Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,618
UJINGA NDIO UMASKINI…
Nawaza sana pale ninapoangalia namna nchi yetu inavyotumia gharama kubwa kulipia vitu ambavyo tunavyo miaka nenda rudi.
Tafiti nyingi zimefanyika na kubaini mimea mingi inayotibu magonjwa mengi sana; lakini kwa sababu viongozi wetu wanasaini mikataba mibovu na makampuni yanayotengeneza madawa – wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha madawa yetu ya asili hayapewi kipaumbele. Nitoe mfano rahisi hapa. Kuna dawa ambayo inatumika kwa ajili ya kutibu maralia – ALU; Dawa hii inatengenezwa kwa mchanganyiko wa mmea unafahamika kama Artemisia. Umea huu unastawi vyema mikoa ya Arusha na Iringa. Kilo moja yam mea huu inauzwa Tshs. 100,000/=. Lakini utashangaa viongozi wetu wanaendelea kuweka mkazo kwenye mimea iliyoanzishwa na wakoloni; mimea yenye kutoa mazao yasiyo kuwa na soko.
Majuzi nilitembea kwenye supermarket nikakuta pakiti ya mbegu; kuchunguza ni mbegu za mzambarau. Nilipojaribu kumuuliza muuzaji - alinijibu kuwa wale wanaojua matumizi yake ndo wananunua. Nilipofika nyumbani nikaanza kufuatilia manufaa ya hizo mbegu. Nilishangaa kuona kwamba utafiti ulishafanywa miaka mingi kuwa mbegu hizo ni tiba sahihi ya ugonjwa wa kisukari. Mtaani mbegu hizo zimezagaa lakini kuna watu wanaagiza mbegu hizo toka Mashariki ya kati.
Kuna mengi yanayokumbatiwa na viongozi wetu ili waendeleze mahusiano mema na nchi nyonyaji lakini uhalisia ni kwamba nyuma ya haya yote kuna kukandamizwa na adui ujinga ambaye akishakomaa anabadilika na kuwa upumbavu.
Tetesi ni kwamba hata uzinduzi wa magari ya kutumia sola kwenye mbuga za wanyama umewauma wengi waliokuwa wametufanya sisi soko lao kuu la mafuta. Kauri ya rais wetu ya kwamba vita ya kiuchumi ni ngumu sana kuliko vita yoyote ile ni sahihi kabisa. JPM anafanya mazuri; swali la kujiuliza ni hili … “Akimaliza muda wake ni nani mwenye roho ngumu ya kuendeleza vita hii ya kiuchumi?”
Ikumbukwe kuwa miundo mbinu inayorejeshwa iliharibiwa na watanzania hawa hawa ili waweze kufanya biashara ya usafirishaji kwa njia ya barabara. Nasi asiyejua kuwa kipindi reli inafanya kazi kulikuwa na unafuu mkubwa wa kusafirisha bidhaa toka sehemu moja kwenda kwingine kwa gharama nafuu.
NINI KIFANYIKE?
Uhuru wetu tuutumie vizuri, mamlaka zinazosimamia shughuli mbali mbali wafike hatua watumie akili zao – wasitumie za kuambiwa tu. Ukienda Kagera kununua Kahawa unakutana na kachombo et indo kakupe kibali cha kununua kahawa. Ukitaka kufanya biashara ya nishati utakutana na Tanesco na figisu zake. Ukitaka kufanya biashara ya chakula na dawa utakutana na TFDA / TBS na figisu kibao. Ni wapi uliona mshindani kibiashara anamkaribisha mshindani wake kwa masharti rafiki?
Narudia tena - watanzania tutumie vyema uhuru wetu wa kufikiri, kutenda kwa usahihi na sio kutenda kwa maagizo ya makampuni ya nje ambayo kazi yao kubwa ni kuhakikisha Africa inaendelea kuwa mteja.

- Nchi yenye maporomoko ya maji inaendelea kuwa mteja wa mafuta kwa ajili ya kuzalisha umeme.
- Nchi yenye hali ya hewa safi (naongelea jua) inaendelea kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kulipia nishati ya umeme (badala ya kutumia sola)
- Nchi yenye mimea tiba kibao; inaendelea kuwa mteja wa madawa kutoka nje wakati malighafi za kutengeneza madawa hayo zinatoka hapa hapa.
- Nchi yenye miti mingi ya mbao inaagiza samani (furniture) za mavumbi ya mbao ambayo uimara wake ni sawa na hakuna.
- Nchi yenye misitu mingi inaagiza nguzo za umeme toka nje.
- Nchi yenye ardhi kubwa, maliasili ya kutosha inaagiza mayai, maziwa, n.k toka vinchi vidogo.
- Yapo mambo mengi ambayo inabidi sisi kama watanzania inatubidi kujichunguza.