Ujerumani, Ufaransa na Italia zasitisha chanjo ya Astrazeneca

Kila dawa ina side effects hii utakuta ni labda 2% wanaopokea ndio wanapata kuganda kwa damu. Ukifanyika utafiti kwa kina tutajua nini hasa kinaendelea. Ila nawapongeza Waingereza wanapokea chanjo kwa rate kubwa tofauti na wenzao wa Ulaya
Ili vaccine iwe effective inatakiwa iwe developed kwa muda gani wataalamu wa MUHAS si wamo humu watueleze...maana naona hii imeundwa kwa muda mfupi sana!? Inatia shaka kidogo
 
Ili vaccine iwe effective inatakiwa iwe developed kwa muda gani wataalamu wa MUHAS si wamo humu watueleze...maana naona hii imeundwa kwa muda mfupi sana!? Inatia shaka kidogo
Yani unataka MUHAS wasome madaftari waje kutupatia majibu hapa. Simply ni kwamba hakuna muda rasmi wa kuwa na vaccine, huwezi kuwa in distress call ukaleta sababu za kusubiri muda.

Chanjo zimepewa emergence approval na hazina patents ngumu ndio maana India anatengeneza chanjo zaidi ya moja kwa reseni. Alafu hii AstraZeneca ni moja. Zipo Pfizer, Johnson's & Johnson's, Moderna, Sinovax, Sputnik V na zote hazina shutma hizi. Tatizo ni effectiveness katika age groups na kwenye variants za kirusi hiki. Watatumia hizo nyingine kama vipi

Hata vitani wanakuwa na silaha zinajaribiwa miaka kadhaa wakati wa amani ila vita ikitokea leo kuna silaha zitaundwa mwezi huu na zitumike mwezi huu bila trial. No time to die
 
Usiwe kilaza., pamoja na watu 17 kuganda damu wamesema wamemtaka wakala wa udhibiti wa dawa wa Ulaya kuchunguza, likely jibu litatoka kama waendelee au la kwa vile milioni 17 tayari washachomwa.

Sasa Tz na nyinyi angalau mungezipokea hizo chanjo kwa kuzichunguza kwanza halafu ikionekana kama zinafaa kwa afya zenu au la, lakini huwezi kukataa moja kwa moja na kuendelea kujifukiza na kunywa limao ambalo nalo pia kisayansi halijathibitishwa, kuna watu wengi wanasema ukinywa limao presha inashuka ambalo nalo ni tatizo kwa mwanadamu.

Kama chanjo hamtaki basi wataalam mnao kwa nini hamtengenezi chanjo zenu TanZaneca mukaokoa watu wenu ambao sasa kuna gumzo kubwa kuathirika kwa watu mbali mbali na wengine kupoteza maisha kwa corona ?
Wewe ndo kilaza.Hujui kuhusu serikali kuunda tume ya kuchunguza ufanisi wa hii chanjo???.
 
Wewe ndo kilaza.Hujui kuhusu serikali kuunda tume ya kuchunguza ufanisi wa hii chanjo???.
sijuw unaishi dunia ipi, Serikali imetangaza hawatapokea chanjo yoyote toka nje maana zina madhara utachunguza vipi kitu ambacho hujakuwa nacho? hiyo tume iko wapi na inachunguza nini toka muliposema mnachunguza zile dawa za mitishamba toka Madagascar mpaka leo hakuna jibu? pokeeni kwanza hizo chanjo ndio mchunguze.,
 
chief. Chanjo hii ikija hivi sasa, uko tayari kuchanja?
 
chief. Chanjo hii ikija hivi sasa, uko tayari kuchanja?
Unajua majirani zenu Kenya wamepokea awamu ya kwanza kwa watu ambao wako hatarini zaidi kuanzia umri wa 50 kwenda mbele ndio kipaombele na tayari wameanza kupiga sasa na Tanzania kwanini wasianze kuhurumiwa hao wazee wetu ambao kwa kiwango kikubwa ndio changamoto hili korona linawabana
 
Naelewa chief, swali langu wewe uko tayari kuchanja?
 
Naelewa chief, swali langu wewe uko tayari kuchanja?
Kama kipaombele kwa wataalamu wetu kwa umri wangu wala hakuna shida, iam ready. Lakini ni ujinga kwamba katika nchi wapo wapo binafsi wana interest kuchanja kwa hiyari lakini wanazuiwa
 
Mnajidanganya bure, Italy muda si mrefu watarudi kwenye lockdown. Wakifuatiwa na France na Germany. Wote hao wametumia mchanganyiko wa chanjo za aina mbali mbali.

UK inaongoza kwa kuchanja watu wengi, lakini mpaka leo hii, kuna maeneo ambayo maambukizo yanaongezeka. Waliotengeneza chanjo, wahajaanza hata majaribio kwa watoto wa chini ya miaka 16, ambao ndio wasambazaji wakubwa kwasababu hawaheshimu rules of social distancing na wengine hawaonyeshi dalali za kuumwa wakiwa wameambukizwa.
Sawa. Israel je?
 
Sawa. Israel je?
Hata huko Israel maambukizo yanaongezeka kutokana na mdudu wa Corona kujibadilisha mara kwa mara. Kitu ambacho Israel hawasemi, ni watu wangapi wamepata maambukizo baada ya kuchanjwa? Hawatoi takwimu hizo kwasababu ndio mkataba wao na kampuni za madawa kuwa hiyo ni siri yao wawili.

This is phase 2!
Wait for phase 3 itakayopita dunua nzima tena km ile ya kwanza ya mwaka Jana!
Mpk dunia itakapojua kuwa yupo Mungu aliyeiumba!
Mpk turudi magotini!
 
Unajua maana ya mjadala?
Ebwana BAK eee hawa mataga wanavimbisha vichwa vyao na kujiona wajanja wakati mwenyekiti wao yuko hoi na hii hii Corona. Kama angekubali chanjo labda ingemsaidia sasa wanachukulia iyo changamoto ya watu 17 tu kuhitimisha kuwa chanjo hazifanyi kazi. Wakati hata utafiti wenyewe hakuna, eti kwa sababu ujerumani na ufaransa wamesitisha na wao wanapita umo umo.

Mataga bwana
 
Huyu msamehe bure hawa ndo wale ambao bado wamepagawa baada ya kibaraka wao mkuu kwa beberu kuchezea kichapo.....atasapoti chochote cha mlengo ule
Kwa hiyo wewe mkuu unafurahia mwenzako kupigwa risasi? Angekuwa ni baba'ko ungeandika huu ujinga hapa?
 
Back
Top Bottom