Jamaa ana style yake ya kusema neno moja hata mara nne katika misemo mingine:~
1."Goto limekata,mapene yamecheua",goto na mapene ni kitu kimoja-pesa
2.Anabonga ngeli,anabwaga ung'eng'e kilatini spanich frech hapo ndio chenye,ngeli na ung'eng'e ni kitu kimoja-kiingereza
3.Beef,cow,kitimoto pork,kitimoto na pork ni kitu kimoja-nyama ya nguruwe
4.Mara vikaanza viboko,bakora,stick michalazo denti akiguna kidogo ticha ndio anatilia mkazoo weee,viboko,bakora,stick,michalazo yote yana maana moja yani fimbo
5.Kajazia haja kubwa,bambataa,taarabu anayo,yani maneno yote hayo yana maana moja ya mkia wa kondoo
6.Mtoto natural color,chotara,mweusi mng'avu ng'avu maji ya kunde kaenda hewani sekunde,uso soft usio chunusi,demu huyo mmoja lakini chotara,maji ya kunde,mweusi,mng'avu ng'avu jamaa anajaribu kumuelezea binti katika angle zote.
7.Makostimetiks,vipodozi na vibwagayose.
8.Chechela segedansi nondo gereza inside ndete lupango kunapotekeza,yani mistali yote anazungumzia neno moja tu jela
~
Jamaa style yake imekaa poa sana ni sawa na temba lazima utasikia pilipili na kachumbali kwenye mistali yake.