Ujue ukweli wa Lowassa kukimbia midahalo

Ujue ukweli wa Lowassa kukimbia midahalo

Mariswaga

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2015
Posts
201
Reaction score
2
Vyama vyote vya siasa vimekubali kufanya mdahalo wa wagombea wa Urais kwenye vyombo vya habari lakini vyama vinavyounda UKAWA vimekataa kushiriki kwenye midahalo hiyo kwa kutoa sharti moja la kutomshirikisha mgombea wao na badala yake waende wenyeviti wa vyama.

Utaratibu wa dunia nzima kwenye midahalo wanahudhuria wagombea na siyo wenye viti wa vyama... Yaani Rais Kikwete aache majukumu yake ikulu halafu aende kwenye vyombo vya habari kufanya midahalo wakati kwenye midahalo wanazungumzia sera za chama husika na sasa aliyebeba sera za CCM ni Ndugu Magufuli.

Baada ya kufanya uchunguzi sababu zifuatazo zimebainika kuwa ndiyo vigezo vya kumfanya mgombea wa UKAWA ndugu Lowassa kususia midahalo hiyo
1. Afya yake ni dhaifu na haimruhusu kukaa muda mrefu bila kupewa dawa ya kumuongezea nguvu. kwenye mikutano yake ya kampeni hajawahi kuzungumza zaidi ya dakika 15, sasa atawezaje kuhudhuria mdahalo akaongea zaidi ya nusu saa?

2. Amehusika sana kwenye kashfa nyingi za ubadhilifu wa mali za umma na hana uwezo wa kukataa ukweli huo, hata alipoulizwa na waandishi wa habari huko Dodoma alikataa kulijibu hilo swali, na endapo atahudhuria kwenye mdahalo wowote hilo swali hawezi kuliepuka

3. Chama chake hakina sera nzuri, anakosa kitu cha kuongea awapo mbele ya watu kwakua chama chake hakijaandaa ilani nzuri yenye sera za kumkomboa Mtanzania. Wakati wenzake wanatoa sera za kupunguza gharama za ujenzi yeye anamwaga sera za kuwatoa jela akina Babu Seya na kubomoa nyumba za nyasi nchi nzima kwa muda wa siku 100
 
UKAWA wanafanya mambo kwa mahesabu. yaani wanachofanya ni kumchanganya adui. wanapo kuwa karibu na adui wanajifanya wapo mbali nae na wanapo kuwa mbali na adui ndio hapo wanakuwa jirani nae mwisho wa siku wanamaliza mchezo. si ulio kwenye tarehe za uzinduzi wa kampeni kama zili karibiana kumbe UKAWA wanawatanguliza.

MUNGU ibariki UKAWA
 
Wenye dalili za kushindwa ndio hung'angania midahalo kama suluhisho lao la mwisho.Mwaka 2010 CCM hawakuona haja ya midahalo,kwa sababu waliona watashinda.Mwaka huu wanaitamani kwa sababu dalili zinaonesha Ukawa watashinda.Ukawa nao wanaringa mwaka huu,kutesa kwa zamu.Hata hivyo Mbatia amewakaribisha.Jitokezeni
 
Babu ananaogopa kwenda kwenye midahalo maana yupo busy na madini makunwa makubwa ambyo atawapa wakubwa..Ivi edo akienda kwenye mdahalo si anaweza kulia, sasa uanazani ataongea nini? atawaambia watu kua atamaliza nyumba zza nyasi ndani ya siku 100. Huo ni upuuzi kutaka kutufanya sisi watoto. Monduli ulishndwa kumaliza leo za Tanzania utamalizaje? nenda zako kapumzike uwpe ng'ombe zako pumba. Hatutaki ahadi za kwa hadaa wananchi, unasema utafungua bank ya bodaboda, kama ulikua unawajali hizo nyumba ulizonunua LONDON ungewekeza hapa uwaajiri. Wewe kalalilie maini makubwa acha watu wa kufanya kazi wafanye.
 
Basi kama hawataki kutupa babu basi watupe makamanda wao mahiri Sumaye aje atueleze kuhusu nyumba za serikali, Pia aje Masha. ila angekuja babu mwenyewe ingekua poa maana kwenye karatasi ya kura jina lake litakuwepo.
#HapaKaziTu
 
Kweli CCM B nakumbuka enzi hizo CHADEMA ilikuwa inataka midahalo ya wagombea leo kulikoni? FINISHED

umejileta mwenyewe! kwanini jk alimkimbia dokta mihogo?
 
Wenye dalili za kushindwa ndio hung'angania midahalo kama suluhisho lao la mwisho.Mwaka 2010 CCM hawakuona haja ya midahalo,kwa sababu waliona watashinda.Mwaka huu wanaitamani kwa sababu dalili zinaonesha Ukawa watashinda.Ukawa nao wanaringa mwaka huu,kutesa kwa zamu.Hata hivyo Mbatia amewakaribisha.Jitokezeni

agiza kinywaji ntalipa
 
Hapo hakuna kujiamini. Siwezi kuongozwa na viongozi bubu. Kura yangu kwa Magufuli.
 
Tupe pia ukweli wa kikwete na ccm kukataa midahalo na sasa wameibuka kuikubali
 
Watanzania dah mbona tunashindwa ku reason cc wenyewe lowassa ambae alikuwa serikalin kwa miaka 30 kama wazir alishindwa kleta ma badiliko leo hii ana2hadaa nawatu macho yanawatoka ety rais haaaa nan amchague huyo fisad
 
Ingia mdahalo na MABADILIKO kwa sababu wananchi wana chagua mabadiliko sio Lowassa!
 
Watanzania dah mbona tunashindwa ku reason cc wenyewe lowassa ambae alikuwa serikalin kwa miaka 30 kama wazir alishindwa kleta ma badiliko leo hii ana2hadaa nawatu macho yanawatoka ety rais haaaa nan amchague huyo fisad

Hakuna mabadiliko ndani ya ccm usichokielewa nini. Wananchi wanatafuta mabadiliko nje ya CCM ndo maana Lowassa yupo nje ya CCM. Ugumu wa kuelewa hili ni nini! Miaka 54 imewashinda miaka 5 utaweza!?
 
Hakuna mabadiliko ndani ya ccm usichokielewa nini. Wananchi wanatafuta mabadiliko nje ya CCM ndo maana Lowassa yupo nje ya CCM. Ugumu wa kuelewa hili ni nini! Miaka 54 imewashinda miaka 5 utaweza!?

Lowassa hawezi kuongoza mabadiliko because he is part of the problem not the solution
Pili, kwa hali aliyofikia na Parkinson yake hata akili yake sasa si nzima. So poleni sana!
 
Ccm iliwahi lini kushiriki midahalo ya mgombea urais? Ebu tutajie

kama kutoshiriki midahalo ndio sababu ya kukosa sera 2010 ccm haukushiriki je hamkuwa na sera?

Afya ya mtu ipo mikoni mwa Mungu mwanadamu hujui nini kitatokea baada ya dakika moja
achani kumkufuru Mungu wanaccm
 
Back
Top Bottom