mdesi
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 1,366
- 2,202
Habari za jioni ndugu na jamaa, Mods naomba huu uzi msiuunganishe na mwingine ili kupata ujumbe usipotee.
Mheshimiwa waziri wa Elimu,kwanza naomba ni kupongeze kwa majukumu uliyonayo, wana nchi tunakuamini sana hasa katika utendaji wako wa kazi, kwa kusimamia majukumu yako bila woga na kwakujiamini. Hili ni jambo la pekee.
Pili napenda kuwapongeza kwa kurudisha heshima ya elimu hasa pale mlipo fanya operation ya kuhakiki vyeti vya waajiliwa wote. Waliogushi vyeti walichukuliwa hatua na wengine kuacha kazi mwenyewe.
Ni takribani wiki mbili, mh. Mmoja ametuhumiwa kutumia vyeti vya mtu mwingine na ni mteule wa wa mh. Mkuu wa nchi. Nimeshangazwa na ukimya wako katika jambo hili licha ya makelele mengi katika mitandao ya kijamii. Kumbuka kuwa anayetuhumiwa ni kiongozi na unajua uhimu wa kuwajibika kama kiongozi. Mbona issues nyingine zikiongelewa mitandaini mnachukua hatua mapema? Rejea walimu walio mpiga mwanafunzi kule Mbeya mlitoa matamko mengi sana na kuwafukuzisha kazi.
Kama utalinyamazia hili swala la vyeti kwa huyu mheshimiwa ni afadhali ukapisha nafasi wakae wengine wanaoweza tenda haki kwa wote na si kuwaonea wanyonge. Vinginevyo halarisheni biashara ya kuziana vyeti na wale waliofukuzwa kazi na kunyimwa stahiki zao warudishwe kazini.
Naomba nikuambie kuwa wanachi tunasubiri tamko la kakanusha au kukiri tena kwa evidence juu ya uhalali wa vyeti vya huyu bwana.
Tunakoelekea utashindwa kufanya majukumu yako kutokana na jipu liliota usoni. Tutegulie mtego huu ili kurudisha imani kwa serikali yetu tukufu. Naomba kuwasilisha.