SaaMbovu
JF-Expert Member
- Oct 8, 2013
- 6,028
- 5,359
Wana JF mimi binafsi naona ujenzi wa Uwanja wa Uhuru ambao bado unaendelea mpaka sasa japo kwa taratibu si wamuhimu sana. Kiukweli huwezi boresha viwanja viwili ambavyo vimepakana hapa nazungumzia Taifa na Uhuru wakati viwanja vingine ni vibovu mpaka TFF inavifunga. Taifa nakubali ni uwanja ambao una hadhi ya kuwa wa Taifa na mpaka uwanja wa Uhuru ulipokuwa katika Standard yake ilikuwa inatosha kabisa. Kilio changu ni kwamba gharama ambazo zinatumika kufanya matengenezo pale Uhuru basi zingetumika kukarabati viwanja vingine mikoani. Mikoa kama Arusha, Morogoro, Mbeya, Mwanza, Dodoma nk.. kuna viwanja ambavyo vikikarabatiwa nchi itakuwa na viwanja vingi vizuri na ambavyo vitasaidia kukuza soka nchini. TFF na CCM (inamiliki viwanja) jamani wekeni hata nyasi za bandia viwanja vya mikoani hayo ya majukwaa baadae. Ukiboresha viwanja hata mapato uwanjani yanaongezeka kwasababu watu wengi pia huvutiwa na mazingira. Mfano uwanja wa Taifa wengine hawendi kuangalia mpira bali hata jinsi uwanja ulivyo nk.
Mwana JF unasemaje kuhusu hilo?
Mwana JF unasemaje kuhusu hilo?