Ujumbe kwenda kwa Watumishi wa Majeshi: Usitumie Uaskari wako kucheza na maisha ya Wananchi

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
Salaam zangu na wosia wangu uwafikie maaaskari Afrika ya Mashariki, ni salaam kutoka kwa Human Rights Defendant and Security Advisor Mr. Don Nalimison.

Leo nataka tujifunze maana ya Askari na majukumu yake ili tusiwe tunaogopana na kutishiana maisha. Na wakati mwingine RAIA wasishindwe kuishi kwa amani kisa kumuogopa Askari.

ASKARI tafsiri isiyo rasmi ni MLINZI WA AMANI na USALAMA wa RAIA. Hivyo Askari maana yake ni MLINZI anayelinda raia ili waweze kuishi salama katika nchi yao au katika majukumu yao.

1. ASKARI POLISI anajukumu la kulinda USALAMA wa RAIA na Mali zake na kuhakikisha raia habughuziwi Wala kukwazwa na yeyote na pamoja kutetea Haki zote za raia anayeonewa, kulinda kanuni zote za Uendeshaji JESHI la POLISI (General Standing Order).

Lakini Mapolisi wa leo hawajui wajibu wao Bali wamekuwa wakitumia UASKARI wao kutisha raia na kuwabambika kesi raia na hata kuwatapeli raia kwa mgongo wa UASKARI POLISI. Badala ya kulinda raia wao wanatisha raia na kuingilia maisha binafsi ya ndani ya raia, kitu ambacho nikuwanyima raia Haki zao na Uhuru wao wa kuishi.

2. ASKARI MAGEREZA anajukumu la kulinda Mfungwa ambaye ni raia aliyevunja Sheria za nchi na sio kumpiga au kumuua au kumtweza.Kuhakikisha Mfungwa anaishi kwa Amani gerezani huku akifundishwa tabia njema ili akitoka aweze kuishi na jamii vizuri au asirudie kufanya makosa. Pia Askari Magereza anawajibu wa kufuata kanuni zote za Uendeshaji wa JESHI la Magereza (Prison Standing Order) ili kuhakikisha hakuna raia ambaye ni Mfungwa ananyanyaswa gerezani.

Lakini Maaskari Magereza wa leo kwanza wao wanafikiri kumpiga Mfungwa ndio njia ya kuheshimika na kuogopwa, kumbe ndio njia ya kudharaulika kabisa maana hakuna Mfungwa atakayekuheshimu kwa kumfanyia unyama gerezani kwa maana umekiuka maadili ya UASKARI badala ya kulinda wewe unafanya unyama. Mfungwa amehukumiwa na Mahakama kutumikia kifungo Cha miaka kadhaa lakini anafika gerezani anapigwa mpaka anakufa.

Je, Hilo ndio agizo la mahakama kupiga mpaka mnaua? Je huyo Mfungwa amehukumiwa kunyongwa au? Mahakama ndio inayotoa adhabu za viboko vya kuchapwa Mfungwa lakini Maaaskari wanawachapa viboko wafungwa gerezani bila idhini ya mahakama zilizo wafungwa.

Utekelezaji wa kazi za Magereza ni kuwafunda wafungwa kuwa watu wema na mnapowapiga na kuwatishatisha Sana mnawapa ujasiri na kuwakomaza sana na mwisho wa siku Kama ni jambazi Basi litaendelea na ujambazi wake maana limekomaa na kuwa na sugu za virungu na hata likipigwa na WANANCHI haliumii maana limezoea kipigo.

Askari lazima utambue kuwa sio wafungwa wote Wana makosa ya wizi na wengine ni wafungwa ambao jamii zinawategemea lakini kwa bahati mbaya wamekutwa na hatia. Askari Magereza unatakiwa kuwaelimisha wafungwa jinsi ya kubadilika nasio kukung'uta mafimbo mgongoni na kuwapiga mavirungu kumbukeni wafungwa ni Raia waliopo gerezani kwa mjibu washeria na kulindwa na sio kudhalilishwa na kunyanyashwa.

Wafungwa sio Watumwa mpaka muwafanyie unyama, wafungwa wapo chini ya sheria. Tumekwisha pata Uhuru nchi zote za Kiafrika. Mfungwa akimaliza kifungo amekwisha toka mikononi mwa Askari Magereza na hana mamlaka tena ya kufatilia maisha binafsi ya Mfungwa huyo. Lakini jamii inashangaa kwanini Maaaskari wañaendelea kufatilia maisha ya RAIA ambaye Sasa sio Mfungwa Tena, je wanataka Nini zaidi au ni wivu na woga kwa kuwa walimfanyia unyama gerezani? Raia akitoka gerezani ataishi anavyotàka kwa kumjibu wa Katiba ya Nchi yake. Lazima Askari ajue wajibu wake kwa JESHI la Magereza na kwa Wafungwa na Mahabusu pia.

3. ASKARI JESHI, hawa ni walinzi wa kuu wa Amani ya Nchi na Mipaka ya Nchi na hawa ndio hupewa hadhi ya Uzalendo kwa Taifa maana ndio wanoipigania nchi hata kwa Vita, ndio wanaojitoa mhanga kupigania uhai wa raia wao. Ndio wanao hakikisha POLISI na Magereza hawafanyi unyama kwa raia.

Hawa ndio huingilia Kati pale majeshi madogo madogo yanaposhindwa kutimiza wajibu wao. Lakini wapo wanajeshi ambao wanatumia uanajeshi kuharibu maisha ya WANANCHI kwa kutumia nguvu ya kijeshi.

Mfano raia anawekwa vizuizini kwa Jambo la kijinga kabisa, badala ya kufungua mashitaka wao wanamuweka vizuizini kinyume na Haki za Binadamu zinavyotaka. Haya mazoea ni mabaya Sana na inamfanya raia kuishi maisha magumu Sana.

Kazi ya JESHI ni kusimamia Katiba ya Nchi ilindwe na Raia wote na majeshi yote na Wala isipuuzwee.

4. ASKARI WA UHAMIAJI yeye nikutambua kuwa raia anapata Haki yake ya uraia bila kubuguziwa lakini JESHI hili ndilo linaloongoza kupotoshea Raia na kuwanyima Haki ya uraia wakiwa ndani ya Nchi yao.

Lazima JESHI litazame kuwaokoa raia wake maana raia wa kigeni wanaweza kutumia uzaifu huo kuingia nchini na kupata Haki ya kiraia kuliko Raia halisi.

5. ASKARI MGAMBO na MAJESHI MENGINE ndio wasaidizi wa kazi za majeshi makuu lakini wengi wao hawajui kabisa majukumu yao wao ni kupigapiga na kubambika kesi WANANCHI maana wengine hawana mishahara. Kwa shughuli zao ni pevu ya uonevu kwa WANANCHI.

6. RAIA au MWANANCHI huyu sio Askari, yeye anaishi maisha ya kiraia kwa kufuata maagizo ya Katiba ya Nchi nasio maagizo ya majeshi. Raia hawezi kuishi maisha ya kijeshi Bali yeye anaishi maisha ya kizalendo akiwa Raia huru Tena bila kuingilia maisha yake binafsi na majukumu yàke.

Lakini nashangaa majeshi ya Kiafrika yamekuwa na tabia ya kuingilia maisha ya raia na kuvuruga hata biashara za maisha ya raia.

7. USALAMA WA TAIFA,hili si JESHI Bali ni JESHI kivuli la kuchunguza Kama Haki zinatendeka na kutetea Haki za watu ili wazipate pale wanapobaini mnyonge kaonewa. Kazi kubwa ya USALAMA ni kuchunguza Mambo kwa undani na kuyafanyia kazi kwa masilahi ya Taifa na mtu mmoja mmoja.

Leo hii watu wanaogopa kufika ofisi za USALAMA kupeleka matatizo yao maana wanaamini ukipelekwa ofisi za USALAMA Kuna mateso makali Sana. Lazima tukubali kubadilika ili tuiokoe jamii na jamii iwe tayari kufanya kazi na majeshi kwa Amani.

Sina mengi Sana Mimi DON NALIMISON ila nashauri msomaji wangu wa Makala hii utanifikishia ujumbe wangu sehemu husika.

DON NALIMISON
O'CLOCK MUSIC PRESS.
10 JULAI 2020.
IMG_1594321357304.jpg
 
Ameandika tu kisiasa, ktk dunia hii jeshi la nchi haliwezi kuingilia wajibu wa jeshi/huduma ya polisi.
Mkuu nahisi kama wewe ndo umeelewa kisiasa hata hapa ishawai tokea kipindi cha JK kariakoo pale
 
Askari Magereza wanaua sana wafungwa kwa vipigo, na hii haitangazwi popote. Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom