Ujerumani kusaidia jwtz hadi 2024

Ujerumani kusaidia jwtz hadi 2024

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555
1093636



SERIKALI ya Shirikisho la Ujerumani kupitia Mpango wa Kusaidia Majeshi Ra - ki, imekubali kuongeza kipindi cha kutoa misaada kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa miaka minne zaidi kuanzia mwaka 2021 hadi 2024, ambako pamoja na mambo mengine itajenga hospitali kubwa ya kijeshi yenye kiwango cha “Level 4” mkoani Dodoma.

Balozi wa Ujerumani nchini, Dk Detlef Wäechter akiwa na ujumbe kutoka Wizara ya Ulinzi na ya Mambo ya Nje ya Ujerumani, ametangaza uamuzi huo Ikulu jijini Dar es Salaam jana, alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli.

Pamoja kujenga hospitali hiyo, Dk Wäechter alisema katika ushirikiano huo, Ujerumani kupitia timu ya Ushauri ya Wataalamu wa Kijeshi (GAFTAG) itaongeza mafunzo na vifaa vya ulinzi wa amani, itaendelea kufundisha madaktari wa jeshi na kutoa vifaa vya matibabu na kutoa mafunzo ya ulinzi wa amani.

Katika ushirikiano wa sasa utakaoishia 2021, kati ya Juni 2017 na Machi 2019, Ujerumani imejenga Hospitali ya Kanda Monduli mkoani Arusha ambayo imewekewa vifaa tiba vinavyotumia teknolojia ya kisasa na itakayotumiwa kama Hospitali ya Rufaa ikisaidiana na Hospitali ya Kijeshi ya Lugalo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu Sh bilioni 5.94 ambazo Sh milioni 346.8 kati yake zimetolewa na Serikali ya Tanzania. Ufadhili mwingine uliotolewa ni upanuzi na uboreshaji wa Chuo cha Sayansi na Tiba cha Lugalo, ujenzi wa karakana za jeshi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Shinyanga na Mwanza, ujenzi wa idara ya dharura ya Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, ujenzi wa mabweni ya wanafunzi katika Hospitali ya Kanda iliyopo Bububu - Zanzibar, uboreshaji wa Hospitali za Kanda zilizopo Zanzibar, Mbeya, Mwanza na Tabora, msaada wa magari na vifaa tiba.

Rais Magufuli aliishukuru Ujerumani kwa kuendeleza na kukuza uhusiano na ushirikiano na Tanzania na alimhakikishia Balozi Wäechter kuwa Serikali ya Tanzania itahakikisha misaada yote inayotolewa inaleta manufaa yaliyokusudiwa
 
Ni msaada maana hata kama unachosema ni sawa,wan hiyai ya kurudisha au kutorudisha
vyovyote vile lakini sio msaada walicho chukua ni kingi ndio maana Ujerumani imejengeka..Ata warudishe vipi hawawezi kufikia thamani walicho chukua
 
One sided story.

What are they getting in return, arms sales contract?

These things remain secret in the third world

The day opposition people are in charge of parliament's defense and foreign affairs committee we won't be blindfolded again
 
Hivi umerogwa na nani mpka unakuwa "jinga jinga hivyo" jiongeze we ni mtanzania kwanza.
One sided story.

What are they getting in return, arms sales contract?

These things remain secret in the third world

The day opposition people are in charge of parliament's defense and foreign affairs committee we won't be blindfolded again
 
Hivi umerogwa na nani mpka unakuwa "jinga jinga hivyo" jiongeze we ni mtanzania kwanza.

naamini hukunielewa, ngoja nirudie kwa Kiswahili

nilimaanisha habari hii haijakamilika, haituelezi Wajerumani wao wanapata nini katika hili dili. Je, wanatafuta mkataba wa kutuuzia silaha?

na nikasema haya mambo kwenye dunia ya tatu huwa yanafanywa siri lakini siku ambayo wapinzani wanachukua kamati ya bunge ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje mambo haya hatutafichwa tena. Mwisho wa tafsiri.

Sasa hapo nani ni Mzalendo kati yetu, mimi ninaetaka kujua Wazungu wanatuingiza mkenge gani au wewe usiyeelewa mambo ya kimataifa unaniita mimi mjinga wakati upeo wako ni wa muuza ulanzi?

Mzungu hakupi kitu bure bure tu, kila kitu anafikiria kimiamala, transactionally! Wangekuwa wanatufa silaha bure basi! Get a clue, please, get a clue blockhead!
 
vyovyote vile lakini sio msaada walicho chukua ni kingi ndio maana Ujerumani imejengeka..Ata warudishe vipi hawawezi kufikia thamani walicho chukua

Ujinga wa Kitanzania, wachaga tuna akili sana, unaweza kuta Mzee anasema.shikamoo mwanangu, anaangalia anacholenga, a gain, ukiipata unalala mbele
 
Back
Top Bottom