Ujinga wa mwafrika

Mzee2000

JF-Expert Member
Aug 7, 2009
527
221
Watanzania tunawakaribisha wageni wanachimba madini yetu wanapeleka kwenye nchi zao wanaprocess hayo madini wanatengeneza vitu kama simu za mkononi silaha na hata vitu vidogo vidogo kama vijiko na umma halafu baadae wanakuja kutuuzia vitu hivi hivi kwa bei ya hata mara tano ukilinganisha na waliyotupatia kuchimba madini yetu. Mwishoni mwa huu mzunguko tunajikuta tumepata hasara kwa sababu tumekwisha nunua malighafi zetu (ingawa mara hii zinakuwa zina sura tofauti) mara tano ya bei inayotakiwa.

Serikari za nchi nyingine duniani zinatoa mikopo kwa wazawa wa nchi zao kuanzisha viwanda vya kuzalisha kutoka kwenya malighafi zilizopo katika nchi zao,hii inasaidia sio tu kuleta ajira bali kuleta ujuzi hasa katika research and development.

Je serikari ya Tanzania ina mpango wowote wa kuimarisha / kuanzisha viwanda vya kusindika madini yetu? Hapa namaanisha strategy au policy maalum?

Ukweli ni kwamba hata tukigundua madini ya uwingi wa namna gani kama tunawauzia wageni wana process na tunanunua finished goods kutoka kwao tena kwa bei kubwa zaidi ni kazi bure ni bora tukae na madini yetu

Ndio maan na uliza, je hatujaliona hili?Au ndio huu ujinga wetu?
 
......................................................................
.................................................................
bump
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom