Ujinga wa MIGA, noah na CHADEMA

Ujinga wa MIGA, noah na CHADEMA

Na je, ingekuwa China wale walioiuza nchi hii kwa tamaa za matumbo yao, wale walioingia mikataba ya hovyo wangefanywaje?
 
Eti tunamtegemea Prof. Kibudu aridhiane na wazungu kwa niaba yetu. Pumbavu kabisa. Tumekosa vyote sasa, si trilioni 425 za kodi wala zile $ mil. 300 za kujenga uaminifu. Sasa CCM na Dikteta wao wamebaki kupayuka tu huku wameinamia chini kwa aibu mithili ya msukule aliyefumaniwa. Pumbavu kabisa, ziko wapi Noah zetu!?
Mkuu hapo vipi?
 
Anaandika mtanganyika halisi kuhusu kuropoka kwa wakili msomi na mahiri,post hii imfikie hukoNairobi

Lilipoanza sakata la makanikia kati ya kampuni ya Acacia na Serekali ya Tanzania na hatimae kulazimisha mwenye hisa kuu kampuni ya Barrick Ltd kubeba dhamana ya kutafuta suluhu alitokea anayeitwa WAKILI MAHIRI na kudai mambo mawili yote yakitaka serikali isizuie mali zilizokuwa zikitoroshwa. Hoja zake kuu zilikuwa mbili:

1. Kuna kitu inaitwa MIGA. Kwa kukurupuka kwake akaelezea MIGA kama Convention na hapohapo akatoa kirefu cha MIGA ambacho kinaonyesha MIGA ni Agency. Ukweli ni kuwa MIGA ni Agency. Ni taasisi ya arbitration (kutafuta suluhu).

MIGA si conventiom (Mkataba) kama alivyoropoka. Convention au Treaty au Agreement hufikiwa chini ya usimamizi wa au kwa niaba ya UN (Umoja wa Mataifa) au Kikundi cha Nchi. Mifano: ILO Convention on Freedom of Association and Collective Bargaining, UN Treaty on Non Proliferation of Nuclear Weapons, UN Framework Convention on Climate Change, UN Convention on Combating Deforestation and Desertification? Iran Nuclear Treaty, East Africa Treaty, etc.

Convention inaridhiwa kati ya nchi na nchi (Parties). Hata ICC japo ni taasisi msingi wake ni TREATY na waliohusika si kampuni bali nchi.

Kwa hiyo WAKILI MSOMI alikosea aidha kwa kutojua, kwa makusudi au kwa jazba kusema MIGA ni convention. Ni ishara ya uelewa finyu sana kuhusu CONVENTIONS. Inatia shaka sifa ya USOMI MAHIRI ikiwa WAKILI MAHIRI hajui CONVENTION ni nini!

2. WAKILI MSOMI alidai kisheria kuna madini SI MALI YA NCHI bali MALI YA MWEKEZAJI. Akimaanisha kuwa kitendo cha kuzuia mali ya mwingine ni uvunjifu wa sheria za kimataifa au makubaliano chini ya MIGA. Matukio ya BARICK kukubali kukaa meza moja na serikali ni ushahidi tosha kuwa MWANASHERIA MAHIRI alikuwa hajui asemacho, aliongopa au aliropoka. Ambaye alitaka tuamini tumezuia mali yake kakubali ana mapungufu na atayasahihisha. Ni ajabu na kioja ambaye tuliambiwa tunamdhulumu atende hivi!

Hoja zote mbili zimeingia shombo. Ingefaa sana MWANASHERIA MAHIRI angetueleza ni vipi MIGA haikutubamiza kama alivyoonya? Ni vipi alotuambia tunamdhulumu kwa kumzuia asiuze madini kaja kutafuta suluhu?

Hizi hadithi za kuwa kila mtu aliahidiwa Noah, tumepunjwa au waliongia mikataba washitakiwe ni njia ya hovyo ya kufunika fedheha!

Hivi tungefuata ushauri wa MWANASHERIA MAHIRI wangejadili vipi kupunjika? Wangepata vipi hizo Noah kwa kuachia madini yaibwe?

Hivi ingekuwa China MWANASHERIA MAHIRI angebaki salama? Yaani Rais atetee madini yasiibwe utoke huko na joho lako jeusi umwambie ACHA TUTASHITAKIWA tena upotoshe bado wakuache?

Watanzania wengi tunasema hata kama raisi angeokoa nusu kilo ya dhahabu TUKO PAMOJA NAYE

Wanaosubiri NOAH kila mtu yake huku wanasoma ALBADIRI na waendelee kusubiri.

TANZANIA KWANZA MADINI YETU KWANZA NOAH BAADAE
Meli ya Samaki
 
1.... Inatia shaka sifa ya USOMI MAHIRI ikiwa WAKILI MAHIRI hajui CONVENTION ni nini!
2. ...Matukio ya BARICK kukubali kukaa meza moja na serikali ni ushahidi tosha kuwa MWANASHERIA MAHIRI alikuwa hajui asemacho, aliongopa au aliropoka.
1. Hoja ya kwanza unazungumzia definition ya MIGA. Sijui ina msaada gani kujua definition. Nilitegemea ungezungumzia majukumu yake zaidi
2. Hoja ya pili unazungumzia kukubali kwa Barick kufanya mazungumzo kuwa kunadhihirisha kuwa hawawezi kupeleka kesi mahakamani. Nadhani umesahau kuwa hata mibaba ikiwapa ujauzito wanafunzi, kuna kesi nyingi tu zimemalizwa kifamilia. Hii haimaanishi kuwa familia za wanafunzi hazina hoja za kisheria za kufungua kesi
 
Matukio ya BARICK kukubali kukaa meza moja na serikali ni ushahidi tosha kuwa MWANASHERIA MAHIRI alikuwa hajui asemacho, aliongopa au aliropoka.
Bila kuangalia unapiga debe upande gani, Barick kukaa na serikali ina maanisha wana interest zao wanazotaka kuzilinda na sio kwamba TL hajui asemalo, au aliongopa/kuropoka yeye alichotoa no tahadhari. Jiulize kwa nini wakati mazungumzo yanaendelea kati ya Bariki na SJMT, Acacia wametoa notes za kupeleka shauri hili mahakamani. Hawa jamaa wanatumia a parallel road strategy-maungumzo yashirikishe Barick na uamuzi watakaoridhia ni Acacia (independent board), na mahakani Acacia wenyewe (hii option wameiweka open kama hawatakubaliana na mapendekezo yatokanayo na mazungumzo). Piga tafakuri tena.
 
1. Hoja ya kwanza unazungumzia definition ya MIGA. Sijui ina msaada gani kujua definition. Nilitegemea ungezungumzia majukumu yake zaidi
2. Hoja ya pili unazungumzia kukubali kwa Barick kufanya mazungumzo kuwa kunadhihirisha kuwa hawawezi kupeleka kesi mahakamani. Nadhani umesahau kuwa hata mibaba ikiwapa ujauzito wanafunzi, kuna kesi nyingi tu zimemalizwa kifamilia. Hii haimaanishi kuwa familia za wanafunzi hazina hoja za kisheria za kufungua kesi
Ukiwaza sana unaweza kuishia kutumia lugha kali-mchango wangu #33 unaonyesha bila chenga ushabiki wa Trump. Nimeijibu hiyo point yake ya pili #46 lakini mfano wako hapo juu ni jibu bora. Mleta maada hakufanya home work yake vyakutosha.
 
Endeleeni kudai kwa mujibu wa invoice ya TRA ya tshs trilion 400 ndio mtajua definition ya MIGA, na sio kuchukua hako kahela ka posa kwa linchi tajiri kwa mujibu wa Pombe

Hawa watu ni wa ajabu sana wanaleta maneno mengi sana kutetea ushindi wa $300 lakini wanajisahaulisha kuwa walikuwa wanadai trilioni ngapi. Hawasemi zimeshukaje, hawasemi maprofesa walifanya estimates zao kwa makosa makubwa kwa kuelewa au kutoelewa. Hatubezi kilichopatikana lakini tuwe wakweli tulikosea na tulichopata na tumepata kwa kubahatisha ndio maana tumeshusha bei kiasi hicho mpka tumewafutia na kosa la wizi au udanganyifu.
 
Lakin najiuliza swali.lissu alipngea haya ili iweje sasa?

Inafika hatua unajiuliza wanasiasa wengine dhamira yao ni ipi,

Tutashitakiwa MIGA?????

Serious na unajiita mwanasheria nguli???

Maguful is so smart ,


Kabla hujatoa povu chini tuambie tunashitakiwa lini??

Kuna wanasheria wapiga kelele kwa kutaja vifungu vya sheria, watu wakisikia ibara zinatajwa tu wanaanza eti mwanasheria nguli, shit
 
Back
Top Bottom