Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,185
- 18,513
Nchi hii inaongozwa kwa kiki sana na vodafaster. Ni miaka mingi tulikua na tatizo la walimu, ikatoka proposal wanafunzi wote wanaomaliza kidato cha sita watafanya kozi ya mwezi mmoja na watakua walimu, ili kuziba pengo la walimu ,agenda ikapotezwa kimiujiza.
Tukaja na issue ya udom, tutakasema kwa kuwa tuna upungufu wa walimu basi tuwachukue wanafunzi waliofanya vizuri olevel wasome diploma 3 yrs kisha wakafundishe , sisonje akaitupilia mbali.
Kwanini tunapokuwa na tatizo tunakuwa wepesi wa kutafuta solution zima moto badala ya kupanga kuliondoa tatizo kimkakati.
Hii ndio sababu umaskini hautoki Tanzania kwa sababu viongozi hawaoni mbali. kila mmoja anataka kuona amefanya kitu.
Kiongozi mzuri ni yule anayepanda mti hali akijua kivuli chake hata kifaidi.
Nimesikia tunachukua umeme Ethiopia ili kutekeleza Sera ya viwanda, ina maana kelele zote za viwanda tulikua tunadanganyana, viwanda bila umeme wapi na wapi? umeme wenyewe ni wa maji walau ungekua wa nuclear.
Tanzania inaongoza Africa kwa kuwa na mito na maziwa mengi hadi bahari, shida IPO wapi kutekeleza miradi ya maji iliyopo kwenye mafaili ya tanesco?
Muhongo uliingia wizarani ukakuta kuna miradi lukuki ya umeme wa maji ambayo jumla yake inawezafikia zaidi ya MW 5000, ukaifuta na kuja na Sera ya umeme wa gas, huo umeme upo wapi na kwanini umekubali kununua kitu ambacho ulisema kimepitwa na wakati?
Nakaribia kuwa zuzu kwa sababu ya viongozi wasio na maono.