Ujenzi wa Nyumba: Je, ninaweza kujenga kanyumba kadogo kazuri kwa bajeti ya Mil. 6!?

Apr 7, 2016
55
31
Wadau, mafundi ujenzi, ninaomba msaada, ninayo ardhi kubwa sana, ila nimechoka kupanga na headaches za landlord. Nimejibana nikakuta nina milioni 6, je ninaweza kujenga ka nyumba kadogo
kenye atleast two bedrooms sebule ka jiko n.k. yaani niweze kujenga kumaliza kwa bei hiyo!?,

Asanteni!?
 
Wadau, mafundi ujenzi, ninaomba msaada, ninayo ardhi kubwa sana, ila nimechoka kupanga na headaches za landlord. Nimejibana nikakuta nina milioni 6, je ninaweza kujenga ka nyumba kadogo
kenye atleast two bedrooms sebule ka jiko n.k. yaani niweze kujenga kumaliza kwa bei hiyo!?,

Asanteni!?

Unaweza sana, especially kama kiwanja kiko flat.
 
Unaweza kwa kujenga ni kuezeka bati bila kusakafia
Unaweka milango na madirisha,pia ujue kuna bajeti ya choo na bafu
 
Hiyo nyumba itakuwa ni simple kupita kiasi. maana hapo gharama za nguvu kazi na ufundi pekee (kujenga, kuezeka, kufit madirisha milango etc.) inaweza kufikia nusu ya hiyo hela - sijui lakini, labda uwe eneo ambalo panapatikana cheap labour, uwe na tofali zako tayari, usahau masuala ya finishing yaani hata ripu usipige, choo kiwe cha shimo n.k. ..... Tshs. 6M bado kidogo, nakushauri ujitahidi zifikie walau 12, au jenga kwa awamu upate kitu kizuri.
 
Wadau, mafundi ujenzi, ninaomba msaada, ninayo ardhi kubwa sana, ila nimechoka kupanga na headaches za landlord. Nimejibana nikakuta nina milioni 6, je ninaweza kujenga ka nyumba kadogo
kenye atleast two bedrooms sebule ka jiko n.k. yaani niweze kujenga kumaliza kwa bei hiyo!?,

Asanteni!?
2 bedrooms, jiko,sebule hutaweza hata 10m haitoshi kujenga mpaka iishe.
 
tofali 1m
mbao mnazi 5k
bati 1m
milango 1m
madirisha 5k
fundi kujenga 6k
fundi bati 4k
mawe 4k
cement 6k

ongeza 3m unajenga nyumba ya vyumba 2 sebure choo na jiko kijijini kwetu.
10^5=k, na 10^6=m.
 
Aiasee usinikumbushe nimetoka kujenga nyumba sehem yenye landscaping matata imenigharimu balaaa....mpaka apo ilipo imegharimu 35m apo bado gypsum,na finishing yote kwa ujumla
 
Unaweza sana tu,lkn inategemea eneo.tumia tofali za kuchoma&uchome mwenyewe.tofali elfu kumi ni laki 2 mtu akikufyatulia.gharama za kuni ni laki 1.matofali hayo yanajenga vyumba 4-5.kujenga chumba kimoja ni laki moja.kuchimba mashimo shimo kubwa laki3+kujengea laki 2na nusu,hujaomba heri.shimo dogo laki 1na nusu kuchimba kujengea laki 1:Tofali za shimo kubwa+dogo ni laki 5 hv.madirisha yako 3 makubwa.sebuleni+vyumba 2 vya kulala.KWA HIYO PESA UNAJENGA&UNAHAMIA.
 
Huku Namtumbo unajenga,
Mvua zikikata unafytua Tofali za udongo.
Toka kufyatua hadi kuchoma ni 60Tsh.
Bati za msouth bando moja ni 19000 na zinakaa 10
Cement kwa ajili ya sakafu mfuko mmoja ni 16000
Labour charge ni low kwa huku.

Boriti ni 7500
So unaweza kukadiria ukubwa wa kimjengo chako
 
Ni ngumi sana kujenga nyumba kwa 6m angalau uwe na 15 hv ila usikate tamaa hicho hicho ulichonacho lianzishe kwani hata 1billion huanza na 1 sh.
 
Kwa hyo hela mkuu bado sana labda ujenge kwa hatua coz vifaa siku hzi ni ghali sana na labour charge nayo mafundi wanakomoa.Weka foundation yako complete then inua vyumba viwili halafu utakuja kumaliza mdogo mdogo as per your plan
 
sijajua mwenzangu upo wapi, mimi nipo Dar kiongozi kama upo Dar hizi data zaweza kukusaidia kidogo kuna mahala hapa Dar nina kishamba nataka kukitumia kwa kufuga miezi miwili iliyopita nikaamua nianze kujenga nyumba ya meneja wa shamba(Shamba boy) yenye Bed room moja, Sebure, jiko, choo na kistoo kidogo tu, nimeisha paua(bati mgongo mpana) nimeweka magrili, nimepiga plasta na fremu za milango yote tayari nimepachika, nimemaliza kupiga Gypsum, wiring na mifumo ya maji safi na taka tayari ila bado tiles top za milango na madirisha na finishing ya white cement na rangi yake, umeme nimeishalipia nguzo mbili, pesa imeisha katika nilikua na M15 kwenye akaunti na hii kazi imefanyika chini ya uangalizi mkali maana nilikua nipo likizo, nimeamua kiwe cha ubora huo ili hata kama hilo eneo nikiamua kulitumia kwa ajiri wa nyumba za kupangisha hata hiyo iwe sehemu ya hizo nyumba
 
Walio wengi wamekupa jibu al uongo kuwa haiwezekani, nasema ni uongo kwasababu wamekujibu bila kukuuliza mahali ulipo! Ukija Kijijini kwangu kule Maneromango unajenga vizuri kabisa mjengo very simple ila vyumba visiwe vikubwa vya kutisha, kwahio ili upate jibu sahihi lazima utueleze mahali ulipo ni wapi,..]]
 
Mkuu kujenga unajenga ila kwa m6 kuna vitu utamaliza katika nyumba ila kupaua utapaua ila finishing utaweza kamaliza kama milango ripu sakafu rangi cha msingi anza kujenga Na hiyo hiyo uku ukijibana utafanikiwa tatizo ata uwe Na hiyo m15 nyumba aitaisha kuna vitu vingi vya kuweka sawa anza kujenga uwe Na usongo Wa kuamia kwako itakufanya kuwa mbaili Na kuwekeza ela nyingi kwenye bajeti ya nyumba Na utafanikiwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom