabisa wanadai mambo yamebadilika, je hayo mambo mbona hayakubadilika awali
  yabadilike leo hii kisa hatuna uongozi wa DARUSO? Tunakatazwa tusibebane
  tena kwa kukaguliwa kwa usumbufu mkubwa na wafanyakazi wa ofisi ya dean of
  students usiku wa manane, kweli hiyo ndiyo kazi ya mlezi na bila kubebana
  tutaweza kuishi ndugu zangu? Tujiulize kwa nini cafteria ya DARUSO
  imevunjwa? Eti kwa sababu mapato yake yanaingia DARUSO ndiyo yanatupa kiburi
  sie wanafunzi kugoma tena huyo ni proffesor mzima ndiyo anachangia hoja hiyo
  kwenye panel badala ya kuainisha kiini cha tatizo. Kweli huku ni kufirisika
  kimawazo kwa uongozi wetu wa chuo na kuzidi kutawaliwa na fikra za kisiasa.
  Ndugu zangu kisheria udahili wetu haukufutwa sie bado ni wanafunzi halali wa
  chuo kiku cha Tanzania, registration number zetu ni zile zile, matokeo yetu
  ni yaleyale yanaendelea kutumika, iweje leo sasa uniambie eti viongozi wetu
  wamepoteza sifa za kuwa viongozi kisa tumedahiriwa upya. Huu ni wizi mtupu
  na propaganda za kisiasa za ndugu yetu Mkaliandara, suala la kutengenezewa
  vitambulisho vipya lilikuwa ni la lazima ili kurekebisha expiring date na
  ndiyo maana tarehe ya kuexpire ni sawa kwa wanafunzi wote, na mtakaobakia
  chuoni mtarudishiwa vitambulisho vyenu vya zamani. Ndugu zangu wasomi haya
  yote yanafanyika kwa sababu hatuna chombo chetu cha kututetea, huu tena siyo
  wakati wa kuogopa ni kusimama imara na kupigania kuirudisha madarakani
  serikali yetu ya DARUSO. Tukulifanikisha hilo wale wenzangu na mimi
  tuliyonyang'anywa vyumba tutalipwa peza zetu pamoja na fidia juu kwa sababu
  wametusitishia mkataba ghafla bila kupewa notes, fedha za matibabu
  zitaeleweka tulizichangia kwa msingi ipi? Na hizo cafteria na stationary
  ambao wamiliki wake ni wao wenyewe watatueleza ni kwa nini wamepandisha bei
  ya vitu hovyo? Na itawezesha pia wenzetu walioko nje kwa ajili ya umasikini
  wetu wanarudi chuoni haraka iwezekanavyo pamoja na mwanaharakati,
  mpambanaji, ndugu yetu mpendwa na mtetezi wa haki za masikini raia wa Uganda
  Silas Kefar Odong Odwar ambaye alifutiwa kibali cha kuishi nchini kwa
  propaganda za kisiasa na kuondolewa nchini mara moja anaungana nasi.
  Tusipokaa chini na kubadili mwelekeo wa fikra zetu hivi sasa, tutajikuta
  tumepelekwa tusikotaka kwenda na tusijue tumefikaje huko, kwa pamoja
  tunaweza "The greatness of our survival here at the hill is not a given we
  must fight for it and solidarity will be only our truly mace" Aluta continua
  vita bado inaendelea tusiogope tuimarishe ushirikiano wetu tukutane
  REVOLUTIONARY SQUARE kwa mikakati zaidi nchi hii ni yetu lazima
  tuipiganie.Ni mimi mtoto wa masikini tuwasiliane kupitia
  masikin...@yahoo.com
   
 2. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Walikubali tshirt za kijani na njano, wakapikiwa pilau na wakapelekewa mabasi wakajiona wajanja sana. Sisi tuliumia sana kwa usaliti wenu wakati ule kuona jamii ya kisomi ikifanya mambo ya kihuni kabisa lakini tulikuwa hatuna cha kufanya uchaguzi ulikuwa wenu. sasa mnaona nyota nyota mnaanza kulialia. Mimi nawaambia na bado usaliti wenu kwa nchi utawatokea puani kwani hili ni part gazeti tu. mafisadi wamehiaribu nchi hata mtakao maliza chuo kwa uchungu ( kama Hawa alivyoambia baada ya dhabi yake kuwa utazaa kwa uchungu) kazi hakuna kwa hiyo mtaendelea kula pilau ya pale diamond na kuvaa Tshirt a kijani na njano nyie watoto wa wakulima na wafanyakazi shame on you!

  Na hii ni zawadi yenu wote mliofanya ule usaliti ili muweze kutubu kwa nchi na kwa wote waliowategemea muwatetee Mithali 1: 8-19
  8 Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, wala usiache sheria ya mama yako
  9 Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, na mkufu shingoni mwako.
  10 Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi wewe usikubali
  11. Wakisema "haya! njoo pamoja nasi na tuvizie ili kumwaga damu tumwotee asiye na hatia, bila sababu
  12 tuwameze hai kama kuzimu na wazima , kama wao washukao shimoni
  13 Tutapata mali yote ya thamani tutazijaza nyumba zetu mateka
  14 Wewe utashirikiana nasi tutakuwa na vitu vyote shirika
  15 Mwanangu, usiende njiani pamoja nao uzuie mguu wako usiende katika mapito yao
  16 Maana miguu yao huenda mbio maovuni, nao hufanya haraka ili kumwaga damu
  17 Kwa kuwa mtego hutegwa bure, mbele ya macho ya ndege yeyote
  18 Na hao hujitolea damu yao wenyewe hujinyemelea nafsi zao wenyewe
  19 Ndivyo zilivyo njia za kila mwenye tamaa ya mali huuondoa uhai wao walio nayo
   
  Last edited: Feb 1, 2009
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ndio hivyo wote utawaona mstari wa mbele kuipigia debe CCM na wache huwepo katika upinzani na sasa nasikia au wameshafungua Tawi la CCM na wamejiunga eti ni wakereketwa wakuu.
   
 4. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
   
 5. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
   
 6. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
   
Loading...