Ujumbe maalum kwa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe maalum kwa serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by abdulahsaf, May 31, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][/h]Written by Stonetown (Kiongozi) // 31/05/2012 // Habari // 6 Comments

  [​IMG]
  Ujumbe kwa Mheshimiwa Waziri Mohammed Aboud Zanzibar
  Kwanza nichukue nafasi hii kumshukuru Allah (S.W) kwa ruzuku aliyotujaalia ya uhai. Pia nachukuwa nafasi hii kumpa sifa Jemedari wetu, kipenzi cha Allah na Kiongozi wa Umma huu wa mwisho Mtume wetu Muhaamad (S.A.W). Hekma, busara na uaminifu aliokuwa nao Muhammad kwa watu wa Mecca na duniani kote ulimpa heshima si miongoni mwa waislamu pekee, lakini hata makafiri ambao kwa pamoja walimpa jina la “Al-amin” na kumfanya ndie mtu pekee aliyepewa jukumu la kuhifadhi fedha na amana mbali mbali za makafiri hao.
  Natoa ujumbe huu kwa Mh. Waziri Mohammed Aboud nikiwa hapa Mwanza katika chuo cha St. Augustine University of Tanzania (SAUT) nikichukuwa shahada yangu ya pili katika fani ambayo ninaipenda sana ya ualimu. Ingawa ni fani inayodharaulika ndani ya jamii (sifahamu nani kachangia hili) lakini kwangu kabla ya kuthamini hayo mengine naamini kwamba watu walioelimika si tu kwamba wanajitambuwa wao wenyewe lakini pia viongozi wetu watukufu huamini kwamba, watu wanaowaongoza si wajinga; tofauti na ilivyo sasa. Ndio maana nahisi nina jukumu la kubaki kwenye fani hii kwa maisha yangu yote ya hapa duniani nikiamini labda naweza kutoa mchango kwa kile Allah atakachoniruzuku.
  Hapa Mwanza, kama ilivyo mikoa mengine ya huku bara habari inayozungumzwa sana ni inayohusu matukio ya hivi karibuni yaliyotokea katika visiwa vyetu vya Zanzibar. Kutokana na kutangazwa sana redioni, kwenye tv na kuandikwa na magazeti mbali mbali, habari hizi zimejenga hamasa kwa vijana wa hapa chuoni kujadili kwa hisia kali. Mbaya zaidi mijadala hii inahamia hata sehemu ambazo tumepanga vyumba vya kuishi. Niseme kwamba wakristo- vijana wa hapa chuoni wamekereka na yaliyotokea huko, kiasi cha kupayuka maneno kwamba “hawa wazanzibari ni washenzi sana”. Kwa mtu ambae ni mgeni na sijui hata pa kukimbiliya likitokea la kutokea (Allah atuepushie mbali), lazima niseme wazi kwamba nimetandwa na hofu na inawezekana hofu hii ipo hata kwa Wazanzibar wengine wanaosoma katika chuo hichi.
  Nimefuatiliya kwa ukaribu viongozi wakuu wa serikali ya SMZ ambao wanaonekana mstari wa mbele kushughulikiya kadhiya hii na inavyoonekana jukumu hili umekabidhiwa wewe kwani katika mitandao mbali mbali ya kijamii na ile ya blogspot picha tofauti tofauti zinaonekana ukiwa katika ziara za kuwafariji wahanga. Kwangu mimi sidhani kama hilo ni jambo baya ukichukuliya wewe ni mtumishi wa serikali ya watu wote. Mbali na hilo jengine lilonishawishi kutuma ujumbe huu ni hizi kauli ambazo nakuwa nazisoma kwenye vyombo vya habari ambazo unazitoa. Ukiachiya serikali kuahidi kuwatafuta wahalifu na kuwachukuliya hatua kali ili iwe fundisho (sijui kama serikali ishakuwa mahakama), lakini hii kauli ya kusema kwamba serikali imekosea sana kuwaruhusu Jumuiya ya Muamsho kufanya mihadhara ambayo ndani yake walikuwa wanafanya siasa badala ya kutangaza dini na mila za kiislamu. Sijui ni serikali ipi ambayo imekosea kati ya mbili tulizonazo lakini inawezakana ni ya SMZ.
  Mh. Waziri kauli hizi zinatuleteya matatizo makubwa hapa chuoni na kwa kweli zinatupa wakati mgumu sana kuweza kuelezea jambo ambalo SMZ imeshakiri udhaifu. Kwa taaluma yangu ndogo niliyonayo juu ya utawala ninaamini kwamba serikali huwa haikosei kwani serikali ni Wazanzibar wote, ila kiongozi wa serikali anakosea. Na ndio maana Naibu Katibu mkuu wa CCM Zanzibar yeye hakuidhalilisha serikali na badala yake alimnyooshea kidole Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar kwamba yeye ndie chanzo cha yote hayo kwani amefeli kumshauri Rais namna bora ya kudhibiti vikundi hivi vya kidini na kumtaka kuwajibika kisiasa (kujiuzulu). Sasa mheshimiwa unapotamka serikali imekosea ina maana Wazanzibar wote tumekosea? Au kwa tafsiri yako serikali ni ipi? Na kama unakiri hadharani mapungufu ya serikali kuwa inakosea sisi watu wa kawaida mnatupa ujumbe gani juu ya kuwaamini viongozi wa aina yenu? Au mheshimiwa hawa vijana wa Kizanzibar kukimbiliya kuwasikiliza Maimamu wa Misikiti badala ya kuisikiliza serikali ni kutokana na makosa serikali inayoyafanya kiasi kwamba vijana wengi hawana imani nayo? Maswali ni mengi…
  Mheshimiwa vyombo vya habari vipo kwa ajili kuripoti matukio zikiwemo kauli za viongozi kama wewe. Lakini ujuwe kwamba namna ya habari hiyo itakavyoripotiwa kwa msikilizaji au msomaji ni vile inavyoweza kuuzika na kumfanya msomaji au msikilizaji kuifuatiliya. Habari hizi za Zanzibar zinaandikwa kwa misingi hiyo, jambo linalofanya sisi tulio vyuoni kunyooshewa vidole. Mheshimiwa hebu fikiria kama kungetokea kifo cha angalau watu wawili na wengine kujeruhiwa; hali yetu huku ingekuwaje? Kwa hisia zilivyo huku habari ingekuwa tofauti kabisa. Mheshimiwa ingawa umeonesha kuwajibikia serikali ambayo haishabikii dini yoyote lakini ni vyema ukaangaliya athari za kauli unazotowa. Kumbuka Wazanzibari tumeenea sehemu mbali mbali za bara kwa shughuli za kutafuta ikiwemo elimu, biashara na kuna wafanyakazi wa Jamhuri ya Muungano. Kama serikali imekosea basi kayaseme hayo kwenye baraza la Mapinduzi lakini usivipe vyombo vya habari kuripoti kitu ambacho kinaweza kujenga tafsiri mbaya kwa sisi tulio bara muda huu na kutuweka na wasi wasi wa usalama wetu.
  Kama umeamuwa kulivalia njuga suala hili mimi sina tatizo lakini ni vyema ukawa makini hasa unapozungumza na watu ambao ni wahanga wa hilo tukio. Zanzibar tuna historia ya kupigwa mara kwa mara na vyombo vya dola na ukiangalia mazingira ya vipigo hivyo tunavisabisha sisi wenyewe labda kiushabuiki au kwa chuki za kisiasa na kauli kama hizi za kwako. Kwani watakaokuja kututwanga mabomu na virungu mtakuwa mmewapa baraka zenu nyinyi viongozi. Matokeo yake ni athari mbaya kwetu sisi kuliko hata hao wanaotekeleza vipigo hivyo. Mheshimiwa serikali inapokosea maana yake ihukumiwe, je muheshimiwa una maana ya kuiambiya serikali ya Tanzania ije ituhukumu? Na kama ni hivyo wewe utafaidika nini? Au watu wa Tanzania wakiamua kutuhukumu huku tuliko utajisikiaje? Ni vyema wanasiasa mnapozungumza matukio ya hatari kama haya mkatoa kauli za kupunguza mambo badala ya kauli za kukuza mambao yenyewe. Busara ni kitu cha msingi sana kwa kiongozi na wala sio kukurupuka na kutoa kauli zisizo na tija kwa Taifa.
  Zanzibar ni ya wazanzibar bila kujali dini, rangi wala eneo mtu analotoka. Tafsiri nyengine yoyote tofauti na hii haiwezi kuwa sahihi. Na ni vyema kama yanatokea matukio visiwani mwetu tukayachukuliya kama ya kwetu na si kuwapa watu wakayatangaza kama wanavyotaka wao. Tusione fahari kunukuliwa na vyombo mbali mbali vya habari kutoka bara tukaona huo ndio ufahari na kuwajibika, ukweli ni kwamba vingi ya vyombo hivyo vina mtazamo hasi juu watu wa Zanzibar. Mheshimiwa nayaandika haya kwa masikitiko makubwa. Na kama hujui mheshimiwa watu wa kawaida wa huku bara wanawaona watu wa visiwani kuwa ni kero kubwa na heshima iliyopo kwao ni kwa sababu ya muungano tu. Na ujuwe kwamba kama ambavyo wazanzibar hawautaki muungano ndo hali iko hivyo hivyo kwa wananchi wa huku bara. Na wengi hata hawaujuwi maana yake ni nini? Kwa hiyo matukio kama haya na matamko mnayotoa kwa kweli hayajengi bali yanabomoa kabisa. Ni vyema mnapobeba majukumu kuweni kama viongozi wa wananchi na wala si wa ksiasa au wa kichama, nyinyi mnaweza mkavizamisha visiwa hivi na mwisho wa siku tukawa wote ni watumwa wa bwana mmoja. Zanzibar Kwanza mengine baadae…
  Nimalizie kwa kumshukuru Allah (S.W) kwa uwezo alionipa wa kuandika haya madogo ambayo kwa uwezo wake yanaweza kusaisdia kwa wale wanaotaka kufahamu.
  Mungu ibariki Zanzibar na watu wake.
  Ameen!!!
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Abdulahsaf, pole sana! nimesoma maelezo yako nikiwa nimetulia sana, nikwambie mkuu, pamoja na kutuambia kuwa wvewve ni msomi, bado HUJITAMBUI!!!! hujaongelea kama vurugu za kizanzibari kule zanzibari ni sahihi au la? nikupe majibu na athari zake uchague 1. kama ni sahihi subirini kushikishwa adabu si huku bara tu mtafuatwa hadi mkondoni!!!!!! 2. kama si sahihi muwaonye ndugu zenu wa damu wakuoneeni huruma wajionee huruma na wao pia. kama vipi mnao wawakilishi bungeni watumieni kwa kanuni, ama muswada binafsi ili kwa umoja wao muipate zanzibari yenu. ondoeni uhuni barabarani , tunakumbuka almanusura G55 itupatie tanganyika yetu bungeni enzi za waziri mkuu MALECHELA, tulipogonga mwamba hatukushambulia madeli ya wauza juisi wa kiunguja kule buguruni!!! usimtwike waziri furushi la lawama kwa ujinga wenu!! mbaya zaidi mnamshikisha na mungu wenu kwenye upuuzi huo. siku kikinuka mkamuita kwa msaada atawaambia mlizitumaini akili na nguvu za miili yenu endeleeni na kupumbazika kwenu!!!!, wakati huo kama si mabomu uloyasema, basi mkitawaliwa na mwarabu ama m-bara. mna nafasi ndogo sana ya kuwa huru kama kwa sasa hamjui kuwa mko huru na mnaitawala tanganyika!!!
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Unaanzisha uzi na kukimbia, vipi bwana abdu!!
   
Loading...