‘Ujinga’ wa CHADEMA na Katiba Mpya

kwani wana ccm siyo sehemu ya wananchi
Kuna sehemu nimesema Wana CCM siyo sehemu ya mwananchi? Ila yule mjinga anaefanya vitu vya kijinga regardless ya Chama na sehemu anakotoka lazima tumchukulie kama mpumbavu.
 
Kuna sehemu nimesema Wana CCM siyo sehemu ya mwananchi? Ila yule mjinga anaefanya vitu vya kijinga regardless ya Chama na sehemu anakotoka lazima tumchukulie kama mpumbavu.
Kigoma walimu baadhi walikataa kuwakilishwa na cwt,huu ni mfano tosha wa mtu kuwa huru,na walijiuna na chama kingine na ndiko upidhani wa kweli unapotokea,chadema inapaswa kushirik na kuunda taasisi hizo na kuzisajiri na kupewa michano ki sheria ,tatizo mboe hana akili
 
kwani wana ccm siyo sehemu ya wananchi
Sasa chadema wanaamini wananchi ni wao tu, na ndo wana haki katiba iandikwaje,
Hawaekewi simple fact ni kwamba hawana majority.

Katiba huandikwa na kupitisha na majorities, haijalishi hiyo katiba, inataka nchi iwe ya kifalme, vyama vingi, kimoja, au bila vyama, majority wakipitisha, hiyo ni katiba halali.

Ndio maana nasema, mwisho wa siku, CHADEMA watatia mpira kwapani, maana wao wanataka katiba, anayotaka mr Lisu😂😂🙆‍♀️
 
asante mzeee
 
Chadema hawawezi kulazimisha kitu sio mahitaji ya wananchi. Nchi hii ina bahati ya kua na umoja wa wananchi wake. Ni rahisi wao kuona kitu hawahitaji au kugundua kitu wanataka kubambikiwa tu.

Katiba mpya sio hitaji lla wananchi ila chadema baada ya kujikuta hawana agenda kimkakati wakarukia agenda ya katiba.

Tukirejea nyuma chadema walikua na agenda ya kuweza kuibwaga ccm madarakani. Agenda ya ufisadi na rushwa. Kutokana na uwezo wa CCM kujirekebisha wakaja na jibu kupitia Magufuli.

Hapo wakawa wameipokonya chadema agenda ya kuweza kuwatoa madarakani.
 
Hongera sana mkuu,
 
Tatizo la baadhi ya ninyi ccm ni kudhani kuwa katiba inayoandikwa ni ya cdm na si ya wananchi. Sasa kama unajua udhaifu uliopo kwenye kupata uwakilishi sahihi, utakaowezesha kupata katiba bora ya wananchi, kwa nini usishauri namna bora mbadala itakayoondoa hiyo kasoro ili kupata katiba bora na badala yake unawalaumu cdm?! Kwa hiyo ndo kusema katiba bora wao ccm hawaitaki? Kwa nini huwalaumu ccm kwa ku capitalize kwenye udhaifu wa kimfumo walioujenga wenyewe kinyume cha sheria na badala yake unmlaumu cdm?!! Kama ccm hawaitaki katiba bora jiulize kwa nini? Kwa nini watake kitu kibovu kinachoumiza nchi na wananchi?

Jukumu la kuunda mfumo bora na sahihi wa kupata katiba bora ya nchi ni la wananchi wote wakiwemo ccm na cdm, huo ni wajibu siyo khisani.

Katiba mpya ni matakwa ya wananchi na ni lazima siyo ombi. Tatizo la baadhi ya ccm mmekariri kuwa mpaka muwaumize kwanza wanachi kwa virungu vya polisi ndo katiba ipatikane, kwamba pawepo na vurugu kwanza, wananchi waumizwe ndo katiba ipatikane. Ni tatizo la fikra za kitumwa za miafrika mingi.

Sasa ni hivi, kwa taarifa yako, katiba mpya ya Tanzania itapatikana bila kuumiza wananchi na bila kumwaga damu ya mwananchi yoyote. Acheni hila za kijinga za kuzuia matakwa ya wananchi. Mimba imeshafikisha miezi tisa, mtoto atazaliwa tu hata kwa operation ikibidi.
 
Liliundwa kisheria kwa kutumia sheria mbovu zilizozalishwa na katiba mbovu. Hila hazitasaidia.
 
Hivi chadema inaweza kuunda Chama cha waalimu Tanzania?

Au shirikisho la wafugaji wa chadema na lipewe usajili kabisaaaaa? Alafu lije liteuliwe kuwa na uwakilishi bunge la katiba
 
Hivi chadema inaweza kuunda Chama cha waalimu Tanzania?

Au shirikisho la wafugaji wa chadema na lipewe usajili kabisaaaaa? Alafu lije liteuliwe kuwa na uwakilishi bunge la katiba
kwa hamjui mbinu hadi mjiweke hadharani,tumieni akili ,mbona ccm wanaweza?
 
Hivyo vyama na asasi zenye mrengo wa Chadema atakayevipa usajili ni nani?
 
Nyerere hakupitisha mfumo wa vyama vingi. Badala yake, kwa kujua uhuni wa chama chake na uchakachuaji uliofanyika ili ionekane kuwa ni 20% tu ya Watanzania walitaka vyama vingi alijenga hoja. Kinyume na matarajio ya ccm Nyerere alitumia takwimu hizo hizo zilizochakachuliwa na chama chake kujenga hoja yake kwamba hiyo 20% ya wananchi wanaotaka vyama vingi wanayo haki ya kupata hicho wanachotaka. Mantiki ya Nyerere ilikuwa kama kweli wananchi walikuwa hawataki vyama vingine vya siasa isipokuwa ccm peke yake basi vyama hivyo vipya vitakavyoanzishwa havitastawi na vitakufa. Nyerere alifanya hivyo kwa sababu yeye ndiye aliyeasisi mfumo wa chama kimoja na baada ya kukaa nje ya madaraka aligundua kuwa mfumo huo wa chama kimoja haufai. Aligundua kuwa mfumo huo ulikuwa unatumiwa na watu wachache wenye madaraka kwa manufaa yao binafsi. Hivyo, alibaini kuwa alikuwa na wajibu wa kusaidia kusahihisha hilo kosa lililofanyika katika uongozi wake kwa nia njema lakini likaleta matokeo yasiyotarajiwa.
 
Shida ni kwamba, katiba haitolewi kama msaada,walio wengi ndo watapitisha katiba na itakua halali,, mfano mdogo tu, rasimu ya warioba, walishindana padogo sana,, serikali mbili au tatu.

Wengi kwenye bunge la katiba walitaka serikali mbili zoendelee,
Ukawa walikua wachache , wakataka serikali tatu, matokeo yake, kwasababu walikua wachache ikashindikana, wakasusa.

Lakini duniani kote, wengi ndio wanapitisha ajenda, na huwezi kususa eti uforce minority wapitishe ajenda,,
Hii labda itokee hapa bongo tu.

Duniani kote, democracy inaamua kwa kura, wengi ndio wanapitisha ajenda
 
Alichofanya nyerere ni fadhila,, sio democracy
 

Donald J Trump, anasema “katiba ndio mama wa nchi “
So kama The real Donald J Trump kaona katiba ndo kila kitu wewe ni nani ukatae???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…