Ujumbe kwa Mh. Zitto Kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe kwa Mh. Zitto Kabwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tankthinker, May 20, 2011.

 1. Tankthinker

  Tankthinker Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh. Zitto, napenda kukupongeza sana kwa mchango wako mkubwa kwa Taifa letu. Juhudi yako tunaiona, na ni imani yetu kuwa utaidumisha. Mh. Zitto, Mungu amekujalia kuingia katika duru la siasa hali ukiwa una umri mdogo. Watanzania wengi bado wana imani na wewe kuwa hutawaangusha katika jitihada zako za kushiriki kuleta ukombozi wa Watanzania.

  Ninajua kuwa kazi za siasa zina changamoto nyingi sana, lakini ni ushauri wangu kwako kuwa jitahidi kuzishinda kwa kuepuka vishawishi vya mafisadi wenye nia ya kuchonganisha ili kuuwa umoja katika CDM jambo ambalo nashukuru kuwa hata wewe umelifahamu.

  Jenga uvumilivu katika kukabili utofauti wowote utakaojitokeza wa kiuongozi katika chama. Wewe, na wengine wenye umri kama wako mna nafasi nzuri tu, kutokana na umri wenu kulitumikia Taifa hili kwa muda mrefu sana.

  Usikubali kabisa pressure yeyote ile ukutoe kwenye mstari wa kuwatumikia watanzania kwa moyo wa dhati. Uvumilivu wako, na kujitoa kwako kutazidi kuwa jengea watanzania imani kubwa juu yako.
  Hata kama kuna mapungufu katika CDM, bado ni ukweri usiopingika kuwa ni chama pekee kwa sasa kilicho onesha kwa thati kuwa kinawapigania watanzania ili yamkini waweze kunufaika na Utanzania wao.
  Bado tunaamini kuwa nchi yetu sio masikini, ila tatizo ni uongozi mbaya. tukipata watu kama ninyi ( CDM ) tunajuwa taifa hili litakuwa kweri ni Bustani ya Eden.

  Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni kweli, kama unatarajia kufika mbali kisiasa tafadhali kuwa mvumilivu na busara itumike kwenye maamuzi na kauli za kisiasa
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naungana nawewe mwandishi, Zitto safi sana sasa nchi inahitaji ukombozi na ukombozi si lele mama, si kucheka, si kufurahia hata baya, tumia busara na nafasi songa mbele, kwa taarifa chadema tu ndio mkombozi wa dhati kwa kizazi na nyinyi viongozi ndio dira ya vita hii ngumu maana kushindana na magamba yaliyokomaa si kazi ndogo yataka moyo
   
 4. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Good Advice,
  I am always happy to see this guy on right/his track,
  He is very potential in this country and we shouldn't let any one play around with him,
  or even allow him get astray.
   
Loading...