Ujumbe kwa Mh rais Samia, kuhusu sherehe za kesho za wafanyakazi.

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
4,040
8,895
Usihangaike kuandaa hotuba ndefu kujichosha wewe mwenyewe pamoja na watakaokusikiliza.

Wafanyakazi wanataka kusikia mambo manne tu:

1. Nyongeza ya mishahara yao ambayo ilisitishwa tangu 2015 pamoja na arrears zote kuanzia January 2016 hadi April 2021.
Increments zipo kisheria mishahara ipande kuanzia pale ilipoishia (Jan 2016) sio July 2021.

2. Hali ya kifedha ya mifuko ya NSSF na PSSSF baada ya fedha nyingi kama sio zote kuchotwa na serikali.

3. Upandaji wa vyeo na madaraja. Hali hii imesababisha watu kustaafu na vyeo na madaraja ya chini hivyo kupata pension pungufu. Mfano wengi waliostaafu 2016-2020 wamepunjwa mafao yao kwani mishahara hawakupandishiwa na madaraja hawakupandishwa.

4. Kuhusu uhamisho wa wafanyakazi. Weka sawa hili jambo. Utaratibu wa kuhama ukoje? Kwani kila mtu anafanya lake wakati serikali ni moja.
 
Na huyo Jenister Mhagama ndio lopolopo kweli. Ameanza kuwadanganya wafanyakazi tangu 2016. Hivi hana mshiba wa aibu? Kila mwaka hadithi ni zile zile.
 
Usihangaike kuandaa hotuba ndefu kujichosha wewe mwenyewe pamoja na watakaokusikiliza.

Wafanyakazi wanataka kusikia mambo manne tu:

1. Nyongeza ya mishahara yao ambayo ilisitishwa tangu 2015 pamoja na arrears zote kuanzia January 2016 hadi April 2021.
Increments zipo kisheria mishahara ipande kuanzia pale ilipoishia (Jan 2016) sio July 2021.

2. Hali ya kifedha ya mifuko ya NSSF na PSSSF baada ya fedha nyingi kama sio zote kuchotwa na serikali.

3. Upandaji wa vyeo na madaraja. Hali hii imesababisha watu kustaafu na vyeo na madaraja ya chini hivyo kupata pension pungufu. Mfano wengi waliostaafu 2016-2020 wamepunjwa mafao yao kwani mishahara hawakupandishiwa na madaraja hawakupandishwa.

4. Kuhusu uhamisho wa wafanyakazi. Weka sawa hili jambo. Utaratibu wa kuhama ukoje? Kwani kila mtu anafanya lake wakati serikali ni moja.
Pwaa pwaaa pwaa (makofi)...

Ni kweli. Hizi ndizo hoja za kuongea kesho...

Nje ya hapo, naye ajiandae kuchukiwa na kutoungwa mkono kqbisa na wafanyakazi wenzake kina sisi...!!
 
Kweli mkuu. Pia nimesahau pension za wastaafu. Kuna watu wamestaafu tangu 2018 hadi leo hawajalipwa hata mia.
 
Mama yupo makini sana na hili ukilinganisha na mkuu wa malaika ambaye hakujali hali ya watu wengine....
 
Ngoja tuone kesho. Watu hawataki hotuba ndefu wanataka wajue anapandisha au hapandishi mishahara.
 
Tulisema humu Magufuli amekomba hela za Wafanya kazi wote wa Serikali na private sector kwenye mifuko ameenda kununua ndege zake ambazo hazina faida.
Tulishambuliwa vibaya sana,lakini Samia juzi kasema lakini Hamna aliye mshambuliwa.

Miradi ipo,na kitu endelevu vizazi na vizazi kiongozi anapaswa kujali maisha ya watu wapate kuishi miaka mingi wakiwa na furaha na amani.
 
Inauma sana mkuu
 
Halafu huyo Waziri mimi hata simuelewagi
Alikuwa mwalimu wa Primary akajiunga CCM, Sasa hivi eti ni waziri.

Kazi yake Bungeni ni kupinga tu kila wanachosema wabunge kuhusu maslahi ya wafanyakazi. Utasikia "taarifa muheshimiwa spika"
Jenister ni janga....
 
Back
Top Bottom