Mh; Waziri kuna tabia inayoendelea nchini katika sekta ya elimu na kama hamjaijua ngoja nikupashe habari kamili. Inahusu vyeti toka nje ya nchi.
Mh. Waziri msiishie kuangalia wafanyakazi hewa tu na wenye vyeti feki au elimu feki kwa waliosomea Tanzania au wenye vyeti toka Tanzania, angazeni vyeti feki toka nje ya nchi pia, Hao ndio wengi kwenye shule, vyuo, taasisi binafsi na hata katika mfumo wa ajira wamejaa na vyeti vyao walivyotoa nchi zingine.
-Kuna watu wamekuja na mbinu za kununua vyeti nchi mbalimbali na kuja kutumia Tanzania kuanzia elimu ya sekondari hadi vyuoni. Vyeti hivi wakishanunua wanakuja Tanzania wanaandaliwa vyeti vya kuzaliwa vyenye majina sawa na majina yaliyopo kwenye hivyo vyeti halafu wanaomba nafasi ya kusoma hasa kwenye shule au vyuo binafsi. Kuna baadhi ya vyeti hivyo huwa ni feki kabisa lakini vinatumika hapa nchini kwasababu hatuna vifaa maalum ya kukagulia vyeti hvyo na hatuna wataalam wanaojua uhalali wa hivyo vyeti.
-Vyeti mara nyingi vinanunuliwa Kenya, Uganda, Afrika Kusini nk na vikishafika Tanzania vinatumika shule na vyuo binafsi ili mwanafunzi aweze kuingizwa katika mfumo mzima wa elimu. Mfano cheti cha Kenya-kidato cha nne hutumika Tanzania kujiunga na kidato cha Tano kwenye shule binafsi au vyuo vingine. Wengine wameenda mbali, imefikia hatua watu wanaotokea nchi zingine wanaingia kwa mfumo wa ajira ndani ya nchi yetu kwa kupitia vyeti hivyo ambavyo vingine sio halali na havina uthibitisho. Mfano wakenya wengi kwa sasa wamejaa Tz wanajidai wanafundisha shule za binafsi kuanzia chekechea hadi sekondari lakini ni wachache wenye vyeti halali. Wengi wana vyeti feki na kinachowabeba ni lugha.
-Kuna hadi mawakala wanaouza vyeti hivi ukitaka wanakuletea kwa kiasi cha pesa utakachokubaliana nao.Fanyeni uchunguzi kuhusu hili mtabaini.
-Kuna umuhimu wa kukagua wenye vyeti toka nchi mbalimbali. Vikikaguliwa asilimia 98 ni feki au hata kama ni orijino basi utakuta sio ya mwenye nayo pale ambapo utakapofatilia elimu ya msingi, historia yake na majina yake halali utakuta sio sahihi.
-Kuna idadi kubwa ya Wanafunzi feki wako shuleni,vyuoni na kwenye mfumo wa ajira wakiwa na vyeti feki toka nchi zingine. Vyeti hivi huwa vinatumika kwa urahisi katika Tanzania kwasababu hakuna anayeviulizia wala kuvikagua ila vinakubalika tu hata kama kimetengezwa stationary hapa Tanzania halafu kikapewa chapa ya elimu ya nchi yoyote ile duniani. #TANZANIA NDIO DAMPO LA VITU FEKI.
WITO: Tusaidiane kumfikishia waziri ikiwezekana Rais ujumbe huu kwa njia ya mitandao mbalimbali. Ukiisoma ichukue isambaze mpaka kwa waziri