UJERUMANI: Chama cha Soka chasikitishwa na uamuzi wa Ozil kutundika daluga

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
_102658456_ozil_getty2.jpg

Shirikisho la soka Ujerumani 'limekataa pasi na shaka 'tuhuma za ubaguzi wa rangi kutoka kwa mshambuliaji wa Arsenal Mesut Ozil lakini linasema huenda lingewajibika zaidi katika kuhakikisha mchezaji huyo hakunyanyaswa.

Ozil, mwenye umri wa miaka 29, alitangaza kujiuzulu katika soka ya kimataifa, akitaja "ubaguzi wa rangi na ukosefu wa heshima" ndani ya soka Ujerumani.

Mchezaji huyo wa kiungo cha kati amesema amepokea barua za chuki na vitisho na alilaumiwa kwa kushindwa Ujerumani katika Kombe la Dunia.

Limeongeza katika taarifa yake: "Tunakataa pasi na shaka kuhusishwa DFB na ubaguzi wa rangi. DFB limejishughulisha na suala la utengamano Ujerumani kwa miaka mingi."

Ozil alishutumiwa na DFB na katika vyombo vya habari Ujerumani baada ya kupigwa picha na rais wa Uturuki anayekumbwa na mzozo Recep Tayyip Erdogan katika hafla moja London mnamo Mei.

Alishutumiwa zaidi baada ya Ujeurmani kutolewa katika awamu ya makundi kwenye Kombe la Dunia.

DFB limekiri kwamba huenda halikulishughulikia suala hilo ipasavyo, likiongeza: " Inasikitisha kuwa Mesut Ozil amehisi hakulindwa vya kutosha dhidi ya kauli za kibaguzi."

Je yote haya yalianza vipi?
Ozil, ambaye kwa kizazi cha tatu ni Mjerumani mwenye asili ya Uturuki, alizaliwa huko Gelsenkirchen na alichangia pakuu ushindi wa nchi yake katika mashindano ya 2014 Kombe la Dunia.

Mweiz mmoja kabla ya Ujerumani kutetea taji lake, Ozil alikutana na rais wa Uturuki Erdogan pamoja na wachezaji wenza wa Ujerumani Ilkay Gundogan, mchezaji wa Manchester City ambaye pia ana asili ya Uturuki.

Baada ya hapo picha zilisambazwa na chama tawala cha Uturuki AK Party kuelekea uchaguzi katika nchi hiyo ambapo Erdogan aliibuka mshindi mwezi uliopita.

Wanasiasa wengine nchini Ujerumani waliwakosoa Ozil na Gundogan na kutilia shaka uzalendo wao kwa Ujerumani.

Ujerumani awali ilikuwa imemkosoa rais huyo wa Uturuki kutokana na kampeni yake dhidi ya wapinzani kufuatia mapinduzi yaliyofeli.

Wachezaji hao walikutana na rais wa shirikisho la soka Ujerumani kueleze kilichotukia, licha ya kwamba Ozil hakutoa tamko hilo hadharani kuhusu suala hilo hadi Jumapili.

Alisema Erdogan alikutana na Malkia wa Uingereza na waziri mkuu Theresa May akiwa England na akaeleza kwamba angekuwa amewakosea heshima mababu zake iwapo angekataa kupigwa picha pamoja na rais wa Uturuki.

Wajerumani waache figisu figisu za kumtafuta mchawi nani? Wajipange mwaka 2022 na kombe LA dunia la QATAR.
Maana kudiri na kina Mesut Ozil aitawasaidia chochote, Maana washafikia kwy kumarizia mpira wao, waandae kizazi cha umri wa kuanzia miaka 16 mpaka 20 kitakacho wasaidia 2022
 
Someni hayo malalamiko Instagram yenye kurasa kama 4,wajerumani ni wabaguzi sana,jamaa alivyoeleza bila shaka alibaguliwa.

Ozil anasema waliposhinda kombe la dunia waliproud of him na kumchukulia kama mjerumani,ila walipotolewa anapewa lawama na matusi na kuchukuliwa kama mjerumani.

Ni sawa na alivyosema Trevor Noah kwamba "waafrika wamechukua kombe la dunia ",kauli ambayo waziri wa ufaransa alikipinga na kueleza ni wafaransa wenye asili ya Africa.
Trevor akajibu tena,yule raia aliyemwokoa mtoto kwenye gorofa alipewa uraia kwa sababu alimwokoa mtoto ambacho ni kitu kizuri na kusema ni mfaransa,mtoto angemdondosha mtoto kwenye hali ya kuokoea je angepewa uraia?wangesema ni mwafrica.
 
Ozil kayataka mwenyewe, kachanganya siasa na mpira, hata hivyo ashukuru kuitwa timu ya taifa mwaka huu, kwani kiwango chake ni kibovu ukilinganisha na yule Ozil wa 2010 pale bondeni
 
Huyo ozil chuki ilianza alivosambaza ile picha akiwa na rais wa uturuki ambaye Huwa haiv na serekali ya German Ukiwa mchezaj jiepushe na siasa

Musiwe Watumwa Wa Kikoloni Mukahisi Kila Anachoongea Mzungu Ni Sawa!

Iwapo Ujerumani Wangelishinda Kombe la Dunia la 2018 je Wangeliibua Huu Mgogoro Wa Ozil?

Kwanini Raisi Wa Chama cha Soka Cha Ujerumani ndiyo awe Mstari Wa Mbele Kumtuhumu Ozil?

Je Kuna Uhusiano Gani Kwa Ozil Kupiga Picha na Erdogan na Kuvurunda Kwenye Michuano?

Je, Wale Wamarekani Wenye Asili Ya Tanzania Kupiga Picha Na Kikwete wakati Yupo Madarakani Ni Siasa? Walipaswa Wamkatalie na Kumkimbia?

Iwapo Rais Magufuli atataka Kupiga Picha na Yussuf Paulsen Wa Denmark, Yussuf itampasa Akatae na Kuondoka ili isiwe siasa?

Ukweli Ni Kwamba Ozil Kabaguliwa Kutokana na asili Yake.
*Wanaposhinda Kombe (2014) → Yeye Ni Mjerumani.
*Wanaposhindwa (2018) → Yeye Ni immigrant.

Sababu Kubwa Hapa Ni Kwamba Wamemfanya Ozil Kuwa Ni Scapegoat Kwa Kushindwa Kwa Ujerumani Kwani Tatizo lao Limeanzia Kwa Kocha Joachim Low Kutokufanya Uchaguzi Sahihi Wa Wachezaji.
Na Chama Cha Soka Kinawajibika Kwa Kutokuwa na Matayarisho Ya Uhakika Ya Timu. Ili Kocha na Chama cha Soka Kujiepusha na Lawama ikiwemo Kutimliwa Kwenye Nafasi Zao, Basi Wameamua Kujificha Nyuma Ya Mgongo Wa Ozil ili Wadau na Mashabiki Wa Ujerumani Waelekeze Lawama Kwa Ozil badala Ya Kwa Viongozi Wa Timu.

Wajerumani Wakubali Matokeo tu na Wala Wasimsukumie Mtu Mmoja Kwa Kufeli Kwao World Cup Kwani Kikosi Kilikuwa na Wachezaji 25 iweje Mchezaji Mmoja ndiye Kasababisha Kutolewa Kwao?

Ni Jambo la aibu na lisiloingia Akilini Kusema Ujerumani Wametolewa Mapema Kombe La Dunia Sababu eti Ozil Kapiga Picha na Raisi Wa Uturuki.

Ozil yupo sahihi wajerumani wabaguzi,mechi ya kwanza tu kombe la dunia walipofungwa media mbalimbali zilitoa taarifa kwamba kuna ubaguzi unaikabili kikosi cha German,kikosi ina pande mbili,kuna wajerumani wazaliwa na wajerumani wahamiaji,wale wahamiaji walikuwa wanabaguliwa ingawa wana vipaji.Ozil yupo sahihi kabisa wala siyo lawama baada ya kombe kumalizika,ilashaanza siku nyingi
 
Ukweli Ni Kwamba Mwaka 1998 France Walishinda World Cup kwa Kusaidiwa Kwa Kiasi Kikubwa Na Wachezaji Wenye Asili Ya Kiafrika.

Lakini Mwaka 2002 walipoboronga Hatukuona Wachezaji Hao Wenye Asili Ya Kiafrika Kutupiwa Lawama badala Yake inawathamini Wachezaji Hao na Kuwaenzi Kama Zidane na Henry.

France hii hii marahii 2018 imebeba Ubingwa Kwa Kusaidiwa na Wachezaji Wengi Wenye Asili Ya Kiafrika.

Ujerumani pia ni Timu iliyosaidiwa Sana Na Wachezaji Wenye Asili za Kigeni (Klose na Podolski wenye Asili ya Poland, Boateng, Khedira, Sane wenye Asili ya Kiafrika, Ozil anf Guandogun wenye Asili ya Uturuki) lakini Haiwathamini wachezaji Hao na Mpaka leo Haiwahesabu Kuwa Ni Wajerumani bali inawahesabu Kuwa ni Wahamiaji.

Mfano Mdogo tu Kocha Alipomuacha Leroy Sane Watu Wengi Walichukulia Kuwa Kaachwa Kimpira tu, Lakini Ukweli ni Kuwa Kaachwa Kiubaguzi Kwani Kina Draxler Waliochukuliwa kwa Utaifa Wao ni Wachezaji Wasiofaa Hata Kuchezea Kikosi B cha Ujerumani.
 
Musiwe Watumwa Wa Kikoloni Mukahisi Kila Anachoongea Mzungu Ni Sawa!

Iwapo Ujerumani Wangelishinda Kombe la Dunia la 2018 je Wangeliibua Huu Mgogoro Wa Ozil?

Kwanini Raisi Wa Chama cha Soka Cha Ujerumani ndiyo awe Mstari Wa Mbele Kumtuhumu Ozil?

Je Kuna Uhusiano Gani Kwa Ozil Kupiga Picha na Erdogan na Kuvurunda Kwenye Michuano?

Je, Wale Wamarekani Wenye Asili Ya Tanzania Kupiga Picha Na Kikwete wakati Yupo Madarakani Ni Siasa? Walipaswa Wamkatalie na Kumkimbia?

Iwapo Rais Magufuli atataka Kupiga Picha na Yussuf Paulsen Wa Denmark, Yussuf itampasa Akatae na Kuondoka ili isiwe siasa?

Ukweli Ni Kwamba Ozil Kabaguliwa Kutokana na asili Yake.
*Wanaposhinda Kombe (2014) → Yeye Ni Mjerumani.
*Wanaposhindwa (2018) → Yeye Ni immigrant.

Sababu Kubwa Hapa Ni Kwamba Wamemfanya Ozil Kuwa Ni Scapegoat Kwa Kushindwa Kwa Ujerumani Kwani Tatizo lao Limeanzia Kwa Kocha Joachim Low Kutokufanya Uchaguzi Sahihi Wa Wachezaji.
Na Chama Cha Soka Kinawajibika Kwa Kutokuwa na Matayarisho Ya Uhakika Ya Timu. Ili Kocha na Chama cha Soka Kujiepusha na Lawama ikiwemo Kutimliwa Kwenye Nafasi Zao, Basi Wameamua Kujificha Nyuma Ya Mgongo Wa Ozil ili Wadau na Mashabiki Wa Ujerumani Waelekeze Lawama Kwa Ozil badala Ya Kwa Viongozi Wa Timu.

Wajerumani Wakubali Matokeo tu na Wala Wasimsukumie Mtu Mmoja Kwa Kufeli Kwao World Cup Kwani Kikosi Kilikuwa na Wachezaji 25 iweje Mchezaji Mmoja ndiye Kasababisha Kutolewa Kwao?

Ni Jambo la aibu na lisiloingia Akilini Kusema Ujerumani Wametolewa Mapema Kombe La Dunia Sababu eti Ozil Kapiga Picha na Raisi Wa Uturuki.

Hawa wazungu sometimes wanakuwaga kama machizi tu.
 
Acha hizo mkuu, naona umeongea kwa hasira sana, Ozil na ikey wameanza kuzomewa na washabiki wao kwenye mechi za maandalizi kabla hata ya mashindano hayajaanza.
Ki ukweli Ozil kiwango chake kipo chini, hata pale Arsenal amekuwa akilaumiwa mara kwa mara.
Kuhusu mawazo ya kikoloni, hivi waliomchagua kuchezea hiyo timu si wao wajerumani wenyewe? Na wanaomshutumu si wao wenyewe?
2010 Ujerumani haikuchukua kombe, mbona hakulaumiwa? Ile ni timu yao, hivyo wanahaki ya kumlaumu yoyote yule ilimradi hakidhi matakwa yao
 
Statistics zinapingana na wewe mkuu, tuache ushabiki maandazi, ozil bado ni key player kwa arsenal
 
Acha hizo mkuu, naona umeongea kwa hasira sana, Ozil na ikey wameanza kuzomewa na washabiki wao kwenye mechi za maandalizi kabla hata ya mashindano hayajaanza.
Ki ukweli Ozil kiwango chake kipo chini, hata pale Arsenal amekuwa akilaumiwa mara kwa mara.
Kuhusu mawazo ya kikoloni, hivi waliomchagua kuchezea hiyo timu si wao wajerumani wenyewe? Na wanaomshutumu si wao wenyewe?
2010 Ujerumani haikuchukua kombe, mbona hakulaumiwa? Ile ni timu yao, hivyo wanahaki ya kumlaumu yoyote yule ilimradi hakidhi matakwa yao

Hapana! Hujaipata point tunayoiongelea nadhani... Inaonesha Bado Hujasoma Makala Za Kiongozi Wa Chama Cha Soka Cha Ujerumani Kuhusu Ozil Bali Umenijibu Kwa Kupitia Replies za Hapa!

Point Ni Kwamba "Hivi Ni Sahihi Kumbebesha Ozil lawama Zote Za Kutolewa Kwao World Cup?"

Kama Unafatilia Vizuri Raisi au Chairman Wa Bayern nilimshuhudia Akisema "Ni jambo Jema Kwa Ozil Kustaafu Kuchezea timu ya Taifa Kwani Kwa Miaka Mingi Hakuwa na Kiwango Cha Kuchezea Timu hiyo" Na akamlaumu Sana Kwamba Kiwango Chake Kibovu Kimepelekea Timu ya Taifa Kuboronga.

Raisi Wa Chama Cha Soka Cha Ujerumani yeye Amemhusisha Ozil moja Kwa moja Kuboronga Kwa Ujerumani na Kukutana Kwake na Erdogan! Kweli inaingia akilini?

Magwiji Wa Soka Wa Kijerumani wanaomkingia Kifua Joachim Low Kwa makusudi Kumfichia lawama Low basi nao Wanambebesha Ozil Lawama Za Kuboronga Kwa Germany ili asijelaumiwa Low.

Hivi na wewe unaamini Kuboronga Kwa Germany Ni Kwasababu ya Ozil?

Hivi Kama Ozil alikuwa na Kiwango Kibovu, Kwanini Asilaumiwe Kocha Kwa Kumchukua Ozil na Kuwaacha Wenye uwezo?

Hivi Kwani Ozil Ni Kama Nani Kwenye Timu Germany Hata awe Decider Wa Kuweza Kutoka au Kubakia World Cup?
 
Hapa umemlisha maneno huyo kiongozi FA. Embu soma link hapo chini kwa mujibu wa sky sport
https://www.google.com/url?sa=t&sou...AxAB&usg=AOvVaw34Wk8MyvxN4NFtXx0ZJN1s&ampcf=1
 
Last edited:
'Mesut created more chances in the 2018 World Cup per 90 minutes than any other player' this is one of them! sorry for "shabiki maandazi"
Ni kweli kabisa, Ila kumbuka hizo statistics ni za mechi dhidi ya south korea ambayo nayo walifungwa ukiangalia mechi dhidi ya Mexico ilikuwa sio
 
Sasa Mkuu si Umeleta Link Ya Huyo Jamaa Kukataa Kuwa Hakumbagua Ozil??
Ulitaka Akubali Kuwa Kweli Nilifanya ama?
Hata Kama Ungelikuwa Wewe ungelikubali Kosa?

Mambo mengine Jiongeze Mkuu tafuta Alichokisema Mwanzo Kabla Ya Kuleta Mrejesho Wa Kuyakataa aliyoyasema.
Mkuu nimekupa link ya alichokijibu, nawe nipe link ya hicho unachodai amekisema, naona utakuwa umechanganya mambo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom