Ujumbe kwa Salim Bakhresa na Azam Tv

drilling

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
4,664
4,764
Ndugu yangu mzee wangu Salim Bakresa nakuomba na uzingatie kuwa Azam Tv watu wengi wanaangalia sasa kama mtu bando lake limeiisha kuna channel zina julikana ambazo zipo free kama cloud itv ch ten TBC na EATV zilizobaki zotee unazikata kama huna bando, sasa nakuomba kama mtu kaishiwa bando ungekuwa unaawaachia channel za dini waone bure.

Maana wakiona chanel za dini wapo watakao ongoka wakawa wema na wewe mzee bakhresa mungu anakulipa kwa kila mtu atakae angalia channel za dini sio tu kutuachia clouds na nyinginezo masaa yote tunaangalia bongo fleva na wasichana kucheza uchi .

Waachie na wenye imani zao wawe wanapata mafundisho bure bila kulipia ili na wewe upate baraka za mungu.
 
mkuu unajua washika dini ndio wenye hela,, maana hawanywi pombe wala hawazini wala hawapekeki kwa waganga,, hela zao ni za sadaka tu,, acha walipie kupata mahubiri
 
Kwenye dini ndo mnafundishwa kupenda vya bure? ,lipia mkuu. Akikuonesha bure unataka afirisike..
 
Kwa hiyo kodi halipi, je halipi wafanyakazi ambao nao wana dini? Kwanza yeye ni mfanyabiashara akileta habari za huruma inakula kwake
 
Wewe Lipa haya mambo ya kumtisha Salim Bakhresa hayana Mashiko, Kumbuka hiyo ni Dini yako haitamfaidisha Chochote!
 
Ndugu yangu mzee wangu Salim Bakresa nakuomba na uzingatie kuwa Azam Tv watu wengi wanaangalia sasa kama mtu bando lake limeiisha kuna channel zina julikana ambazo zipo free kama cloud itv ch ten TBC na EATV zilizobaki zotee unazikata kama huna bando, sasa nakuomba kama mtu kaishiwa bando ungekuwa unaawaachia channel za dini waone bure.

Maana wakiona chanel za dini wapo watakao ongoka wakawa wema na wewe mzee bakhresa mungu anakulipa kwa kila mtu atakae angalia channel za dini sio tu kutuachia clouds na nyinginezo masaa yote tunaangalia bongo fleva na wasichana kucheza uchi .

Waachie na wenye imani zao wawe wanapata mafundisho bure bila kulipia ili na wewe upate baraka za mungu.
Unata neno la mungu bure ktk tv alafu bure uliona neno la mungu litangazwa bure lipia neno likuakae vizuri.ungeambiwa mchango wa harusi nk ungelipa
 
Back
Top Bottom