Ujumbe kwa RPC wa Geita - Hata Zombe alikuwa RPC kama wewe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,650
218,105
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Geita , Mtukufu Mponjoli Mwabulambo amenukuliwa na gazeti la Nipashe " AKIONGEA KWA MAJIVUNO " kwamba Jeshi hilo halina taarifa za kutofikishwa mahakamani kwa viongozi 51 wa CHADEMA , Chato .

Ikiwa kama jeshi lake ndio limewakamata watu hawa inakuwaje hazijui taarifa zao ? Ikumbukwe kwamba viongozi hawa wa Chadema wamekwisha achiwa kwa dhamana na Mahakama , lakini kwa ubabe wa kishamba jeshi hilo limeendelea kuwashikilia kinyume kabisa na katiba ya nchi.

Natumia nafasi hii kumkumbusha ndugu yangu Mwabulambo kwamba Abdallah Zombe , aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa kanda maalum ya DSM , Kabla ya mwisho wake mwema aliteuliwa kuwa RPC .

Cheo ni dhamana tu .
 
Tatizo la hawa watu hufikiri hiki cheo ni cha milele, wanatakiwa kusoma alama za nyakati. viburi kama hivi viliangamiza wengi. Aelewe kuwa Mungu hawezi kumwacha kudhalilisha, kuonea na kukandamiza wengine milele. Kumbuka ukiwa hivyo nawe siku yako ipo na malipo huanza hapa hapa duniani.
 
Back
Top Bottom