Ujumbe mzito kwa Rais Magufuli

Supervision

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
265
203
Mheshimiwa Rais pole kwa kazi, lakini naomba nichukue wakati wangu kuandika au kukueleza hiki ambacho sina uhakika kama kitakufikia au hakitakufikia. Lakini kwa imani na mapenzi ya taifa langu nitaandika pasipo kujali kama ujumbe huu utafika au haufiki ila naamini wapo watanzania watakaosoma.

Mheshimiwa umeingia madarakani ukiwa na vision ya mapinduzi ya viwanda, sawa ni nzuri sana ila tuangalie njia ya kupita. Vision ambayo nilikuwa natafuta ama nina ndoto ya kumsikia raisi atokee na kuisimamia.

Lakini katika kutimiza ndoto hii kuna namna ambayo naona tunaweza kuchemka nikirudi mbali na kupekua document mbalimbali, tunaona wazi kuwa nchi zote duniani ambazo zilifanya mapinduzi ya viwanda zilianza na kilimo.Bila kufanya mapinduzi ya kilimo Baba itakuwa ni ndoto ya mchana.

Angalia China, Marekani, Uingereza, Ubelgiji na kwingineko, walianza na mapinduzi ya kilimo. Nikitazama katika taifa la Tanzania kwanza naona ardhi ipo ya kutosha ila hakuna jitihada za dhati. Kwani tungeweza kwenda mbali kuliko ambavyo tumejaribu.

Kwanza ili viwanda viwepo ni lazima malighafi iwepo ya kutosha kisha kupata malighafi ya kutosha kwasababu viwanda vingi hutegemea mali ghafi basi sekta ya viwanda ingeweza kufanikiwa na endapo mali ghafi inatoka nchini basi hata uwezekano wa kuuza bdhaa zinazotokana na viwanda kwa bei rahisi ni rahisi mno,kwani malighafi hazifuuatwi kwa gharama kubwa.

Mheshimiwa raisi sababu nyingine ya kuweza kufanikiwa kiviwanda kupitia kilimo ni kwamba Uingereza, China na Marekani walipata faida kubwa kupitia kilimo baada ya kupata mazao mengi hivyo kuuza na kupelekea kupata mtaji ulioweza kuwafanya waanzishe viwanda na kuongeza uwekezaji katika kilimo. Mheshimiwa Magufuli hapa nchini tuna maeneo mengi makubwa lakini wananchi wanashindwa kuyatumia wakitegemea mvua na maeneo mengine mvua ni za kuungaunga.

Mheshimiwa raisi ukitaka kufanya nchi iendelee kiviwanda ni lazima tuhakikishe kwanza tunalima mwaka mzima na kilimo kinaleta tija ili kupata malighafi na kukuza uchumi ikiwemo hali za wananchi kwani wengi hutegemea kilimo.

Eneo la mikoa ya kati kama Dodoma, Singida na ya mikoa ya magharibi watu wanatakiwa kupata maji mwaka mzima kwani hawana mvua za kutosha lakini eneo hili lina rutuba ya kutosha. Mikoa mingine iliyobaki yapo maeneo yanayopata mvua za wasiwasi kama Tanga na mikoa mingine michache. Ukija mikoa ya nyanda za juu kusini hawa wamebarikiwa kupata mvua na siku mvua ikigoma mikoa hii nchi nzima itakumbwa na njaa. Mikoa kama Mbeya, Iringa, Ruvuma, Njombe na Rukwa na hata Morogoro inalima mazao kwa wingi ila hutegemea mvua.

Lakini kama kutakuwa na mpango wa kupeleka maji taka kwa ajili ya kilimo vijijini basi nina uhakika maeneo mengi wananchi wangekuwa wanalima mwaka mzima na wangekuwa kiuchumi kwani maeneo haya watu hawalimi kama inavyotakiwa.

Ukitaka taifa watu wapige kazi basi waboreshee miundombinu. Kama hakuna mapinduzi ya kilimo,mapinduzi ya viwanda ni ndoto. Mataifa mengi yaliyoendelea kiviwanda yalianza kuboresha kilimo. Ukiweka miundombinu katika kilimo watu watapata soko hadi nje ya nchi na mwishowe watapata pesa za kuanzisha kuongeza uchumi kwa taifa.
Yako mengi ila leo naishia hapa.

NISAIDIE KUSHARE
 
Back
Top Bottom