Napenda kuwaeleza kuhusu kasoro za bili tunazoletewa na Mamlaka ya MWAUWASA (MWANZA), Mamlaka inao wasomaji wa mita na wanatakiwa wapite majumbani, sehemu za biashara n.k. Hawa wasomaji wa mita wanaposoma mita hawamshirikishi mwenye nyumba kwa mfano usomaji wa mwezi uliopita ni units kadhaa na usomaji wa mwezi huu ni units kadhaa ili hesabu ifanyike na ijulikane units zilizotumika lakini kwa ujeuri wao wanasoma mita peke yao, kufanya hesabu peke yao bila kumshirikisha mwenye nyumba au mwenye nyumba ya biashara. Leo nimemkuta msoma mita kwangu na kufanya naye mahesabu na kugundua kuwa kuna tofauti ya Tshs.60,000 ya hesabu ya mwezi uliopita. Mimi nawashauri kuwa kuanzia sasa kila msoma mita LAZIMA amshirikishe mwenye nyumba au yeyote atakayemkuta kwa kufanya naye mahesabu na kumuelewesha na siyo kusoma mita peke yake na kufanya mahesabu peke yake vinginevyo tusije tukafika pabaya na hawa wasoma mita wenu.