Ujio wa obama: Mashule Dar, kufungwa

Ujio wa obama: Mashule Dar, kufungwa

Bahimba

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
510
Reaction score
346
Wakuu ni imani yangu kuwa mpo salama,

Nimeshusha uzi huu ili tujaribu kuliangali swala hili kiupana zaidi. Katika vitu ambavyo vimeniacha hoi zidi ya ujio wa Obama ni kufunga baadhi ya shule jijini Dar, ukiachilia mbali hatua kadhaa zilizochukuliwa na serilikali yetu katika ziara hii lakini hili la kufunga baadhi ya shule ndo hasa tuliangalie.

Najiuliza hivi hata Rais wangu Kikwete huwa akienda Marekani huwa yanafanyika haya? Na kama hayafanyiki nini basi uzaifu wa maamuzi ya viongozi wetu wa nchi pindi nchi yetu inapotembelewa na viongozi wa mataifa makubwa? Ni dhahiri kuwa Tanzania bado tuna viongozi ambao mitazamo yao na fikra zao ni hasi, nakumbuka katika utawala rais wa awamu ya pili nchini mwetu, mambo kama haya yalikua yanafanyika pindi rais alipotembelea sehem flani, ilitulazim wanafunzi kutoka madarasani na kujipanga barabarani na kupungia mkono kwa msafara wa Rais hata kama hata simama na tena msafara wenyewe ulikua ukipita kwa speed kubwa.

Awamu ya tatu ilifika Rais wa awamu hiyo alipiga marufuku utaratibu huo na alisema waachwe watoto wasome, leo mambo haya yanajirudia tena kwa viongozi wa nje, najiuliza ni nini azima ya mambo haya kwa serikali yetu? Napata wasiwasi mkubwa jinsi serikali yetu inavotukuza ujio wa Rais Obama. Kuna nini nyuma ya pazia? Mbona marais wengi hua wanakuja na mambo haya hua hatuyaoni, ni hivi karibuni tu Rais wa China alikuja nchini mbona hatukuona mambo haya, karibuni wana JF tulidadavue hili. WANAWASILISHA.
 
We need to change seriously "wake up Tanzania wake up "
 
Janga la Taifa TZ ,heshima aliyoicha Mwl Nyerere imepotea,sasa shule zifungwe what for?wamekufa watu Arusha na bomb la mwinguru mbna hata bunge halikufungwa?Kweli nmeamini ccm akili ndogo wanahisi wanaona KAKAKUONA leo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
leo nimewahi ofisini leo 12 kukwepa usumbufu wa Obama nimefika machinga nikakuta ajali mbaya ya fuso imepasuliwa kwa mbele inawezekana ni treni iliyofanya kazi hiyo na barabara imefungwa inatumika upande mmoja, nikafika temeke ccm nikaona wanachama wa ccm hasa wamama wanagawana tshit,vitenge na kofia kuwahi kwenda kumpokea obama barabarani.
 
Shule zılıshafungwa kıtambo tuzungumzıe kazı maofısını leo zıtafanyıka? Nashaurı tarehe ya leo ıtangazwe rasmı kuwa Obama Day na ıwe publıc holıday
 
Shule zılıshafungwa kıtambo tuzungumzıe kazı maofısını leo zıtafanyıka? Nashaurı tarehe ya leo ıtangazwe rasmı kuwa Obama Day na ıwe publıc holıday

mambo ya mzee ruksa! Alikuwa halazii damu viji issu kama hivi, unapigwa pumziko hadi unahisi unaiibia selikari
 
Sio kila jambo unalaumu au unapingga. Leo usafiri utakuwa shida, kuna uwezekano kwamba watu wengi Leo watakuwa barabarani kuona ujio huo. Hali ilivyo yaweza kuwa shida kwa watoto hasa wanaosoma mjini au wanaosoma mbali na makazi yao na wanategemea usafiri wa daladala. Binafsi, naona sawa tu, ni usalama kwa watoto wetu, lkn ni kwa Dar tu.
 
Sio kwamba wanafunzi wako likizo tayari?! Mashule gani yanayofungwa mwezi huu?!
 
Wanafunzi WaPo likizo wewe , kipindi cha sabasaba ni kawaida ... Acha kupotosha umah
 
Wakuu ni imani yangu kuwa mpo salama,

Nimeshusha uzi huu ili tujaribu kuliangali swala hili kiupana zaidi. Katika vitu ambavyo vimeniacha hoi zidi ya ujio wa Obama ni kufunga baadhi ya shule jijini Dar, ukiachilia mbali hatua kadhaa zilizochukuliwa na serilikali yetu katika ziara hii lakini hili la kufunga baadhi ya shule ndo hasa tuliangalie.

Najiuliza hivi hata Rais wangu Kikwete huwa akienda Marekani huwa yanafanyika haya? Na kama hayafanyiki nini basi uzaifu wa maamuzi ya viongozi wetu wa nchi pindi nchi yetu inapotembelewa na viongozi wa mataifa makubwa? Ni dhahiri kuwa Tanzania bado tuna viongozi ambao mitazamo yao na fikra zao ni hasi, nakumbuka katika utawala rais wa awamu ya pili nchini mwetu, mambo kama haya yalikua yanafanyika pindi rais alipotembelea sehem flani, ilitulazim wanafunzi kutoka madarasani na kujipanga barabarani na kupungia mkono kwa msafara wa Rais hata kama hata simama na tena msafara wenyewe ulikua ukipita kwa speed kubwa.

Awamu ya tatu ilifika Rais wa awamu hiyo alipiga marufuku utaratibu huo na alisema waachwe watoto wasome, leo mambo haya yanajirudia tena kwa viongozi wa nje, najiuliza ni nini azima ya mambo haya kwa serikali yetu? Napata wasiwasi mkubwa jinsi serikali yetu inavotukuza ujio wa Rais Obama. Kuna nini nyuma ya pazia? Mbona marais wengi hua wanakuja na mambo haya hua hatuyaoni, ni hivi karibuni tu Rais wa China alikuja nchini mbona hatukuona mambo haya, karibuni wana JF tulidadavue hili. WANAWASILISHA.

Shule gani zimefungwa mkuu? Dah hii itakuwa imevuka mipaka sasa..
 
wewe mkuu uongo unaona sifa,shule mbona zimefungwa siku nyingi.
 
Hizi habari zingine ni za kuongeza chumvi....ni shule gani ambazo hadi leo hazijafungwa kwa likizo ya kati ya mwaka? For what i know, shule zinazofuata mtaala wetu zimefungwa zamani....mwanzoni mwa June na kama zipo shule ambazo hazijafungwa ni zile shule zao; ambazo wafunge wasifunge kimpango wao! Sana sana labda useme kwamba shule zinapofungwa, baadhi ya madarasa, kv Darasa la IV, VII, Form II, IV huwa hawafungi kwa ajili ya kujiandaa na mitihani! Lakini kwa kawaida tangu miaka ya nyuma, hata pale madarasa haya yanapokuwa yanaendelea kwenda shule; mara nyingi kama sio zote, huwa wanapumzika wiki ya mwisho....yaani hii wiki ya kuelekea Saba saba! If so, I doubt ukweli wa taarifa hii!
 
ujio wa obama umekuwa kero, bora wangekutania visiwani sio tanzania
 
Nyie mnaongea msilolijua. Obama sio sawa na marais wengine. Ulinzi wake ni mkali kwa sababu ya wingi wa maadui anaojitengenezaea Marekani kupitia foreign policy yake. Msongamano wowote usioeleweka, kizuizi chochote kwenye msafara wake kinaweza kutafsiriwa kama njama dhidi yake. Kwa taarifa yako alipokuwa Ujerumani wale waishio maghorofani mjini walipewa amri ya kutofungua madirisha wakihofia snippers. In short unaweza kumpiga picha hata CIA ikiwa tu kumpiga kwako picha hakuwezi kwa namna yoyoye kumzuia kutimiza majukumu yake.

Pangu Pakavu.
 
ninaamini Obama mwernyew akijua kuwa watoto hataenda shule eti kisa amekuja atasikitika sana, so so sad to live in Tanzania, hiki kipindi cha mpito kimekuwa kirefu mno
 
Mkuu shule mbona zishafungwa kwa likizo ya nusu muhula au unazungumzia tuation centers
 
Back
Top Bottom