Ujumbe kwa wanandoa na wachumba

salaniatz

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,678
2,000
"USIMVUE NGUO MUME WAKO"
Wakati anafungua zawadi kutoka kwa watu mbalimbali Jane alishika Box kubwa na kuanza kulifungua kwa pupa kwani alikuwa akikumbuka kuwa alipewa na Mama yake siku ya harusi yake na alitaka kujua ni kitu gani Mama yake mpendwa alimpa, Box lilikuwa jepesi sana na alipolifungua alikutana na kikaratasi kidogo kumeandikwa *USIMVUE NGUO MUME WAKO* hakukuwa na maneno mengine.

Alishangaa sana kwani alishaolewa na suala la kumvua nguo mumewe alishafanya katika honeymoon. Siku iliyofuata alienda Kumuona Mama yake na kumuuliza alimaanisha nini? Hapo ndipo Mama yake alianza kumfafanulia kwa kumuambia kuwa "Moja ya kazi kubwa katika ndoa ni *kuficha mapungufu ya mume wako*huo ndiyo msingi wa ndoa na ndiyo kazi yako kama msaidizi wake.

Hakuna mwanadmu aliyekamilika, mwenza wako atakuwa na mapungufu mengi ya kimaumbile na kitabia, jaribu sana kumfichia mapungufu yake. Unapowaambia marafiki zako kuhusu mapungufu ya Mume wako unakuwa unamvua nguo na kumuondolea heshima yake mbele yao. Lakini mlolongo hautaishia hapo kama wewe ulivyoshindwa kuvumilia na kuwaambia kuwa mume wako anatabia kadha wakadha, maumbile yake yako hivi na vile ndivyo nao watashindwa kuvumilia.

Watawaambia marafiki zao wengine, watawambia wanaume zao na wanaume zao wataongea, yatasambaa mtaani na kuingia mpaka ofisini. Kila anapopita watu watamuangalia kwa mapungufu yake na hata akifanya kitu kizuri watu watakipima kwa mapungufu yake na kumdharau".

Anna kwa wasiwasi alimuuliza mama yake "Sasa nitafanyaje kama nikishindwa kuvumilia mapungufu yake?' Mama yake alimjibu "Kama ni mapungufu ya kitabia ongea naye na msaidie kubadilika, kama ni mapungufu ya kimapenzi basi msaidie kubadilika pia ila kama ni mapungufu ya kimaumbile *jifunze namna ya kukaa naye*, usimpe presha kwa kitu ambacho hawezi kukibadilisha, hajajiumba yeye hata wew una kasoro ambazo atalazimika kuzivumilia na hata hao unaowaambia wenza wao wanakasoro pia lakini hawatangazi!

Akamaliza kwa kumuuliza "Hivi kama mume wako ana Mikono midogo ukimuambia shoga yako ndiyo mikono yake itakuwa mikubwa?" Jane akajibu *Hapana*. Mama yake akaendelea "Basi huna haja ya kumtangazia na kuongelea udogo wa mikono yake, mpakulie chakula na mikono hiyo hiyo midogo aliyonayo na mfundishe namna ya kufinya tonge na mikonon kwa hiyo midogo"

Mama akamaliza na Jane akarejea nyumbani kufurahia ndoa yake. Acha kuwa balozi wa mabaya ya mwenza wako. Kama post hii imekubariki usisahau kushare ili iwabariki na wengine.

C & P
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom