Ujumbe kwa Anna Kilango Malecela na Matayo David Mathayo

Ujumbe kwa Anna Kilango Malecela na Matayo David Mathayo

Kilahiro

Senior Member
Joined
Aug 5, 2013
Posts
171
Reaction score
46
Wabunge wetu wapendwa wa serekali sikivu ya ccm sisi wananch wa Same tunaomba kaulizenu bungeni tuzikie kuhusu barabara yetu ya mkomazi-kihuri -gonja -kisiwani same.Barara hii ndo mbovu kupita zote mkoa wa Kilimanjaro tena ndo barabara mbovu kupita zote kanda ya kaskazini inayo peleka mbuga ya wanyama mkomazi.pamoja na kuwa mkomazi national park ndo mbuga ya 2 ilioko karibu na mji(TOWN/CITY) hapa Tazania ukitoa Arusha national park barabara hii ni mbovu kupita maelezo.Kwa zaidi ya miaka 10 wabunge wetu mpo bungeni ila hatusikii lolote kutoka kwenu.mbo na Rombo,HAI, Barabara zinajenga kwa kasi kubwa?why!nyie?tumechoka na viraka mnavyo tuwekea tunaomba tusikie sautizenu bungeni.nimimi mkulima wa tangawizi kihurio-Same.PAMOJA NA SEREKALI YETU NI SIKIVU ILA....!(kilonzo kiraghenja!)
 
Watakusikia kwani wote ni viongozi wasikivu sana
 
Watakusikia kwani wote ni viongozi wasikivu sana

Kwakuwa ni ccm ni wasikivu,walikuwa wapi siku zote,wewe bi mchumia tumbo nini?maana kila la ccm liwe baya,zuri au la kifisadi ilimradi linahusu ccm utashabikia na kusifia,ama kweli wewe ni mfu kwenye brain!
 
mathayo msikivu sana ha ha ha. .akichinja mbuzi c mnasaha matatizo. . . .nlisoma huko wanafunzi tukawa upande wa mgombea wa cdm kidogo tufukuzwe shule.
 
nyinyi same ndio mnao tia aibu mkoa wa kilimanjaro na kanda ya kaskazin kwa kukumbatia hawa wezi
 
Nyie ngojeni. Tumalize barabara za Mikoa, kisha za wilaya, halafu ndio hizo zenu za vijiji. Mnaharaka ya nini?
 
Nyie ngojeni. Tumalize barabara za Mikoa, kisha za wilaya, halafu ndio hizo zenu za vijiji. Mnaharaka ya nini?

Ha ha ha ha mama umenichekesha sana uliivyomshushua mleta mada ha ha ha .
 
FF ana haki na uhuru wa kuwasilisha yale anayoona wabunge hao wanapaswa kuyasema bungeni kwa kuwa ni mahitaji yao na zilikuwa ni ahadi za wabunge hao
 
Wabunge wetu wapendwa wa serekali sikivu ya ccm sisi wananch wa Same tunaomba kaulizenu bungeni tuzikie kuhusu barabara yetu ya mkomazi-kihuri -gonja -kisiwani same.Barara hii ndo mbovu kupita zote mkoa wa Kilimanjaro tena ndo barabara mbovu kupita zote kanda ya kaskazini inayo peleka mbuga ya wanyama mkomazi.pamoja na kuwa mkomazi national park ndo mbuga ya 2 ilioko karibu na mji(TOWN/CITY) hapa Tazania ukitoa Arusha national park barabara hii ni mbovu kupita maelezo.Kwa zaidi ya miaka 10 wabunge wetu mpo bungeni ila hatusikii lolote kutoka kwenu.mbo na Rombo,HAI, Barabara zinajenga kwa kasi kubwa?why!nyie?tumechoka na viraka mnavyo tuwekea tunaomba tusikie sautizenu bungeni.nimimi mkulima wa tangawizi kihurio-Same.PAMOJA NA SEREKALI YETU NI SIKIVU ILA....!(kilonzo kiraghenja!)

Shigha du avaae, ...thi thi em thio yetu tena!
 
Kilahiro,

kuna tatizo lingine kubwa zaidi ya hilo la barabara, nalo ni kuanguka kwa ELIMU katika wilaya ya Same. Kwa muda mrefu wilaya ya Same imekuwa ikishika mkia katika matokeo ya mitihani ya kitaifa kwa mkoa wa Kilimanjaro. Katika shule 10 zenye matokeo mabaya ya mitihani katika mkoa wa Kilimanjaro 7 ziko katika wilaya ya Same. Hii ni FEDHEHA kubwa sana kwa wenyeji wa wilaya SAME na suala ambalo linatakiwa kushughulikiwa sasa hivi.

cc Not_Yet_Uhuru, FaizaFoxy, Mkwawa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom