Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Chato uko kwenye taarifa ya waziri wa fedha na mipango?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,920
Sehemu ya taarifa ya waziri ni hii hapa chini:

Fedha zilizotolewa Julai – Novemba, 2016Katika kipindi cha Julai – Novemba, 2016 jumla ya Shilingi bilioni 9,481.260 zilitolewa na Hazina kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Shilingi bilioni 7,295.455 zilizotolewa kwa ajili ya matumizi ya Kawaida (ikijumuisha makusanyo ya Halmashauri Shilingi 61.047)

Mishahara ya Watumishi wa Serikali Shilingi 2,834.695,

Deni la Taifa Shilingi bilioni 3,552.249

Matumizi Mengineyo Shilingi bilioni 928.511

Shilingi bilioni 2,185.805 kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo (ikijumuisha makusanyo ya Halmashauri shilingi bilioni 91.571)

Fedha za ndani Shilingi bilioni 1,749.047

Fedha za nje Shilingi bilioni 436.758

Maeneo ya Msingi ambayo fedha zimeelekezwa

Matumizi ya kawaida yaliyopewa kipaumbele zaidi katika utoaji wa fedha kwa kipindi cha Julai – Novemba 2016 ni pamoja na:

Uboreshaji wa huduma za afya katika ngazi zote ikiwemo ununuzi wa dawa na vifaa tiba Shilingi bilioni 69.346;

Mitihani ya darasa la nne na saba Shilingi bilioni 33.745;

Mitihani ya kidato cha pili na nne Shilingi bilioni 31.051;

Posho ya chakula kwa askari wa vyombo vya ulinzi na usalama;

Chakula cha wafungwa Shilingi bilioni 7.5;

Mishahara ya watumishi wa Serikali;Elimu msingi bila malipo Shilingi bilioni 93.885 (kwa kutenga shilingi bilioni 18.777 kila mwezi);

Malipo ya posho na stahili mbalimbali kwa maafisa katika balozi zetu nje shilingi bilioni 23.127;

Ruzuku ya pembejeo shilingi bilioni 10.00;

Ununuzi wa chakula cha Hifadhi ya Taifa shilingi biliioni 9.00.

Deni la kuchapisha Vitabu vya Hati za Kusafiria Shilingi 2.569;

Uendeshaji wa vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge, Mkutano wa Bunge, Posho ya Jimbo kwa Wabunge pamoja na shughuli za Mfuko wa Bunge Shilingi bilioni 31,137;

Michango ya Taasisi na Jumuiya za Kimataifa Shilingi billion 8.833;

Ruzuku ya Vyama vya Siasa Shilingi bilioni 7.168;

Aidha, sehemu iliyosalia ya fedha za Matumizi ya Kawaida ilielekezwa kwenye shughuli za kila siku za uendeshaji katika Mafungu mbalimbali.

Matumizi ya Maendeleo yaliyopewa kipaumbele kwa kipindi cha miezi mitano ni pamoja na:

Ununuzi wa ndege mbili za Serikali Shilingi bilioni 103.386 na malipo ya awali ya ununuzi wa ndege 4 shilingi bilioni 91.533;

Usambazaji wa umeme vijijini Shilingi bilioni 266.493;

Ujenzi na ukarabati wa barabara Shilingi bilioni 335.931;

Usambazaji wa maji vijijini na mijini Shilingi bilioni 65.2445;

Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu Shilingi bilioni 210.758;

Mfuko wa Reli Shilingi bilioni 42.404;Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma na Mwanza Shilingi bilioni 12.353;

Ujenzi wa majengo ya utawala katika Wilaya mpya na Mamlaka za Serikali za Mitaa Shilingi bilioni 11.00;

Ujenzi na ukarabati wa ofisi za Halmashauri Shilingi bilioni 30.10;

Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo Tanzania bara Shilingi bilioni 9.0;

naUboreshaji wa miundombinu ya shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum Shilingi bilioni 2.5.


Sasa wadau mradi huo wa kiwanja cha ndege Chato mbona haunekani katika hiyo orodha?

Au huo mradi hauko katika orodha ya vipaumbele?

Mwenye uelewa atusaidie.
 
Back
Top Bottom