Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,272
- 21,448
Wana JF, nimekuwa nikijiuliza sana juu ya hii ahadi ya serikali kwamba reli ya kati itabadilishwa toka gauge ndogo iliyopo sasa na kupanuliwa kuwa kubwa standard gauge ambayo ni ya kimataifa. Kitu ambacho serikali haituambii ni kama hii reli ya standard gauge itakuwa mpya au itajengwa katika njia ile ile ya reli ya zamani, na nini kitafanyika kuhusiana na huduma za reli wakati wa kujenga standard gauge.
Kama standard gauge itajengwa katika njia/reli ya zamani, ina maana huduma ya treni za abiria na mizigo zitasimamishwa wakati wote standard gauge ikijengwa? Najua kwamba kujenga standard gauge katika njia mpya ni gharama kubwa, ambapo sidhani kama huo ndio mpango uliopo. Na pia, kumbuka kwamba tunapoongelea standard gauge ni kwamba hatuna mabehewa na locomotives za standard gauge, na hivyo hatuwezi kusema wakati tunaendelea kujenga standard gauge, huduma zinaweza kuendelea kule ambako tayari standard gauge imekamilika, kama tunavyofanya kwenye ujenzi wa barabara.
Nimeona niliongelee hili kwa kuwa ni kama suala la standard gauge linaongelewa zaidi kisiasa kuliko kiteknolojia. Kama kuna mtu ana majibu yanayoeleweka tafadhali tuelimishane.
Update
Ujenzi reli ya kisasa kigugumizi
By Fidelis Butahe,Mwananchi fbutahe@mwananchi.co.tz
Dodoma. Licha ya wabunge kushinikiza ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge), Serikali jana imeendelea kusisitiza kuwa haiwezi kujenga reli hiyo kwa kutumia bajeti yake, huku akishikwa kigugumizi kueleza mpango ilionao kuhusu ujenzi huo.
Akijibu hoja za wabunge kwenye mjadala wa mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali mwaka 2016/17, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema kama Serikali itatumia fedha za mfuko wa reli, ambazo ni Sh50 bilioni kila mwaka, itatumia miaka 320 kujenga reli hiyo.
Siku tatu zilizopita, wabunge wanaotoka kwenye mikoa ambayo Reli ya Kati inapita, waliungana kushinikiza ujenzi wa reli hiyo, wakisema bila ya Serikali kusikiliza kilio chao, watahamasishana ili waisusie bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.
Katika maelezo yake, Dk Mpango alisema gharama za kujenga reli hiyo ni kati ya dola bilioni saba mpaka tisa na nusu (Sh15 trilioni).
Alisema hata nchi ikitumia mapato yake yote ya kodi ambayo ni takriban Sh12 trilioni, kwa mwaka mmoja na miezi mitatu, reli hiyo itajengwa kwa miaka minne.”
Alisema mbali na uwezo wa Serikali kuijenga kwa mapato yake ya ndani, utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa, ili mradi huo uwe na manufaa kiuchumi, lazima matawi yake ya kwenda nchi za Burundi, Rwanda na DRC yajengwe. Alisema kama nchi itaamua kujenga reli hiyo kulingana na mawazo ya wabunge, nchi itakosa fursa kubwa kwa kuwa mzigo wa kwenye reli ya kati hautaweza kurudisha gharama ya ujenzi.