Heshima kwenu wakuu!
Leo wakati wa taarifa ya habari ya saa moja ITV habari ya kwanza ilikuwa kuhusu kuwasili nchini kwa wanamuziki wa kikundi cha PSquare. Mimi nilishtuka kidogo, kwa kuwa tumezoea kusikia habari muhimu kitaifa zikipewa kipaumbele wakati wa taarifa za habari.
Sasa ujio wa hawa wasanii una umuhimu gani kitaifa? Kwa wananchi wa kule vijijini ambao hawana hata uhakika wa mlo mmoja kwa siku hii taarifa ina umuhimu gani? Hata kwa wananchi walio nje ya Dar es Salaam ambao hawategemei kuhudhuria tamasha la wanamuziki hao hizi habari zina manufaa gani?
Naomba michango yenu kuhusu hili wadau.